Mfanyabiashara kuongoza Shirika la Umma Rais Samia unaenda kusiko

Uko sahihi!
 
Tatizo ni nini?
 
Hilo ni kweli kabisa, sijui kama ulivaa mashati ya "Victory" yaliyotengenezwa na Urafiki miaka ya 1980-81, hii ilikuwa baada ya vita ya Kagera.
Uchumi wa kibepari una ubunifu kw mtu mmoja mmoja, lakini downside in self interests.
Hivi tujiulize China na Centrally Planned Economy mbona wamefanikiwa sana ina the last 60 years?
Tena wamefanikiwa kiasi kuwa wanaanza kuitia wasiwasi Marekani.
Wamefanya vipi, kile sisi tunachoshindwa?
 
China na Tanzania ni tofauti sana, sidhani kama ofisi ya CAG ya China inarekodi madudu mengi kama haya yanayofanyika hapa nchini kwetu.

Kuna mwanazuoni mmoja aliwahi kusema 'ujamaa unakufa pale ambapo pesa za wachache zinashindwa kuendelea kutunza maisha ya walio wengi'.
 
Mkuu hatuna tofauti yoyote na China.
Ila wao wako focised na wanamaanisha kile kinachotakiwa kufanywa.
Kule wezi wa mali za umma mwisho wao ni mmoja: RISASI ya kichwa.
Hapa kwetu mwizi anaundiwa tume , mtuhumiwa anawahonga Tume , mwisho wa sik anapelekwa kwingine kuiba.

We are not serious.
 
Ujamaa upo kwa wale wenzangu na mimi wenye umri fulani tena umebaki kwenye kumbukumbu zetu.

Uhalisia ni vigumu kumpata kiongozi wa taasisi za kiserikali akawa hana mawazo wala nia za kutafuta mali binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…