Mkuu
Eiyer habari za siku.... Umepotea sana jukwaani ila nmefurahi sana umeweza kuja na kutupa elimu adimu kama kawaida yako great thinker
Nkirudi kwenye mada...kwa kuzingatia objections zako za ''kisomi'' nina maswali kadhaa naomba utujuze
1. Je wanefili waliwezaje kurudi baada ya gharika if at all waliangamizwa wote kwenye gharika?? Na biblia iko wazi kuwa wale malaika walifungwa kuzimu kusubiri hukumu siku ya mwisho je hiyo bloodline yao iliponaje gharika sasa ambapo tukikataa ogu alisalimika.
Mkuu,kwa namna ninavyoelewa mimi ni kwamba,kwanza suala au dhana ya malaika "kufungwa" kwa upande wangu bado halijakaa sawa....
Nasema hivui kwa sababu sijawahi kuelewa huko "kufungwa" ni kwa namna ipi,lakini pia bado sijaelewa kama walifungwa kweli walifungwa wakati upi. Nasema hivi kwasababu kwenye kitabu cha Ayubu ule ukurasa wa kwanza tu kuna kisa cha Shetani kujumuika na Malaika [Wana wa Mungu] mbinguni huko na alipoulizwa alisema kuwa ametokea duniani alikokuwa anazunguka zunguka. Ukiacha tukio hili kuna tukio la Shetani kufungwa miaka 1000 kwenye kitabu cha Ufunuo baada ya ile dhiki kuu.Hapa inaonekana huyu balaa alikuwa hajafungwa au kuwepo kifungoni...
Ayubu 1:7
7 Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.
Ufunuo wa Yohana 20:1-3
1 Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;
3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.
Sasa kwa mantiki hii ni vigumu sana kuhitimisha tu wamefungwa kuzimu na hawatoki humo [kwa maana ya wengi na iliyopelekea kuleta swali uliloniuliza] na kufanya swali la kizazi chao kuwa kuendelea kuwepo kuwa ni gumu zaidi...
Jambo la msingi ambalo wengi hapa wanapaswa walielewe ni kwamba Wanefili walikuwepo hata baada ya Gharika.Waliendelea namna ipi hilo ni jambo la kufanyia utafiti lakini kuna nadharia moja inaeleza kuwa,kwasababu viumbe hawa [Wanefili] walikuwa wanauelewa mkubwa sana wa kanuni za maumbile [physical law] waliweza kupona kwenye gharika kwa namna moja au nyingine au hawakupona lakini malaika wale waliendeleza kizazi kile kwa namna ile ile kwasababu wao gharika haikuwahusu...
Ukiniuliza mimi binafsi naelewaje au kufahamuje viumbe hawa waliwezaje kupatikana baada ya gharika,kama msingi wa swali lako ulivyo ukweli ni kwamba hadi sasa sijapata jibu lenye mashiko au niseme tu kuwa sifahamu ilikuwaje wakaendelea kuwepo lakini nina uhakika kuwa waliendelea kuwepo....
Nina dhana nyingi tu ambazo zinajaribu kuelezea hawa majitu waliendeleaje kuwepo na bado naendelea kufuatilia....
2. Hoja ya kusema Mungu alisimamia gharika hivo basi hakuna mnefili ambaye angepona sababu Mungu alishadhamiria..... Mbona wakati ukuta wa yeriko unaangushwa yule malaya alisalimika kwa Mungu kuacha nyumba yake pekee je haiwezi kuwa case kwa Nuhu ukizingatia alimsaidia kwenye ujenzi hasa kufuata miti iliyotumika kwenye ujenzi haikuwa ikipatikana mashariki ya kati na vilevile ukubwa ule wa meli usingeweza kuwa assembled na binadamu wa kawaida kwa teknolojia ya enzi hizo ila huyu ogu alikuwa msaidizi mkubwa je haiwezi kuwa sababu ya Mungu kumpa neema yake asife kwenye gharika kma alivompa yule malaya wa yeriko??
