Hpn muuaji ndie aliye mpa pesa jamaa amuagizie gari Aina ya fuso ikapita muda bila kuletewa gari ndipo muuaji akamuita jamaa na Kisha kuja kumuua nyumbni kwake aliko panga bean muuaji
Kutoka mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam:
Godoro,pazia vyapokewa kortini kielelezo ushahidi kesi ya mauaji
www.ippmedia.com › habari › godoropa...16 Sept 2022 · MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepokea kielelezo cha godoro, pazia na nyavu ambavyo vinadaiwa kumfungia marehemu Farahani Maluni, ......
September 24, 2022 Udaku

MKEMIA Mwandamizi kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kaijunga Brassy ameiambia mahakama mabaki ya mwili wa marehemu Farihani Maluni, ikiwamo mifupa, hayakuonyesha majibu ya vinasaba kwa sababu ulikuwa na udhahiri mdogo.
Pia amedai mwili huo ambao ulifukiwa mbele ya nyumba iliyoko Ilala Sharif Shamba inawezekana ulichomwa moto kabla haujazikwa au ardhi aliyozikwa ilikuwa na chumvi, hivyo seli hazikuwa na muunganiko.
Brassy alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Joyce Minde wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati akitoa ushahidi wake dhidi ya Hemed Ally anayetuhumiwa kumuua Maluni na kumfukia.
Alidai kuwa vielelezo alivyovifanyia uchunguzi huo ni mifupa miwili ya paja, nguo ya ndani ya marehemu, plasta, mifupa ya kwenye kiuno, kamba na nguo yenye vifungo, meno, fuvu la nyuma la kichwa, mkanda, upindo wa suruali na kola ya shati.
Alidai barua ya kufanya uchunguzi wa vitu hivyo pia ilimtaka afanye uchunguzi wa vinasaba vya Abisalum Maluni ambaye ni baba wa marehemu, Faisal na Fahadi (watoto wa marehemu), ambapo aliwachukua mipanyuso mitatu ya kinywa.
Alidai kuwa uchunguzi huo wa vinasaba DNA ulikuwa na lengo la kufananisha mabaki ya marehemu na ndugu hao ili walinganishe vinasaba vyao kama Farihani ni ndugu yao.
Alidai vielelezo hivyo alivipa namba za usajili 115/2015 na baadaye alivihifadhi na akaja kuvifanyia kazi Julai 27/2018 na alibaini kuwa vielelezo namba moja hadi nane havikutoa majibu ya vinasaba.
Hata hivyo, kielelezo namba tisa - baba na watoto wa marehemu vilitoa majibu ya chembe halisi za urithi DNA , katika kulinganisha vilifanana vinasaba vya watoto na baba wa marehemu Farihani.
"Kielelezo namba moja hadi nane yakiwamo mabaki ya mwili wa Maluni havikutoa majibu kwa sababu havikuwa na udhahiri, inawezekana huo mwili ulichomwa moto kabla haujazikwa au ardhi aliyozikwa ilikuwa na chumvi, hivyo seli hazikuwa na muunganiko," alidai.
Awali Brassy alidai Februari 12, 2015 akiwa ofisini, alipokea vielelezo na barua kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam wakiomba uchunguzi wa vielelezo tisa.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Jumatatu saa tatu asubuhi. Inadaiwa Juni mwaka 2014, Hemed Ally alimuua Farihani Maluni eneo la Sharif Shamba ndani ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam
September 2022
Amedai kuwa haikuwa rahisi kujua chanzo cha kifo cha Maluni lakini kutokana na uwapo wa plasta eneo la fuvu, alihisi aliuawa kwa kuzibwa mdomo na kusababisha akose pumzi.
Dk. Mosha alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Joyce Minde wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati akitoa ushahidi katika kesi ya mauaji inayomkabili Hemed Ally.
Alidai kuwa Februari 9, 2015 akiwa katika eneo lake la kazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alipelekewa taarifa na Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa (RCO) wa Ilala, ikimtaka kwenda Sharif Shamba ndani ya Wilaya ya Ilala kuchunguza mwili wa binadamu unaohisiwa kufunikwa ndani ya ua wa nyumba.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali Salome Asey, Dk.Mosha alidai alichukua vifaa vyote vya kazi na kuongozana na askari polisi hadi eneo la tukio.
Walipofika eneo hilo majira ya saa sita kasoro mchana, Dk. Mosha alidai kuwa alikuta vijana wakiwa wameishaanza kufukua eneo hilo na ndani ya shimo walikuta matofali mapya, mabaki ya mwili yaliyokuwa yamezungushiwa ndani ya godoro, huku mikono ikionekana kufungwa kwa katani na fuvu likiwa na plasta.
Shahidi huyo alidai baada ya mabaki ya mwili huo kuonekana, wananchi waliokuwapo katika eneo hilo walikumbwa na taharuki wakitaka kumpiga mtuhumiwa aliyekuwapo pale na kumfanya ashindwe kufanya uchunguzi, ikabidi wachukue mabaki na nguo hadi Muhimbili.
Alidai Februari 10, 2015 alifanya uchunguzi akiwa na askari pamoja na ndugu wa marehemu waliotambua mavazi ya marehemu ikiwamo fulana ya pinki.
Dk. Mosha alidai katika uchunguzi wake, alibaini kuwa yale yalikuwa mabaki kweli ya binadamu kwa kuangalia fuvu, mpangilio wa meno na mifupa michache iliyokuwapo.
Baada ya kutoa ushahidi, Dk. Mosha aliiomba mahakama kupokea ripoti ya uchunguzi kama kielelezo na mahakama ilipokea kama kielelezo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho kutwa, Septemba 28, 2022 itakapokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.
Inadaiwa kuwa Juni, 2014 Hemed Ally alimuua Farahani Maluni eneo la Sharif Shamba, Ilala na kumzika mbele ya nyumba aliyokuwa akiishi.
Mfanyabiashara ahukumiwa kunyongwa hadi kufa Dar
www.mwananchi.co.tz › ... › Kitaifa1 day ago · Hemed Ally akitoka Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya ... leo Jumatatu Oktoba 17, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu, Joyce Minde, ...