Sugu angeendelea kuwa mbunge asingepata akili ya kuwekeza fedha alizopata kama kiinua mgongo. Tena ameamua tayari kesha chelewa.
Tanzania kila baada ya miaka mitano, tunatengeneza ma milionea wapya 400 ambao ni wabunge. Badala ya pesa waloyoipata wawekeze kufungua ajira mpya, wanaenda kuhonga wajumbe ili warudi bungeni.
Kukomesha tabia hizi, katiba mpya iweke vigezo vifuatavyo:-
1. Mbunge aruhusiwe kugombea kwa vipindi viwili tu. Akimaliza afanye kazi nyingine.
2. Kwa anayetaka kuendelea, tuweke kigezo cha awe ameajiri watu wasiopungua 500 na wawe wanalipa P.A.Y.E. Hii itasaidia kuongeza uwekezaji.
3. Kwa shughuli za shamba, uvuvi na ufugaji, tuweke sharti la mfano mtu awe analima heka kuanzia 1,000
4. Wasafirisha mazao mfano mtu akiweza kupata soko nje ya nchi, anachukua mazao na anayaprocess na kusafirisha, huyo pia awe na sifa za kuongeza toka 10yrs na kuendelea.
Hapa tutakuwa tumelazimisha badala pesa kuhongwa wajumbe, itumike kufanya uwekezaji.
Sugu hongera sana