mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,735
Mkuu ukiwa msomaji wa biblia utaelewa hoja yangu kivipi Mungu anaweza toa hukumu ila akaruhusu masalia wabaki na amefanya hivyo hata kwa wanefili wa baada ya gharika (Waamori)ambayo ni familia ya mfalme Ogu
Twende taratibu
1. Mungu anamuamuru waisraeli waue wakaanani WOTE wasibakize kitu
Kumbukumbu la torati 20
16 Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo BWANA, Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu cho chote kipumzikacho;
17 lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, kama alivyokuamuru BWANA, Mungu wako;
2.Tukisoma kwenye joshua baada ya kuwa wameikamata canaani waliweka makubaliano na hawa wanefili ya kuwaacha hai!!
Joshua 9:15
15 Naye Yoshua akafanya amani pamoja nao, na kufanya agano nao, ili kwamba waachwe hai; na wakuu wa mkutano wakawaapia
3.Kinyume kabisa na maagizo ya Mungu ya kwanza tunaona wagibeoni wakiachwa hai na waliingia agano ambalo Mungu alisupport
Kumbukumbu 7
1 BWANA, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang?oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe;
2 wakati BWANA, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao
4.mpaka hapa unaweza kufikiri waliamua wenyewe waisrael lahasha..... Huko mbeleni tutaona MUNGU akiwaadhibu waisraeli kwa kuvunja agano hilo la kuwaacha waamori/wagieboni hai
2 samuel 21
1 Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.
Je unataka kusema Mungu ni kigeugeu au utakubaliana na mimi kuwa Mungu aliamua kuwaacha hao wagibeoni kwa kusudi lake???
Na je kama tunaona hapa Mungu aliamrisha waue waamori WOTE ila baadae Mungu alitaka wengine wabakizwe je huoni hoja ya kusema Ogu kuwa mnefili pekee kuachwa kwenye gharika kuwa ina mashiko maana tumeona kumbe Mungu akitoa hukumu ya WOTE huwa anaacha exceptions!!!
Karibu tuelimishane mkuu wangu
Cc SALA NA KAZI Malcom Lumumba Eiyer popbwinyo Kudo900
mkuu asante kwa elimu.
kama nilivyowasilisha hoja huko nyuma.
1:Bibilia inasema katika mwanzo hakupona mtu zaidi wa watu wanane. na kutoka kwa wanane hao Mungu akawaambia waijaze nchi na kuitiisha.
2:Miaka zaidi ya 2000 nadhani baadae anakuja Mungu kwa umbile la wanadamu kwa jina la Yesu. Anatukumbusha stori hiyo hiyo na kisisitiza kiwa walipona watu wanane, wengine wote waliangamia.
3:Miaka kadhaa baada ya Kupaa Yesu, Anaandika Petro kwa watu wote nikiwemo mimi na wewe kuwa
"Wala hakuuachilia ulimwengu wa Kale, bali alimuhifadhi nuhu mjumbe wake, na watu wengine saba, hapo alipoileta gharika juu ya ulimwengunwa wasiomcha Mungu" 2Petro 2:5.
######
Mkuu hoja yako nimeipata kwa uzuri. kuwa ikiwa hukumu nyingine kuna watu waliponyoka hivyo kuna uwezekano watu wakapona kwenye kila hukumu ya Mungu.
yawezekana sodoma na ghomora kuna waliopona kwa hekima hiyohiyo, wenda kwa hekima hiyohiyo hata kiyama cha mwisho kuna uwezekano wakawepo watakaokwepa (nimeexagerate kidogo kuleta maaa.).
Mkuu unazungumziaje kwa hukumu hiyo na idadi ya watu waliopona kuthibitishwa kuwa ni wanane tu na vyanzo tofautitofauti vilivyoongozwa na roho mtakatifu?.
Mungu anapomuagiza mwanadamu atekeleze hukumu zake, naye akafanya tofauti nadhani ni tofauti na Mungu akitekeleza Hukumu zake.
mfano, Mungu hakumuambia NUHU awaangamize watu, bali yeye aliifanya hiyo kazi mwenyewe kwa ufanisi wote. Kuhusu kugeuka baadae. Mungu katika operations zake agano la kale kuna mahala anaonyesha kuheshimu makubaliano ya watu. mfano Hesau alipomuuzia yakobo uzao wa kwanza. Yakobo aliirithi ahadi wakati kiuhalisia Mungu alipaswa kumpa huo urithi mkubwa yaani Hesau. Lkn Mungu akaweka kumbukumbu sawa kuwa "Basi zamani zile za ujinga Mungu alijianya kama hazioni, Bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu" Matendo 17:30
nakubaliana na wewe pia, tunapaswa kujadili hao watu wenye sifa za wanefili au waliotambulishwa kama wanefili baada ya Gharika.
maswali kadhaa yanaibuka.
Je, Hicho kitendo kilichotokea kabla ya gharika kikazaa wanefili hakiwezi kutokea baada ya gharika?
Kwa nini hakitokei sasa?
Je hawa watu warefu wa sasa ambao si wakawaida wanauhusiano wowote na Og au ni genetics za kawaida?
kitanda cha og? je tunamaarifa yoyote juu ya vitanda vya wakati huo? kuna maandiko yanaonyesha watu wa kale hasa wafalme walikuwa wanaexaggerate vipimo vya vitanda ili waonekane warefu zaidi? cc http://jbqnew.jewishbible.org/assets/Uploads/401/jbq_401_og.pdf
Kwa mujibu wa chanzo hapo juu, makadilio ya urefu wa OG au Goriath ni kama mara mbili ya urefu wa Mtu wa kawaida, Je hili ni jambo la ajabu sana?
kwa genetics za kawaida inashindikana kuwepo mtu wa namna hiyo?