DOKEZO Mfanyabiashara wa Magari, Gideon Mlokozi Mashankara amepotea

DOKEZO Mfanyabiashara wa Magari, Gideon Mlokozi Mashankara amepotea

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kazi yake ni mfanyabiashara wa kuuza magari lakini pia ni mwanaharakati huru wa mitandaoni,hajulikani alipo siku ya saba leo baada ya kutekwa na kupotezwa.

Alitekwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari wa jeshi la Polisi siku ya Ijumaa ya tarehe 02 August 2024 majira ya Saa 2 :00 usiku.
Kuanzia tar. 02 August mpaka leo ni siku saba?
Au taarifa hii imeandikwa lini?
 
Watanzania TUANZE KUJILINDA.

Hayawani vichwa vimepata moto. Ogopa sana mwanamke akishaonja damu ya mtu

Mlinipuuza niliposema tukaipinge sheria inayowapa kinga TISS wanapoamua kuua

Kumbukeni Dotto Magari ni chawa kiherehere hivyo kumuuza mtu adakwe ni chap kwa haraka
Dotto magari kaingiaje hapo ww?
 
Polisi inabidi waanze kutoa taarifa effectively na efficiently kuhusu haya mambo hata kama ni uzushi inabidi wafuatilie na walete majibu yanayoeleweka (Hio ndio kazi yao na wanalipwa kwa kazi hizo); Mzaha mzaha mwisho hutumbuka Usaha... (Ingawa Usaa ushatumbuka zamani sana ni wakati wa kufanya amputation)
 
Ili kukabiliana na huu utekaji wa kikosi kazi ambacho kipo chang'ombe Kwa mujibu wa hotuba ya mh mbowe,serikali inatakiwa ilegeze masharti ya umiliki wa silaha kama ilivyo marekani ili tuwashughulikie Hawa wahuni wanaojifanya hawajulikani wakati wanajulikana na niwajingawajinga ambao uwezo wao wa kuchanganua mambo ni sifuri.
 
Sheikh kirahisi tu ivo? Hawa watu hawaheshimu haki Wala maisha ya raia, unaweza kufatilia wakakukamata na wewe, mtu anayeheshimu kazi yake hawezi kukataa kutoa kitambulisho anapofanya arrest.....
Ni kweli au unaweza kupigwa hata shaba biashara ikaishia hapo , ila serikali ijitahidi kudhibiti mambo haya , maana ikiendelea tusije kuwa kama southafrica, wahuni wataanza kuhukumiana mtaani kiholela, maana southafrica walianza kiutani utani sasa hivi wahuni wanakusanya hadi kodi kwa wafanyabiashara na serikali imeahindwa kudhibiti, usipolipa protection fees wanakumaliza

 
Back
Top Bottom