Huyo jamaa alikuwa hatari bin danger.
Nakumbuka kisa almanusura atupitie.
Ni miaka zaidi ya 20 iliyopita.
Tumeenda zetu Morogoro kumchukua mdogo wetu marehemu aliyefariki kwa ajali.
Tuko na gari Prado mpyaaa ndo kwanza zimeanza kutoka.
Tulioenda kuchukua maiti na tunarudi Dar , mmoja wa tuliokuwa nao alimtambua Leshesya baada ya kusimama sehemu fulani.
Ilikuwa jioni na kagiza kanaingia.
Huyooo Lesheya akatuambia nyie msiagize, msiagize kabisa chakula, mimi nitawaletea chakula, nyie ndugu zangu.
Tulikataa, lakini haikupita dk 5 tayari akaleta sahani nne za chips mayai!
Ambacho huyu Lesheya hakujua ni kwamba kati ya tulikuwa katika msafara alikuwemo ndugu ambaye ni kachero mbaya sana, na alitupa ishara tusikiguse chakula kile.
Baadaye tusiomfahamu yule kachero akatuambia, tatizo ni hilo gari, tungekula tu takrima ya huyo Lesheya, aidha tungekufa au kusinzia na kunyang'anywa hilo gari.
RIP Lesheya.