Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Duh! Yani hamu alimgegeda Mama yake? Mkuu, kitabu gani unasoma kupata hizo nadharia nami nikitafute?

Maana Mwanzao 9: 20 na kuendelea mbona inasema Nuhu alilewa kupindukia akawa hajitambui mwisho akakaa uchi ndo huyo Hamu akauona uchi wa Babake.

Pombe zilivomuisha ndo akatambua Hamu kamuona uchi na ndo laana ikaanzia hapo
 
Kumbukumbu la torati 27:20
20 Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina

Sasa hapa ndio watu wakaja na theory kwa kuwa musa alisema mtu akilala na mamake amemvua babake nguo basi wakaconclude ham alilala na mamake na akabeba mimba ya CANAAN ndio maana akalaaniwa CANAAN na sio ham.....ni nadharia tu mkuu bado sio FACT
 
Nimependa sana hii historia imenifanya kwa muda nijaribu kufuatilia historia ya biblia ila nmesoma andiko la mwanzo 15:18-20 inaonekana warefaimu walikua kikundi(jamii) waliojulikana pamoja na jamii zingine na ni tofauti na wanefiri wanaotajwa kwenye mwanzo sura ya 6 pia nimeona 2sam 21:16 inatoa wazo kama warefaimu walikua wakubwa na nguvu kuliko wengine na ilikua jamii kulingana na kitabu kimoja insight on the scriptures kinataja hawa walikua wazao wa mtu mmoja alieitwa Raphah(ha`Ra•phah)
 
Nashukuru mkuu kwa taarifa yako ya kwamba umefanya utafiti kwa kusoma biblia ubarikiwe sana na ndio nia ya mada hii sio kupinga maandiko ila kufanya watu tusome maandiko na vitabu mbalimbali tuongeze maarifa so heshima kwako

Tukirudi kwenye hoja nafkiri warefai kuitwa wanefili ni sawa sababu kiebrania warefai maana yake ROHO ZA MIZIMU yaani kwa kirefu ni UZAO WA ROHO/MIZIMU/MAPEPO/MAJINI.... Hivyo hiyo ni tafsiri sawa na WANEFILI kwa kiebrania....

Ukitaka kuprove hilo soma upya kuna mistari zaidi ya 20 inayotambua warefai kama wanefili tuangalie huu mmoja

Hesabu 13
33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.

Hivyo tunaweza hitimisha warefai na wanefili ni kitu kimoja

Barikiwa
 
Asant sana
 

Yasiyo wezekana kwa watu kwa Mungu yanawezekana
Goliath alikuwa jitu kubwa sana DAUD alionekana kama kifaranga na jiwe aliloweka kwenye kombeo ni kama punje ya harage kwa Goliath lakini alianguka jiulize aliangukaje pia mkuki wa Goliath ulikuwa wa shaba uzani zaidi kilo 20 na urefu sawa na mikono sita lakini (huenda DAUD wakati huo alikuwa na kilo 45 maana alikuwa kijana mdogo sana ) lakini aliunyanyua na kumuua goliath
 
Aseee upo deep mkuu umetoa mfano wenye mashiko sana.... ubarikiwe
 


Nami pia naomba nikuunge mkono kuipinga hoja number tatu, kwa facts kinzani kutoka kwenye maandiko ya biblia kama ifuatavyo;kwa kulinganisha sehemu zilizo in red(hapo chini) ni wazi kuwa maji yalimzidi kimo huyo mfalme Ogu au sio???? naomba kuwasilisha hili........

-Mwanzo 7
20 Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano.

-Kumbukumbu la torati 3:11
11 (Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho je! Hakiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni mikono kenda, na upana wake mikono minne, kwa mfano wa mkono wa mtu).
 
Mkuu vipimo vya kitabu cha mwanzo na kumbukumbu la torati ni tofauti kabisa mind you ilishapita miaka maelfu sasa inakuaje vipimo mlinganishe kama hii ni hoja mbona hatuchukui vipimo vya Nabii Amos aliyemfananisha urefu wake na miti ya mwerezi ilio sawa na MINAZI ya huku pwani

Amos 2:9
9 Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini

Hivyo tusilinganishe vipimo kwenye karne tofauti na ndio maana kwenye vitabu vya kumbukumbu waisraeli wanasema walikuwa wadogo kama PANZI mbele yao ikimaanisha jamaa walikuwa warefu sana maana huwezi ukawa panzi kwa mtu wa futi 14!! Za karne ya sasa
 


Ila mkuu Zitto unaposema tusilinganishe vipimo vya karne tofauti natatizika kidogo....maana hoja inabaki kuwa garika ilitokea karne moja wakati huyo mfalme Ogu akiwa bado yupo au sio???....na si ndo maana kichwa cha Uzi kinasema mfalme aliyepona kwenya gharika......au gharika zilikuwa mbili kwa utofauti wa karne na uwepo wa mfalme Ogu????......pia niogezee kuwa kitabu cha mwanzo na kumbukumbu LA torati vinabiki kuwa ni vitabu tu vilivyo rekodi tukio husika pasipo kujali viliandikwa wakati gani!!....

