Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Mfalme Ogu wa Bashani: Mnefili pekee aliyepona kwenye Gharika la Nuhu

Mi kwa uelewa wangu nadhani mnachanganya
OGU Alitoka kwenye jamii ya amorites people
Na AMORITES ni uzao wa CAANAN mwana wa Nuhu.
Na biblia iliposema alibaki OGU kati ya Giants ni kwamba yeye ndio alikuwa wa mwisho kwa duniani kusumbua kipindi kile.
SWALI MUHIMU NI KUWA: WALIRUDIJE BAADA YA GHARIKA??
Ndio wengi tunarudi kwa Ham baba yao na mama yao ambae haongelewi na huyo mtoto wa CAANAN why alizaa GIANTS mbona watoto wengine wa HAM hawakuzaa GIANTS??
SO CAANAN NDIO SHIDA HAPA YEYE NDIO WA KUDADAVUA.....(NA WHY NUHU ALIMLAANI)...KWA CAANAN NDIO PENYE JIBU LA KWELI
Hapo umenena mkuu kula like
 
1 uko sahihi kabisa kwa mujibu wa biblia ila vitabu vya wayahudi wenye nchi yao alipoishi ogu wanasema alikuwepo kabla ya gharika ndio maana nikaleta uzi humu ili tujue nani mkweli nani anapotoaha.... Wanadai hata hao waamori ni zao lake yeye ndio maana alikua mfalme wao miaka yote.

2.Kingine ni kweli nakubaliana na wwe kuwa itakuwa ham alioa mwanamke mwenye damu ya kinefili ndio maana wanefili walirudi baada ya gharika ila swali langu je Mungu hakulifahamu hilo na kma alifahamu kulikuwa na haja gani kuiangamiza dunia nzima ili kuwafuta wanefili ilihali mwingine (mke wa ham) alipona ??

3. 90% ya wanefili ni kweli walitokea kwenye kizazi cha ham kupitia canaan ila usisahau pia Mizraim naye alizaa mnefili mmoja anaitwa caphtor kma sikosei na ndio alizaa wafilisti kina goliath waliokuwa wanefili pia.....

Ni hayo tu
Neno Mabaki Mabaki baada ya uyu jamaa kuna waanaki so issue nikuelewa neno mabaki tumia nabiblia zaidi
Ndugu Zitto
 
Neno Mabaki Mabaki baada ya uyu jamaa kuna waanaki so issue nikuelewa neno mabaki tumia nabiblia zaidi
Ndugu Zitto
Kwa maoni yako je kwanini Mungu aliangamiza dunia kwa gharika ilihali alijua wanefili wangerudi tena na kuendeleza maasi yaleyale??
 
Kwa maoni yako je kwanini Mungu aliangamiza dunia kwa gharika ilihali alijua wanefili wangerudi tena na kuendeleza maasi yaleyale??
mkuu habr za Jpili. Nimepita nikavutiwa ghafla ni Hii comment.
Nadhani chanzo cha uovu sio wanephili ni shetani. Wawepo au wasiwepo Uovu utakomeshwa.
Nadhani tukiendelea kumjifunza Mungu katika kauli zake za kwenye bibilia tutaishia kusema walipona wanane tu.
Kuna sehemu nyingi wanaandikwa wanaume tu, mfano Wale watu 5000 waliolishwa na yesu, au wale waliobatizw siku ya pentecoste. ila mahala ambapo mwanamke ameandikwa nadhani hatuhitaji kulazimisha kuwa kuna watu bado walirukwa.
Mfano Mathayo 1, anapozungumzia genealogy ya Yesu wanawake wanarukwa, mahala ambapo palisisitizwa waliwekwa mmfano Tamari aliyewazaa Peresi na Zera kwa Baba mkwe yake Yuda, au Rahabu au mke wa Boaz RUth.

mfano.
HApo hao watu wanane waliopona walichambuliwa na wasifu wao na jinsia zao. Tofauti na vyanzo vingine ambavyo viliweka idadi jumlajumla bila mchanganuo. Hivyo haitupi mwanya wa kuwa kuna watu waliingia kwenye safina lakni hawakutambuliwa unless wawe wanajinsi ya tatu ambayo haipo.

naendelea kutafakari.
barikiwa mkuu.
 