Kwanza mkuu nianze kwa kukueleza kuwa ishu ya Yericko ni tofauti sana na hii japokuwa inahusiana pia. ni tofauti kwasababu Rahabu [kama sijakosea] alitoa msaada kwa wapelelezi wa Israeli na wakamuahidi watamuacha hai.Hapa kuna jambo kubwa sana mkuu kwasababu bloodline ya huyu mwanamke ndiyo hii tunayokuja kuipata kwa Yesu.Yaani uzao wa Rahabu ndio blood line ya Yesu. Hili niliache kwa sasa maana kuna mengi hapo,lakini pia unapaswa ukumbuke kuwa maelekezo ya Mungu ya kuwaangamiza Wakanaani ilikuwa ni wanaume wote na wanawake waliomjua mwanaume.Jambo hili linasababishwa na suala hili hili la Wanefili.Hili nalo lina mengi lakini ninachotaka ukione hapa ni kwamba kitendo cha Mungu kuruhusu Rahabu kuendelea kuishi bila kujali alikuwa ni kahaba na kitendo cha kuwa kahaba kina maana kuwa na uwezekano wa kuwa na watoto wenye damu hii ya Wanefili kinaleta maswali mengine magumu sana...
.....sasa basi,kunakuwa na sababu ya kahaba huyo kuachwa hai,je kuna sababu ipi ya Wanefili wa kabla ya gharika kuachwa? [Japokuwa sijasema hawakuachwa] Dhana ya huyu OG kumsaidia nuhu ni ya kufikirika zaidi kwasababu haina ushahidi wa kimaandiko kuwa alimsaidia Nuhu,ni mawazo ya watu tu. Kwa maoni yangu,kama walipona basi huenda ni kwa sababu ambayo huenda hatujaijuwa bado....
Kuhusu Tekinolojia ya wakati huo ni kwamba mimi binafsi ninaamini kuwa wakati ule kulikuwa na maendeleo ya kiteknolojia zaidi ya wakati huu.Ninasema hivi kwasababu nimepitia dicumentary nyingi tu zikielezea maendeleo ya hatari ya wakati huo.Kwa kukuonesha hili nenda katafute documentary moja inaitwa "Technology of the Fallen" utapata mwanga.Maendeleo haya yalitumiwa na binadamu wengine,sisemi kuwa Nuhu aliitumia isipokuwa nataka tu nianze kubadili mtazamo wako kuwa zamani hizo hawakuwa na maendeleo au maendeleo yao yalikuwa duni kuliko leo....
....Mungu kaka alivyo yeye ndiye baba wa teknolojia yote,malaika waasi waliona namna Mungu alivyokuwa anaweka kanuni zote za Physics na vitu vyote kwa ujumla wake na wakaweza kuwa na uelewa mkubwa sana wa kanuni hizo na zingine nyingi.Kumbuka tu ni malaika hao hao waliokuja kuleta maarifa haya kwa binadamu,maarifa ambayo kimsingi binadamu hakupaswa kuyafahamu,maarifa haya yanaitwa "forbiden knowledge".Binadamu hakupaswa kuyaelewa maarifa haya kwasababu hakuumbwa kuyahimili na ndiyo maana walipoyajuwa walianza kuangamizana wao kwa wao na hata leo unaona yanavyotutesa.Sasa kama hawa waliona tu na wakawa na ujuzi huo,vipi Mungu mwenyewe ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa kujengwa safina hadi gharika yenyewe ambaye ndiye mwenye kanuni na ujuzi huo?
Ninachotaka ukielewe hapa ni kwamba,jambo lilalosimamiwa na Mungu mwenyewe weka pembeni yanayowezekana na yasiyowezekana kwa binadamu. Kwa hiyo dhana ya huyo OG "kumsaidia" Nuhu siioni kama ina mashiko kwasababu tu Nuhu "asingeweza" kuijenga mwenyewe....
3. Je Hawa wanefili waliishia wapi mkuu.... Kuna mmoja hapa katoa hoja kuwa damu yao bado ipo na kuna viongozi wakubwa wa dunia hii wana damu za kinefili je kuna ukweli hapa au conspirancy?? Na kma sio kweli je hawa wanefili waliishia wapi mbona leo hii hatuoni majitu ya size hiyo??
Ni hayo tu kwa sasa
Cc:
Malcom Lumumba Kudo900
Hawa Wanefili hawajaisha mkuu,tena nasema hivi kwa uhakika kabisa...
Ni nini kinanipa uhakika mkubwa hivi?
Vipo vingi tu na cha kwanza ni Biblia yenyewe....
