milele amina
JF-Expert Member
- Aug 16, 2024
- 6,045
- 8,080
Anaitwa GIDEON MLOKOZI MASHANKARA ana umri wa miaka 30, mkazi wa Tabata Segerea,
Kazi yake ni mfanyabiashara wa kuuza magari lakini pia ni mwanaharakati huru wa mitandaoni,hajulikani alipo siku ya saba leo baada ya kutekwa na kupotezwa.
Alitekwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari wa jeshi la Polisi siku ya Ijumaa ya tarehe 02 August 2024 majira ya Saa 2 :00 usiku.
Akiwa katika ofisi ya magari ya rafiki yake inayojulikana kama RAPHAEL STAR iliyopo maeneo ya Segerea Stand.
Watu hao waliojitambulisha kama askari wa Jeshi la polisi walikuwa watano,walivamia ofisi hiyo wakiwa wamevalia kiraia na kumuweka Chini ya ulinzi.
Ndipo alipowahoji waoneshe vitambulisho lakini wakakaidi na kudai wanampeleka kituo cha polisi Tabata,atajua huko huko.
Walitumia nguvu na kumfunga pingu kisha wakamuingiza kwenye gari walilokuja nalo aina ya Landcruiser hardtop, ikiwa haina namba
Lakini mashuhuda waliokuwa nje ya ofisi wanasema,gari hilo halikuwa na namba kwa nyuma ila kwa mbele liliandikwa "STL" tu.
Gari hilo halikuelekea Kituo cha polisi Tabata kama walivosema bali lilielekea njia ya kwenda kinyerezi.
Familia ilianza juhudi za kumtafuta vituo vyote vya Polisi Jijini Dar es saalam bila mafanikio
Tulianza kituo cha polisi Tabata, tukaambiwa hayupo na hawana taarifa zake,Tukaenda kituo cha polisi cha Staki Shari,Kinyerezi na Buguruni pia hawakuwa na taarifa zake
Kesho yake asubuhi tuliendelea na vituo vingine tulianzia Central, Oysterbay na vituo vyote bila Mafanikio
Tumezunguka Hospitali zote jijini Dar es saalam na vyumba vya kuhifadhia maiti "Mortuary" bila Mafanikio.
Tulifungua taarifa kituo cha Polisi cha Staki Shari na kupewa RB namba STK/RB/6642/024
Baada ya siku ya tano bila Mafanikio tumeenda Central polisi kufungua jalada la Uchunguz,tumeambiwa upelelezi unaendelea.
Kwa niaba ya Familia tunaomba mtu yoyote mwenye taarifa kuhusu ndugu yetu awasiliane na Baba yake GIDEON kwa namba 0786878133 au kwa namba ya rafiki yake ambayo ni 0624497811
Asante sana.