Sio maudhui ya mada hii
Kuna mada kibao za aina ya ubishani unaoutafuta.
Kama huoni hizo mada, basi anzisha mada yako kwenye forum ya dini na sio huku kwenye jukwaa la intelligence lenye watu makini wasiohitaji mabishano yasiyojenga

Mbona uliandika mwenyewe kuwa yesu alikufa , hivi ubishani niliuanza wapi?? nimeuliza tu au ulivyoandika ulikuwa hujielewi ??

Ingalikuwa hukuandika hata nisingalikuuliza kabisa ndio maana kama ulivyosema hili ni jukwaa la intelligence , usiropokwe tu , utaulizwa , kama huna ushahidi si sema tu sina , nani atakuweka kwenye kwenye mfuko wa plastiki na kukutupa coco beach ???
 
mkuu tunaomba mchango wako kwenye mada pia kama jamaa anavyokusisitiza.
kuvizia vitu vilivyonje ya mada, ili uweke jukwaa la kufanyia mihadhara nadhani mleta mada ametutahadhalisha.

unaweza kutumia kitabu chako kitukufu Quran, au elimu dunia kutupa darasa ili tupanue uelewa mkuu.
nimeguswa kutoa huu mchango ili ulichokishauri kiishie hapo hapo.
 
Huu ni upotoshaji wa hali ya juu sana. Sikatai kama Mfalme Ogu hakuwepo lakini nakataa kuwa aliishi zaidi ya miaka 3500. Pia nakataa kuwa eti mfalme huyu Ogu alikuwepo kabla ya Gharika na alinusurika kwenye gharika, huu ni uongo wa kiwango cha lami.

Wewe unasema tusiweke mambo ya imani kwenye huu uzi wako, lakini wewe mwenyewe umetumia vifungu vya kwenye Biblia kuhalalisha huu "uongo" wako na "upotoshaji" wako. Sasa na mimi nitakujibu hoja zako kwa kutumia vifungu vya kwenye Biblia. Kwanza kabisa Biblia imebeba NENO la MUNGU, na NENO la MUNGU halisemi uongo. Unapotuambia eti Ogu alikuwepo wakati wa gharika unataka kutuambia kuwa NENO la MUNGU, lilitudanganya kwa kusema kuwa Wanadamu walionusirika kwenye gharika walikuwa ni watu 8 tu.

"Maji yakapata nguvu hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano. Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu; kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu. Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao walio pamoja naye katika safina. Maji yakapata nguvu katika nchi siku mia na hamsini". MWANZO 7:20-24

Hicho kifungu hapo juu kinatosha kuonyesha ni jinsi gani stori yako imejaa uongo na upotoshaji. MUNGU wetu siyo muongo na kamwe hawezi kusema uongo hata siku moja!

Ukweli ni kwamba mfalme Ogu alizaliwa miaka mingi baada ya gharika kama watu wengine walivyozaliwa, tena alizaliwa na wazazi wa kawaida kabisa na alikuwa kama binadamu wa kawaida kabisa, isipokuwa tu yeye alikuja akawa mrefu na mwenye mwili mkubwa. Ukubwa wa mwili wake ulitokana na kitu kwa kitaalamu inaitwa "gene mutation", na hii huwa inatokea kwa nadra sana na ndiyo maana utaona kuwa Ogu alikuwa ni wa pekee kabisa na hakuna aliyekuwa akifanana naye wakati ule miongoni mwa wanadamu.

Tena ufahamu kwamba baada ya Ogu kuuawa, miaka mingi baadaye akazaliwa mwingine ambaye naye alipata hiyo "gene mutation" ambaye alijulikana kama Goliathi. Wote tunafahamu stori ya Goliathi na Daudi nini kilitokea.

