jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,530
- 9,550
mbona story yako haijaisha mkuu alikamtwa vipi? maana ni majirani zetu hao ilalaMfanyabiashara Hemed Ally amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa kukusudia Farihani Maluni.
Habari inaeleza Farihani alimpa milioni 30 Hemed amuagizie lori aina ya fuso na baada ya muda mrefu kupita bila ya lori kufika na mdai kulidai, Ally alimuita Farihani nyumbani kwake alipopanga eneo la Sharif Shamba, Ilala.
Hamjat Nassoro wakati akitoa ushahidi wake ambae ndie mmiliki wa nyumba hiyo alisema Ally hakumaliza kodi yake ya mwaka wa pili na alikaa miezi mitano pekee akidai amenunua nyumba Magomeni hivyo anahama.
Hamjat amesema wakati Ally akiishi kwenye nyumba hiyo alimuomba ruhusa aende kwa mjumbe ili achimbe shimo nje ya nyumba atapishe maji kutokana na shimo kujaa majitaka hata hivyo mjumbe hakutoa ruhusa.
Ally alirudi kwa Hamjat akimwomba amruhusu achimbe shimo kwa ndani ya uzio wa nyumba ambapo alimruhusu kwa maelekezo afukie vizuri kama kulivyokuwa, shimo hilo lilitumika kumfukia marehemu Juni 12, 2014.
Februari 9, 2015 Hamjat alipokea simu kutoka kwa polisi wakimtaka aende katika nyumba yake kuna tukio mshtakiwa alilifanya naye akaenda na baada ya kufukua walikuta mabaki ya mwili wa Farihani ukiwa umefungwa kamba mikononi na plasta maeneo ya fuvu(Daktari alihisi ilitumika kumziba mdomo na kumsababishia akose pumzi).
jamaa alihama kabisa ilala na kwenda magomeni,mwenye nyumba akampata mpangaji mwengine ambae ni sharifu aliyekuwa anatibu watu kwa Quran.
sharifu alikuwa kila akilala usiku kuna nafsi inalalamika full maluwe luwe navhasa akienda au kupita hapi alpozikwa marehemu.
Basi ilifanyika dua na kugundua kuwa kuna kitu kibaya kimezikwa sehemu hyo,ndipo alipoitwa mwenye nyumba,baada ya kuja naye akakubali wafukue lakini mjumbe na mwenye kiti awepo na mwenyekiti nae akasema si vibaya wakawepo wale polisi wanaokaaga kata.
kwenye kuchimba ndo wakakutana na mwili wa huyo marehemu mwenye nyumba kubwanwa hana ajuacho mpangaji aliyetoka alipobanwa kidogo tu akafunguka yote.
ni kesi ya muda mrefu nimeshangaa mtu kuhukumiwa leo wakat ushahid ulikuwa waz kabisa