Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kwenda Jela miaka 81 Mfanyabiashara Timotheo Wandiba baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kujipatia fedha ambazo ni Sh.Bil 2.1 kwa njia ya udanganyifu.
Hukumu hiyo imotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri ambapo amesema Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa makosa 27 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
"Katika makosa hayo 27 kwa kila kosa unahukumiwa kwenda jela miaka 3 ambapo jumla itakuwa ni miaka 81 lakini adhabu hiyo utataumikia sambamba," amesema Hakimu Mashauri.
Imeelezwa kwamba kati ya December 2012 na April 2014 waligushi fomu za makubaliano ya kuhamisha fedha Benki ya BOA ambazo ni BILIONI 2.1 kwenda NMB.
Chanzo: Millard.com