Mosi,Biblia yenyewe inakiri Wanefili walikuwepo hata baada ya gharika [mwanzo 6:6],kama walikuwepo baada ya gharika basi watakuwepo hadi leo maana sijaona sababu ya kutokuwepo kwao....
Pili,Yesu mwenyewe alisema "kama ilivyokuwa nyakati za Nuhu ndivyo itakavyokuwa wakati wa kuja kwake mwana wa Adamu" hii inamaana kuwa,moja ya alama za kurudi Yesu mara ya pili ni uwepo wa mambo kama ya nyakati za Nuhu na moja ya mambo ya wakati ule ni uwepo wa Wanefili...
Tatu,utafiti ambao umeshafanywa na watu wengi sana unaonesha kuwa Majitu haya yapo hadi leo hivyo sina sababu ya kupinga na nimeshaangalia video moja kutoka kwa mtu aliyeshuhudia kuona majitu haya kwenye D.A.M.Bs [Deep Underground Military Bases] zilizoko karibu dunia nzima chini ardhini na yanachapa kazi kabisa. Kilichoko huku juu ni mfano wa kilichoko huko chini.Majiji unayoyaona huku juu ni madogo sana kwa size ya majiji yaliyoko huko chini ardhini ma majiji yote yameunganishwa kwa barabara zilizojengwa kwa viwango vya hali ya juu kiteknolojia,ngoja niishie hapa kwenye hili...
Nadhani swali litakalofuatia hapa ni kuhusu sababu za majitu haya kufichwa au kujificha.Sababu namba moja iliyofanya haya ni udanganyifu....
Ni udanganyifu namna gani?
Kwanza kabisa baada ya gharika Shetani aliamua kutengeneza namna mpya ya kukabiliana na Mungu na njia hiyo ni udanganyifu. Udanganyifu wa kwanza kabisa ni kuhakikisha kile ambacho Mungu anawaeleza binadamu kionekane ni uwongo.Mojawapo wa mfano wa jambo hili ni suala hili la uwepo Mjitu haya.Shetani aliamua kuendesha harakati zake mafichoni huko na siyo wazi maana kama ikiwa siyo mafichoni watu wataona majitu haya na kuverify maelezo ya kwenye Biblia kuwa ni kweli yalikuwepo majitu na hili lina madhara makubwa sana kwao maana kuna mtaalam mmoja wa masuala ya Evolution alisema kuwa kama itaonekana ni kweli kulikuwepo Wanefili basi evolution inakufa kifo cha kibudu.Kuna aina nyingi sana za udanganyifu haswa kwenye historia ambako ndiko kwenye msingi mkubwa sana wa kuona Mungu anasema kweli namna ipi kwenye kwenye Biblia na maeneo mengine.
Hii ndio sababu moja na ndogo sana na zipo nyingi sana na nadhani hii inatosha kwa hapa....
Ni kweli kuwa viongozi wa dunia wengi ni bloodline isiyokuwa na asili ya binadamu,Moja ya damu inayosadikiwa haina asili ya binadamu inaitwa RH-Negative,nakupa kazi mkuu kafukue ufahamu mengi kuhusu group hili la damu....
Kuna namna ambayo unaweza kuwa na bloodline ya Wanefili na hutakuwa na umbo kubwa na hili linaratibiwa kwenye DNA yako na hiki ndicho alichokifanya shetani ili kuendelea kufanya kazi yake kwa kutumia kizazi chake.Kwa namna hii hata leo tuna "Wanefili" lakini hawaonekani kwa namna inayotarajiwa na wengi kuwa Mnefili ni mwenye umbo kubwa...
Hii siyo ajabu kwasababu ukiwafuatilia marais wa Marekani kwa mfano unaona kabisa ni bloodline moja na inakwenda kuungana na bloodline ya Royal Family kule UK.Brad Pit naye ni blood line hii,ukiangalia hakuzaa na Angelina Jolie kwa bahati mbaya maana naye pia ni bloodline hii hii...
Nadhani kuna mtu anaweza hoji juu ya Barack Obama na bloodline yake,ninachotaka kusema hapa ni kwamba kuna mengi ukiyajuwa kuhusu mtu huyo unaweza baki mdomo wazi...
Acha niishie hapo kwa leo mkuu....
Mungu akubariki sana..
Tuombe uzima tuendelee kupeana kiduchu kiduchu namna hii....