mkuu habr za Jpili. Nimepita nikavutiwa ghafla ni Hii comment.
Nadhani chanzo cha uovu sio wanephili ni shetani. Wawepo au wasiwepo Uovu utakomeshwa.
Nadhani tukiendelea kumjifunza Mungu katika kauli zake za kwenye bibilia tutaishia kusema walipona wanane tu.
Kuna sehemu nyingi wanaandikwa wanaume tu, mfano Wale watu 5000 waliolishwa na yesu, au wale waliobatizw siku ya pentecoste. ila mahala ambapo mwanamke ameandikwa nadhani hatuhitaji kulazimisha kuwa kuna watu bado walirukwa.
Mfano Mathayo 1, anapozungumzia genealogy ya Yesu wanawake wanarukwa, mahala ambapo palisisitizwa waliwekwa mmfano Tamari aliyewazaa Peresi na Zera kwa Baba mkwe yake Yuda, au Rahabu au mke wa Boaz RUth.
mfano.
HApo hao watu wanane waliopona walichambuliwa na wasifu wao na jinsia zao. Tofauti na vyanzo vingine ambavyo viliweka idadi jumlajumla bila mchanganuo. Hivyo haitupi mwanya wa kuwa kuna watu waliingia kwenye safina lakni hawakutambuliwa unless wawe wanajinsi ya tatu ambayo haipo.
naendelea kutafakari.
barikiwa mkuu.