Kwenye stori yako umeweka uongo mwingi sana na chumvi kibao ili kupotosha watu wasiokuwa na imani na ufahamu. Kwa mfano unasema eti Ogu alinyanyua "mlima" ili awatupie wana wa Israeli. Huu ni uongo wa karne! Mlima siyo jiwe au mwamba uliokaa peke yake hata uweze kuunyanyua juu. Mlima ni mchanganyiko wa udongo, mchanga, mawe na miamba na kamwe haiwezekani kuunyanyua juu ukiwa mzima mzima kwa kutumia mikono ya kibinadamu, hata kama huyo binadamu ana umbo kubwa namna gani.

Inasikitisha sana ndugu yangu zitto junior kuona unaandika mambo ya "uongo" tena ukitumia maandiko ya Biblia vibaya ili kumfanya MUNGU BABA yetu aonekane ni "muongo". Hii ni hatari sana kuona kuna binadamu wamefikia hatua hii ya kumsizingizia MUNGU uongo tena bila woga kabisa.
 
Nimeona nisiache ku coment japo kidogo baada ya kusoma hii mada tokea mwanzo hadi sasa japo imenichukua siku 3 usiku na mchana.

Pongezi nyingi sana mleta mada na wachangiaji wote hakika nawatakia heri njema kwa kushirikisha kile mlichokipata katika kusoma kwenu, hakika huo ndio UPENDO.

Lakini pia nami nimebahatika kupata mawili matatu ya kuimarisha imani yangu katika Kristo. Ilaa ni kiri wazi kabisa Biblia isiwe kwangu kitabu cha mwisho kujifunza elimu ya Mungu japo lugha ya kiingereza imekua changamoto kwangu lakini najiahidi kujifunza hii lugha ili nipate kujifunza mengi japo mwisho wa kusoma kwangu ni darasa la saba.

Lakini pia nikubali tuu kama Mkristo Mkatoliki hawa mapadre na maaskofu na waalimu wa kanisa hawajathubutu kutumegea japo kidogo kile walichofundishwa huko seminarini kwenye teologia na falsafa zao zaidi ni habari za watakatifu wa kizungu na wachache wa kiafrika, kwa hili nisiwalaumu lakini hawatutendei haki.

Lakini pia huyo OGU japo kuna maelezo mengi kumuhusu lkini baya lake naona ni moja kutokuwapa waisrael ruhusa ya kupita. Sijui kama kuna mabaya yake yamelioelekezwa kwake labda wajuzi watujuze.

Natoa tena na tena pongezi kwa kila mmoja aliechangia mada hii pamoja na mleta mada heri njema ziwe nanyi.
 
Mkuu Son of Gamba nani anapotosha ilihali nimeweka sources zangu??

Quran(hadeeth)
Biblia
Jasher
Book of giants
Book of enoch
Tanakh
Torah
Talmud
Na article tofauti

Sasa kama ni kupotosha hao ndio waliopotosha maana mie nimesoma tu ndio nimeweka hapa hoja sasa nimepotosha maneno gani?? Wapi nimesema ACCORDING TO ZITTO JUNIOR OGU ALIPONA GHARIKA??

Kingine historia ya israel wanaijua waisraeli wenyewe na wameiandika kwenye vitabu vyao wanavyotumia kuswalishana kwenye masynagogue ikiwemo TALMUD na ndio inasema OG alinyanyua mlima,alipona gharika na aliishi miaka 3500 ina maana wwe ndio unajua sana historia ya israel kuliko waisraeli wenyewe hadi upinge maandiko yao kisa tu biblia ilioamuliwa vitabu gani viwekwe na visiwekwe na wazungu 21 haijaandika ??

Kingine nimesema hii mada sio ya kidini sababu nilijua watu kma ww mtakuja na nukuu za biblia kuniita mpotoshaji mie nmequote tu biblia kma ambavyo nmequote kubeba mlima kutoka kwenye talmud na kupona gharika kutoka kwenye hadeeth za kiislam ssa unapotetea hoja yako kutumia biblia tu una maana gani??? Kwani wapi nmesema ogu kaongelewa na biblia pekee??

