Hii ndio Taarifa yake mpya aliyoisambaza kwa Umma, kwamba ameamua kuahirisha mpango wake wa kuhamishia biashara zake nje ya nchi baada ya Rais mpya Samia Suluhu kuonyesha mwanga wa kujali wawekezaji.
Sugu tayari alishapata ofa ya kupewa maeneo ya kuwekeza kwenye nchi tatu za Africa ikiwemo Zambia, Malawi na South Africa, hata hivyo ameahirisha mpango huo baada ya kusikia maneno kutoka kwa Rais mpya aliyesisitiza wawekezaji kutendewa haki .
Sasa tuendelee kusikilizia kama yanayosemwa na Mh Rais ndio yatakayojiri.