Mfalme wa Morocco - Kweli alistahili heshima ya Rais wetu Muadilifu Magufuli?

Mfalme wa Morocco - Kweli alistahili heshima ya Rais wetu Muadilifu Magufuli?

ALIYE-PHOTOSHOP PICHA YA MFALME WA MOROCCO ALIKUA NA MALENGO GANI?

View attachment 425961
· Kuuchafua Uisalmu.

· Kuichafua nchi ya Morocco ya utawala wake.

· Kumchafua Mfalme wa Morroco binafsi.

· Kuichafua serikali ya Magufuli.

· Kuchafua Zanzibar.

Angalia (zoom) vizuri picha sehemu iliyozungushiwa duara utaona katikati kuna mstari unaomaanisha kuna muunganiko wa picha mbili ndani ya picha moja, angalia zaidi kwenye sikio palipozingishiwa kuna muunganiko wa masiko mawili tofauti. Hiyo ilkua ni kuthibitisha tu mchezo uliofanyika kwa wale ambao si wajuzi wa mambo haya mpaka kupelekea kudanganyika na kuona kwamba picha hiyo ni ya kweli mpaka wengine kufikia kuanzisha nyuzi kutokana na picha hiyo.

Swali la msingi nini ilkua malengo ya mtu huyu?
Mimi mwenyewe nilivyoziona hizo picha nilishiwa nguvu mwili na roho kama wamezi photoshop watakuwa na lao jambo washughulikiwe
 
hata kama dunia imetuchoka,basi isitufanyie hivi!!

kipindi cha jk tulishuhudia viongozi wenye nguvu kubwa ya uchumi na kijeshi kutoka marekani,china,na mataifa mengine wakitua Tanzania.

Hakika zilikuwa ziara nzito kwa nchi hii na ziliipeleka Tanzania kilometa milioni kwenye dunia ya diplomasia.

Baadae awamu hii tukaacha kwenda nje ya nchi,serikali nzima ikaacha kwenda nje ya nchi.

matokeo yake tukaanza kupata wageni ambao ni kichekesho kwa taifa.Jamani tujirekebisheView attachment 426049 View attachment 426049
Naililia Tanzania , kutoka kuwa NCHI hadi kuwa kiji nchi !
 
Jamani please sio vizuri kuweka picha kama hizo, huyo ni kiongozi mkuu wa watu, tumheshimu kuna maisha mengine ni y ndani tuyawache huko. mbona wabongo kila kitu mnapenda kuvishape ili mpate kiki ya kisiasa. Hapana Hapana hizi picha ni za kweli lakini haziendani na bandiko. Mods huu ni uchochezi ondoeni
alipigia chumbani kwake au public area?
 
Hayo ni maisha yake binafsi. Anapenda kufanya shopping zake mwenyewe. Jamaa yuko poa sana,hana mbwembwe. Hakuna cha kushangaa. Ila hapoooo hao dada zetu hasa huyo mweusi ataachiwa mtaji akijua kusoma lugha za alama na akijituma
 
Huyu wa morocco waislamu mmeingizwa chaka ndugu zangu..ehehe! Amekula tisheti lake la mmea wa Marley kweli?
 
Kipindi hicho pia si mlikuwa mnasema jamaa keshauza nchi walipshana viongozi wakuu wa mataifa makubwa mawili mlipiga kelele sana ,sana kaja ustadhi huyu kelele tena ,!!mungu simamisha hii dunia nishuke maana nshachoka hawa watu wanaoitwa wana wa adamu maana hawana jema hata kidogo
 
Unaelewa unachoongea? Ni wakati wa ziara ya Rais wa Marekani nchini Tanzania, ndipo Marekani ilipoamua kutoa msaada mkubwa kabisa kwa nchi za kiafrika. Msaada mkubwa kabisa ulitolewa kwa Tanzania, iliyofuatia ilikuwa Ghana.

Ni pesa hiyo ya Wamarekani ndiyo iliyofanya miradi mikubwa kadhaa kama ile ya barabara na umeme iweze kutekelezeka.

Ni wakati huo ndipo maelfu ya kilometa za barabara zilijengwa. Leo tulivyo wajinga tunashangilia ujenzi wa njia moja ya barabara toka Mwenge hadi Morocco na njia mbili za barabara kutoka viwanja vya Furahisha mpaka uwanja wa ndege Mwanza, umbali usiozidi kilometa 4. Tulikuwa tunajenga maelfu ya kilometa bila mbwembwe lakini sasa tunajenga kilometa 4 kwa mbwembwe na sifa kila kona. Siamini kama sisi Watanzania ni wazima!

Kwa bandiko hili nami nakuunga mkono kuwa huenda sisi watanzania si wazima, ni kwa namna gani unaweza kufurahia sana kupewa msaada kisha ukabeza kitu unachokifanya kwa pesa yako mwenyewe?? Ni kwa vipi unaona ni sawa ukaishi kwa msaada kisha pesa yako mwenyewe ukafanyia sherehe ya siku moja??
Ok...sasa zimepanuliwa barabara mbili ya mwenge-morocco na Furahisha -Airport, je hayo maelfu ya kilomita nyingine yamekoma???
Watanzania aina yako hii Msambichaka Mkinga si wazima.
 
Jf ni balaa. Jamaa hoi tuache unafiki. Tuache ukweli uchue mkondo wake.
 
Lete picha halisi tumalize huu mjadala vinginevyo tunachukulia ni porojo tu.
 
Back
Top Bottom