Mfalme akasema atafutiwe vijana wenye akili na Maarifa

J Japo damu ya B's inakulilia unaanza kuwa na akili
 
Kwenye Yom Kippur makomandoo wa Misri waliuwawa kwa wingi mkubwa sana. Makomandoo wa Israel walishangaa kuona maiti zenye miili mikubwa, wakajiuliza inamaana kuwa komandoo Misri inabidi uwe umejazia? Nafikiri mkuu Tumaini anazungumzia meritocratic society, japo mfalme alikuwa ni wababeli si Israel lakini naona Israeli ya sasa kuwa ni pure meritocratic society. Kupima uwezo wa mtu pengine ndiyo kitu kigumu sana. Afya ni kigezo cha kuwa kwenye elite forces lakini siyo kigezo pekee, kuna IQ na saikolojia. Pengine usomi wa kuwa prof siyo kigezo pekee cha kuwa waziri kama alivyoonyesha mkuu Chige hapo.

Naunga mkono kuwa intelligence services ziwe na watu wenye uwezo kwelikweli japo kupata watu wanaokidhi vigezo vingi si kazi ndogo. Kiongozi asiye na uelewa hawezi kuchagua washauri wenye uelewa - Makaveli.
 
Zile za kwetu hazikuwa shule za vipaji zilikuwa shule za wanaopata maksi nyingi hata kwa cheating na kukariri.
 
Waisrael ni kabila moja lenye historia moja na kwa asiri wana maadui nje ya mipaka, na maadui hao wanatamani kizazi cha Israel kifutike. Mfano unaposema kabila fulani halitakiwi, unasababisha kabila hilo kuungana hata kama hawapendani.
Sisi ni makabila mengi, kwa lugha nyingine, sisi ni mataifa mengi yenye historia, mila na desturi tofauti tofauti, sisi ni taifa lililolazimishwa na mipaka ya kikoloni. Hatuna adui wa pamoja, hivyo kazi kubwa tuliyonayo ni kulazimisha makabila hayo kuwa taifa moja chini ya udhaimini wa CCM. Katika safarini hiyo tunajikuta tukijenga uadui ndani ya nchi yetu. Mungu Ibariki Tanzania.
 
Kabla hata hujaendelea. Mtu mwenye karama.ya kuona mambo.yatakayotukia miaka hata 50 ijayo huyo nabii. Iwe ni mcha MUNGU ama si mcha MUNGU.

Akiwa mcha MUNGU ataitwa mtu wa MUNGU na akiwa si mcha MUNGU basi ataitwa mwenye pepo la utambuzi
siku hizi tunamebarikiwa WACHA MBUZI na wana nguvu kuliko WACHA MUNGU
 
Daah sijui hata nisemeje, lakini ukweli ndiyo huu japo sidhani kama watakuelewa hawa watu maana wamevurugwa sana.
 
Mkuu hili la watu wenye akili ni dhambi kwa CCM, hawataki kabisa watu wenye akili na kama wapo basi siyo kwa Merit bali ni kuingizana watoto wa wakubwa ambao wanaweza kulinda mfumo. It's sickening...
 
nchi zetu ni masikini kwakua hata hatujui kwanini tunakuwa masikini, kila mtu anakuja na fantacy zake, mara usalama mara raisi n.k lakini ni ujinga mtupu.

huwezi kutatua tatizo ambalo haulielewi vizuri, utaishia kubahatisha bahatisha tu.
Huo ndio ukweli. Nchi hii imepata na kiongozi mmoja tu tangu tupate uhuru ambaye alikuwa visionary na alistahili kupanga Ikulu, Baba wa Taifa hili.
Ukiacha makosa madogo madogo ya kibinadamu aliyoyakiri. Huyu alijua alikokuwa anataka kuwafikikisha watanzania.
Awamu ya pili alipigania hali iliyokuwepo (status quo). Waliofuata hakuna makubwa waliofanyia taifa: mmoja aliuza viwanda na nyumba za serikali kwa bei chee. Mwingine akaandamwa na EPA, RICHMOND, na ESCROW.
Tulie naye hajui anachokifanya; mara mapato ya serikali; (alichukua hatua gani kwa makontena ya makonda?), madawati na madarasa, bombadier, serikali kuhamia Dodoma, SGR, Stieglers Gorge, nk. almradi ni kutapanya rasilimali zetu huku wananchi tunateseka.
Hata ujenzi wa kibanda cha mtu binafsi unazingatia uwepo wa pesa. Aidha, ni busara kukamilisha mradi kwanza kabla ya kuanzisha mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…