Naomba kuwasilisha hoja mkuu!!!
 
Mkuu ukisoma biblia ya kiebrania hayo maelezo ya mikono 9 ni zaidi ya futi 28 !!! Maana wanadai MIKONO ilipimwa kwa kutumia mikono ya wacaanani yaani wanefili wenzake na ogu sio mikono ya zitto junior ama Mshana Jr .....

Mfalme OGU kwa simulizi hizi aliishi miaka kati ya 2000 hadi 3500 sababu ya ukubwa wake..... Kwahiyo ukisoma TALMUD yaani biblia ya wayahudi ambao ndio walimuona uso kwa uso... Talmud sura ya 61 utagundua hilo suala na hoja ya kwamba aliishi kuliko mwanadamu yeyote yule na alipona gharika hadi kuja kuuawa na MUSA

Kwahiyo kwa kujibu hoja yako ni kwamba tokea ogu anapona gharika hadi anakufa HAIKUWA WAKATI MMOJA ni GAP la miaka zaidi ya 1000

Ahsante
 
Hivi mtu wa futi 28 akionekana leo pale mitaa ya posta mida kama ya mchana hivi, si itakuwa patashika nguo kuchanika watu kutoka ndukiii....!!!

Itakuwa ni kuanguka na kuzimia. Me futi tano manake kwa Ogu naingia mara tano na bado futi tatu atanidai duuuh!!! Mungu katuficha mambo mengi jamani....!!!!

Na kwanini iwe hivyo wakati katuumba yeye???
 
Kwa namna moja inaweza kuwa Mungu ndio alitaka wanadamu wa kale wawe hivo sababu ya umri waliokuwa wakiishi..... Yaani mtu aliishi miaka 900+ kama Adam au Methuselah ni lazima mwili uwe wa kibabe ili iweze kuhimili miaka yote hiyo sidhani kama unaweza kuwa na kamwili kama wa joti alafu uishi miaka 900 never!! Sijasoma biology au genetics ila kwa mtazamo wangu naona kuna connection kati ya UIMARA wa mwili na kuishi miaka mingi

Na ndio maana baada ya kupunguza umri wa wanadamu yaani baada ya gharika tunaona watu waliishi miaka sio zaidi ya 300 na ndio maana hata majitu makubwa yalipungua yakabaki yenye damu ya wanefili pekee!! Hii pia inaweza kuongezea sababu kwenye hoja yangu ya hapo juu kuhusu UMRI=UIMARA WA MWILI

Hoja kinzani itasema kuwa huenda kuna ukweli kuwa walikuwa kizazi cha kitofauti yaani mchanganyiko wa kizazi cha nyoka + na kizazi cha Mungu na ndio maana wakazaliwa watu warefu na wenye nguvu za ajabu ni katika kipindi hiki ndipo simulizi za majitu mashujaa kma nimrod Saigon gilgamesh na Hercules Zilikuwa kipindi hicho hadi wakaitwa MIUNGU kwa wakati wao hivo hoja ya uzao wao kutokuwa wa kibinadamu inapata mashiko hapa sababu tuliona uzao wa wanadamu wengine nje ya wanefili hawakuwa warefu sana kufikia hawa warefai/wanefili

Anyway labda watalaamu wa genetics wanaweza kusaidia hapa cc Kiranga
 
Umenene Vyema
 
Kweli mkuu
 
Wadau nimeona ITV habari za saa mbili usiku, wazee wa Ntwara aka Mtwara wameitaka serikali kulitumia pango flani hivi lipo huko ambalo wajerumani walilitumia kujificha wakati wa vita vya dunia. Pango Hilo linaitwa nyumba ya mungu sababu halijachongwa na mtu. Lina vyumba kibao. Lkn kingine walichongundua juu yake ni makaburi ya watu yaliyokuwepo juu ya huo mlima. Makaburi hayo ni ya watu waliokuwa na urefu wa futi nane hadi kumi. Hii inaendelea kuthibitisha hizi habari za giants existence pande hizi za bongo
 
Og aliweza kukata mlima, kuubeba na kuutupa? Na bado akaishi akapona gharika nje ya safina, wakati ambapo maji yalichukua mwaka mzima kukauka, nadharia nyingine, zinataka uvumilivu, kuzielezea!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…