Ni vizuri tujenge tabia ya kukubali mawazo mapya na kupinga kwa hoja kma wenzako walivyofanya sio kuitana wapotoshaji ilihali source nmekuwekea labda useme wayahudi wametudanganya ila kusema mmi mpotoshaji umenishangaza sana na kwa staili hii hatutofika kokote !!
 
Nimeona nisiache ku coment japo kidogo baada ya kusoma hii mada tokea mwanzo hadi sasa japo imenichukua siku 3 usiku na mchana.

Pongezi nyingi sana mleta mada na wachangiaji wote hakika nawatakia heri njema kwa kushirikisha kile mlichokipata katika kusoma kwenu, hakika huo ndio UPENDO.

Lakini pia nami nimebahatika kupata mawili matatu ya kuimarisha imani yangu katika Kristo. Ilaa ni kiri wazi kabisa Biblia isiwe kwangu kitabu cha mwisho kujifunza elimu ya Mungu japo lugha ya kiingereza imekua changamoto kwangu lakini najiahidi kujifunza hii lugha ili nipate kujifunza mengi japo mwisho wa kusoma kwangu ni darasa la saba.

Lakini pia nikubali tuu kama Mkristo Mkatoliki hawa mapadre na maaskofu na waalimu wa kanisa hawajathubutu kutumegea japo kidogo kile walichofundishwa huko seminarini kwenye teologia na falsafa zao zaidi ni habari za watakatifu wa kizungu na wachache wa kiafrika, kwa hili nisiwalaumu lakini hawatutendei haki.

Lakini pia huyo OGU japo kuna maelezo mengi kumuhusu lkini baya lake naona ni moja kutokuwapa waisrael ruhusa ya kupita. Sijui kama kuna mabaya yake yamelioelekezwa kwake labda wajuzi watujuze.

Natoa tena na tena pongezi kwa kila mmoja aliechangia mada hii pamoja na mleta mada heri njema ziwe nanyi.
Barikiwa mkuu kwa maoni yako ya kujenga... heri njema pia
 
Hii mada kuhusu canaan kulaaniwa na sio ham ni pana sana itabidi nipandishe uzi kabisa wa kujitegemea watu wafunguke
Kuna dhana kwamba huyu Canaan baada ya kulaaniwa na Baba yake ndo akaanza kuzaa watoto weusi, Na kwamba ndo mwanzo wa waafrica. Hebu shusha nondo kidogo tuu kuhusu hapo
 
mkuu habr za Jpili. Nimepita nikavutiwa ghafla ni Hii comment.
Nadhani chanzo cha uovu sio wanephili ni shetani. Wawepo au wasiwepo Uovu utakomeshwa.
Nadhani tukiendelea kumjifunza Mungu katika kauli zake za kwenye bibilia tutaishia kusema walipona wanane tu.
Kuna sehemu nyingi wanaandikwa wanaume tu, mfano Wale watu 5000 waliolishwa na yesu, au wale waliobatizw siku ya pentecoste. ila mahala ambapo mwanamke ameandikwa nadhani hatuhitaji kulazimisha kuwa kuna watu bado walirukwa.
Mfano Mathayo 1, anapozungumzia genealogy ya Yesu wanawake wanarukwa, mahala ambapo palisisitizwa waliwekwa mmfano Tamari aliyewazaa Peresi na Zera kwa Baba mkwe yake Yuda, au Rahabu au mke wa Boaz RUth.

mfano.
HApo hao watu wanane waliopona walichambuliwa na wasifu wao na jinsia zao. Tofauti na vyanzo vingine ambavyo viliweka idadi jumlajumla bila mchanganuo. Hivyo haitupi mwanya wa kuwa kuna watu waliingia kwenye safina lakni hawakutambuliwa unless wawe wanajinsi ya tatu ambayo haipo.

