Mfanyabiashara Timotheo Wandiba ahukumiwa miaka 81 kwa kujipatia Bilioni 2.1 kwa udanganyifu

Mfanyabiashara Timotheo Wandiba ahukumiwa miaka 81 kwa kujipatia Bilioni 2.1 kwa udanganyifu

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kwenda Jela miaka 81 Mfanyabiashara Timotheo Wandiba baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kujipatia fedha ambazo ni Sh.Bil 2.1 kwa njia ya udanganyifu.

Hukumu hiyo imotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri ambapo amesema Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa makosa 27 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

"Katika makosa hayo 27 kwa kila kosa unahukumiwa kwenda jela miaka 3 ambapo jumla itakuwa ni miaka 81 lakini adhabu hiyo utataumikia sambamba," amesema Hakimu Mashauri.

Imeelezwa kwamba kati ya December 2012 na April 2014 waligushi fomu za makubaliano ya kuhamisha fedha Benki ya BOA ambazo ni BILIONI 2.1 kwenda NMB.


Chanzo: Millard.com
 
Waandishi wa kibongo bana ni makanjanja hatari...
Hapo ataenda jela MIAKA 3 tu na sio 81...

Makosa 27 kila kosa 3 years ...hapo sentence ni concurrent so ataserve miaka 3 tu..

Uyo miladi ayo naye mbulula si karipoti miaka 81
 
Hapo anakaa miaka mi 3 tu maana wamesema adhabu zote anazitumikia sambamba
Niliwaza kuliko kumuhukumu miaka 81 si wangerahisisha tu kwa kusema amefungwa maisha. Kumbe Miaka mitatu tu anamaliza kesi anarudi zake kutumua mihela yake.
 
Wewe jamaa bana, kumbe unamaanisha Tzshs mimi nilidhani ni KES.
 
Bada ya mda tu atatoka hukumu za miaka mingiii hivyo wakikata rufaa tu huwa wanatoka
kwani hujaelewa? atatumikia miaka mitatu kwa makosa 27 na hukumu hiyo itakwenda sambamba.
 
Back
Top Bottom