Mfanyabiashara ashitakiwa kwa makosa 106 likiwamo la utakatishaji wa fedha zaidi ya Sh 1.5 bilioni

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Mfanyabiashara, Gaspton Danda (40) amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 106 likiwamo la utakatishaji wa fedha zaidi Sh 1.5 bilioni.

Wakili wa Serikali, Adolf Verandumi akishirikiana na wakili wa Serikali, Yusuph Aboud amedai mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka 69 ya kugushi, mashtaka 36 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na moja la utakatishaji wa fedha.

Verandumi akisoma hati ya mashata hayo alidai katika mshtaka hayo inadaiwa kuwa kati ya Agosti 26, 2020 hadi Novemba 10, 2020 maeneo benki ya CRDB Tawi la Msasani mshtakiwa huyo alighushi barua ya utambulisho na fomu ya kuombea mkopo ambapo alitumia akaunti za majina tofauti ya wafanyakazi 69 wa kampuni ya Savanna Mining.

Katika shtaka la kugushi inadaiwa kuwa kati ya Agosti 26, 2020 eneo la Benji ya CRDD Tawi la Msasani jijini Dear es Salaam mshtakiwa huyo aligushi barua ya Oktoba 26,2020 ikionyesha Jonson Clement bi mfanyakazi wa kampuni ya Savanna Mining.

Katika shtaka lingine mshtakiwa huyo aligushi fomu ya mkopo kiasi cha Sh49 milioni kwenye akaunti ya CRDB yenye jina la Jonson Clement huku akijua kufanya hivyo ni kosa.

Katika shtaka lingine inadaiwa kati ya Oktoba 31, 2020 maeneo hayo mshtakiwa huyo alljipatia fedha Kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Sh49 milioni kwenye akaunti ya CRDB yenye jina la Jonson Clement Hulu akijua kufanya hivyo ni kosa.

Katika shtaka la mwisho la utakatishaji wa fedha inadaiwa kati ya Agosti 26, 2020 hadi Novemba 10, 2020 mshtakiwa huyo alijipatia zaidi ya Sh1.56 bilioni huku akijua ni zao ya makosa aliyoyafanya kujipatia kiasi hicho.

Chanzo: Mwananchi
 
Tuulize Kwanza kabila....ili tumsifie au tumlaumu!

Hapa ndipo alipotufikisha magufuli
 
Hawa walipiga bank kama 5 hivi, naona wameanza na ya CRDB, bado kuna NBC n.k zinakuja ila walipovuta parefu ni NBC kama Bilioni 4 hivi...kuna mchaga mmoja kwenye hiyo crew yao huko jela ndio balaa kabisa
Fafanua zaidi walkua wanazipiga pigaje hizo pesa[emoji848]
 
Walighushi majina na identity za kuonyesha wafanyakazi wa kampuni zao wanahitaji mikopo, kukamilisha hilo walifoji bank statements, vitabu vya mahesabu n.k wakaanza kulamba hela za bank tangu 2019. N.B.C waliipiga 4.7B kesi yao ilianza kusikiliza mwezi wa tatu 2022

Ring ya hawa jamaa ni wale waliokuwa wanazipiga banks miaka ya kuanzia 2007, baada ya kutimuliwa na wengine kufungwa ndio wakafungua vi micro finance na makampuni mengine ya IT n.k

Hii ni moja crew ya vijana matapeli wenye hela wa mbezi beach wana kiu ya hela
Screenshot_20221109-023843_Samsung%20Internet.jpg
Screenshot_20221109-023853_Samsung%20Internet.jpg
Screenshot_20221109-023900_Samsung%20Internet.jpg
Screenshot_20221109-023915_Samsung%20Internet.jpg
Screenshot_20221109-023929_Samsung%20Internet.jpg
 
Kweli life begins at 40. Lakn kwa mtonyo walionao pesa itatembea kila kona na kuna wakili atakula parefu.
Subr tuone mwisho wa muvi
 
Mfanyabiashara, Gaspton Danda (40) amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 106 likiwamo la utakatishaji wa fedha zaidi Sh 1.5 bilioni.

Wakili wa Serikali, Adolf Verandumi akishirikiana na wakili wa Serikali, Yusuph Aboud amedai mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka 69 ya kugushi, mashtaka 36 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na moja la utakatishaji wa fedha.

Verandumi akisoma hati ya mashata hayo alidai katika mshtaka hayo inadaiwa kuwa kati ya Agosti 26, 2020 hadi Novemba 10, 2020 maeneo benki ya CRDB Tawi la Msasani mshtakiwa huyo alighushi barua ya utambulisho na fomu ya kuombea mkopo ambapo alitumia akaunti za majina tofauti ya wafanyakazi 69 wa kampuni ya Savanna Mining.

Katika shtaka la kugushi inadaiwa kuwa kati ya Agosti 26, 2020 eneo la Benji ya CRDD Tawi la Msasani jijini Dear es Salaam mshtakiwa huyo aligushi barua ya Oktoba 26,2020 ikionyesha Jonson Clement bi mfanyakazi wa kampuni ya Savanna Mining.

Katika shtaka lingine mshtakiwa huyo aligushi fomu ya mkopo kiasi cha Sh49 milioni kwenye akaunti ya CRDB yenye jina la Jonson Clement huku akijua kufanya hivyo ni kosa.

Katika shtaka lingine inadaiwa kati ya Oktoba 31, 2020 maeneo hayo mshtakiwa huyo alljipatia fedha Kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Sh49 milioni kwenye akaunti ya CRDB yenye jina la Jonson Clement Hulu akijua kufanya hivyo ni kosa.

Katika shtaka la mwisho la utakatishaji wa fedha inadaiwa kati ya Agosti 26, 2020 hadi Novemba 10, 2020 mshtakiwa huyo alijipatia zaidi ya Sh1.56 bilioni huku akijua ni zao ya makosa aliyoyafanya kujipatia kiasi hicho.

Chanzo: Mwananchi
Sildenafil is used to treat men who have erectile dysfunction (also called sexual impotence). Sildenafil belongs to a group of medicines called phosphodiesterase 5 (PDE5) inhibitors. These medicines prevent an enzyme called phosphodiesterase type-5 from working too quickly.
 
Back
Top Bottom