naendelea kutafakari.
barikiwa mkuu.
Ila hao wanefili ndo walisababisha Gharika
 
Hapa inaonekana wazi ni mpango wa Mungu hawa wanefili majitu yaendelee kuwepo hata baada ya gharika, Maana kama shetani baada ya kuasi mbinguni alitupwa tuu duniani akaachwa huru aendelee kuishi huku akitamba na uwezo wake woote, Iweje Mungu hakumuua??? sembuse hao wanefili? So I think its plan of God
 
acha kuwa mgumu mimi nimesema malaika hao wamefungwa??
Au hukuelewa nimesema aliyefungwa ni shetani na ninakazia tena ni baada ya yesu kufufuka kama nilikosea kuandika nisamehe kwa hilo mkuu
Kingine ujue kama shetani angeoparate duniani mpaka Leo ungewaona wanefili wa kizazi kipya but wanao oprate now ni malaika Walio chini yake. Tena hawana nguvu wala haki hiyo kwa sababu kabla ya agano jipya walijiamlia kumwingia mwanadamu watakavyo.ila sio kama sasa hawa malaika kukutumikisha jua umeamua mwenyewe uliza tena mkuu nakukaribisha kwa upendo
Vyovyote mkuu,huo mstari si unaona unaoneshakuwa shetani ndiye atafungwa miaka 1000? anafungwaje wakati yupo kifungoni?
 
Kuna dhana kwamba huyu Canaan baada ya kulaaniwa na Baba yake ndo akaanza kuzaa watoto weusi, Na kwamba ndo mwanzo wa waafrica. Hebu shusha nondo kidogo tuu kuhusu hapo
Hapana mkuu canaan alilaaniwa sababu inadaiwa ham alimlala mama yake yaani mke wa Noah ndio akazaliwa canaan ila nadharia nyingine inasema canaan ndio aliona uchi wa nuhu ndio akaenda kumwambia ham ambaye naye ndio akaenda kuwaambia kina shem na japhet nadharia ya tatu inasema Ham alimuhasi Nuhu ndio maana hakupata watoto wengine baada ya gharika hivyo kwa hasira akamlaani canaan sababu ni kizazi cha HAM maana HAM aliua kizazi cha nuhu pia so bado kuna debate god willing ntapandisha uzi tujadili kwa kina

Kuhusu watu weusi kutokana na canaan kunaweza kuwa na ukweli ila kizazi cha canaan kibiblia kilifutika 90% hivyo hata kma walibaki walimezwa na semites wengine wa mashariki ya kati hivyo wakaishia huko yemen au qatar ila hawakufika afrika however watu weusi hatukulaaniwa kokote kumbuka waafrika wametoka kwa watoto wa ham wale wakubwa yaani Cush mizraim na phut ambao laana ya nuhu haikuwapata hivyo sio kweli kwamba ile laana ndio ilitufanya tukawa weusi na hta kma ni kweli ingemhusu tu canaan ambaye kizazi chake kilishapotea so sioni wapi laana imetufikia waafrika

Ni uelewa wangu tu huu wajuzi wanaweza tusaidia
mitale na midimu Malcom Lumumba Eiyer
 
Kuna dhana kwamba huyu Canaan baada ya kulaaniwa na Baba yake ndo akaanza kuzaa watoto weusi, Na kwamba ndo mwanzo wa waafrica. Hebu shusha nondo kidogo tuu kuhusu hapo
Hizi ni story tu za wazungu hakuna ukweli hapo.
Watu wa mwanzo hawakuwa weupe.
Hii ni stry za wazungu ili tuwaone wao ni bora kuliko sisi na tujihisi wanyonge mbele yao lakini sio kweli.
Rome wakati wanawapiga vita waisrael wa kipindi cha Yesu then wakakimbia nchi yao unadhani walikimbiloa juu ambako rome ilikuwa inatawala? Au walikimbilia chini (Africa) ambako warumi hawakuwepo?
Huwezi kimbilia sehemu iliyo na adui...
Na kumbuka egypt ya kale haikiwa ya waarabu wala wazungu.
 
Back
Top Bottom