Mfanyabiashara ahukumiwa kunyongwa Dar, alimuua mdai wake aliyempa hela amuagizie Fuso

Mfanyabiashara ahukumiwa kunyongwa Dar, alimuua mdai wake aliyempa hela amuagizie Fuso

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mfanyabiashara Hemed Ally amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa kukusudia Farihani Maluni.

Habari inaeleza Farihani alimpa milioni 30 Hemed amuagizie lori aina ya fuso na baada ya muda mrefu kupita bila ya lori kufika na mdai kulidai, Ally alimuita Farihani nyumbani kwake alipopanga eneo la Sharif Shamba, Ilala.

Hamjat Nassoro wakati akitoa ushahidi wake ambae ndie mmiliki wa nyumba hiyo alisema Ally hakumaliza kodi yake ya mwaka wa pili na alikaa miezi mitano pekee akidai amenunua nyumba Magomeni hivyo anahama.

Hamjat amesema wakati Ally akiishi kwenye nyumba hiyo alimuomba ruhusa aende kwa mjumbe ili achimbe shimo nje ya nyumba atapishe maji kutokana na shimo kujaa majitaka hata hivyo mjumbe hakutoa ruhusa.

Ally alirudi kwa Hamjat akimwomba amruhusu achimbe shimo kwa ndani ya uzio wa nyumba ambapo alimruhusu kwa maelekezo afukie vizuri kama kulivyokuwa, shimo hilo lilitumika kumfukia marehemu Juni 12, 2014.

Februari 9, 2015 Hamjat alipokea simu kutoka kwa polisi wakimtaka aende katika nyumba yake kuna tukio mshtakiwa alilifanya naye akaenda na baada ya kufukua walikuta mabaki ya mwili wa Farihani ukiwa umefungwa kamba mikononi na plasta maeneo ya fuvu(Daktari alihisi ilitumika kumziba mdomo na kumsababishia akose pumzi).

VIDEO 2015
 
Kwa hiyo, marehemu aliuawa kwa sababu alidai chake?

Na kwamba hela aliyokuwa anadai marehemu ilinunulia nyumba Magomeni badala ya kununulia Fuso kama marehemu alivyokubaliana na mshtakiwa/muuaji?

Kwa hiyo Marehemu na Muuaji walikuwa wanaaminiana kiasi cha marehemu kumpa hela muuaji akamwagizie Fuso?

Hivyo basi, bwana muuaji aliingia tamaa na kumdhulumu marehemu pesa na roho yake?

Kikulacho ki nguoni mwako!
 
Dah, hiii kesi nakumbuka hii,

Jamaa muuaji alipohama na kuhamia kusikojulikana.

Mpangaji mpya aliyehamia baadae ndiye aliyegundua shimo ambalo lilikuwa linatitia.

Ikabidi aitwe mwenye nyumba kukiwa na Mjumbe na polisi.

Hapo ndipo waligunduwa mabaki ya mwili wa marehemu.
 
Back
Top Bottom