Mfanyakazi anayeshangilia Ongezeko la Mshahara hajui Hisabati

Mama Samia hajaleta mfumuko wa Bei,
Suala la mfumuko wa Bei Ni dunia nzima kutokana na Vita inayoendelea uko Ukraine.
Kwenye Corona ulikuwepo? Corona na hiyo vita kipi kilipaswa kutuathiri? Urusi na Uarabuni wapi ni karibu Kwetu?
 
Hongera mkuu Benson angalau umekomaa,umeanza kuleta mada jukwaani ambazo zinasomeka lakini pia zina jadilika kwasababu zina maslahi kwa watu,nikwambie ukweli kipindi cha nyuma kidogo ilikuwa tukiona thread zako hata hatuhangaiki kufungua tunajua ni utopolo tu uliojaa mambo binafsi ya watu mara Mbowe mara Mrema mara Mnyika.Kuna hatua umesogea hongera zako mzee baba.
Kuhusu isue ya increment ya mishahara uko sahihi,lakini hata ungekuwa wewe unge opt njia aliyoichukua mama.Hali ya mfumuko wa bei iliyopo sasa kwa sera tulizonazo,kwa brain tuliyonayo inayosimamia na kuendesha mambo ya kiuchumi ningumu kurudi tulikokuwa kwahiyo acha tu waliopata increment wafurahie angalau hata Kama haitawasaidia kiuchumi lakini itawasaidia kisaikolojia.
 
Mkopeshaji mwenyewe ni CRDB unaomba mkopo leo unapewa baada ya miezi mitatu!?
 

Kwahiyo ulitaka asiongeze? Nenda Chato wewe!!
 
Kwa hiyo angekuwepo Magufuli angezuia bei ya mafuta isipae duniani?Mbona mnajipa matumaini hewa?Na ni kipi kinakuumiza watumishi wakiongezewa mishahara?Ni lipi tatizo wakipata nyongeza?
 
Magufuli alidanganya wananchi kwamba tunajenga kwa fedha zetu kumbe alitumia mikopo ya mabeberu.
 
Kaongeza 23%, mwakani uchumi wetu ukifanikiwa kujuwa anaweza akaongeza zaidi ya 23%, mwaka utakaofuata 2024/2025 uchumi ukiendelea kukuwa natumaini ataongeza tena.

Kwa nyingeza hizo unategemea akose kura za Wafanyakazi?

Atapata kura nyingi sana toka kwa wafanyakazi na familia zao.
 
Watumishi pokeeni hicho kidogo japo ninyi na watoto wenu mtajamba siku mbili tatu .
 
Wivu na husuda tuu..

Aliyekwambia vitu vitapanda daima ni nani?

Kipi Bora kupata hilo ongezeko au kukosa..

Unakuta na wewe eti ni think tank wa Sukuma gang 😆😆,bure kabisa.
 
Sasa wewe ulitakaje?;Magu hakuongeza Mshahara tukamlaumu Mama Samia ameongeza Mshahara mnasema tusishangilie sasa binadamu tupewe kitu gani ndipo tuweze kufurahi??.Hata km unamchukia mama Samia lkn ktk hili apongezwe.
 
Kwenye Corona ulikuwepo? Corona na hiyo vita kipi kilipaswa kutuathiri? Urusi na Uarabuni wapi ni karibu Kwetu?
Kwani kipindi Cha corona kulikuwa na tatizo la mafuta duniani?Tatizo la mafuta ndio linalosababisha mfumuko wa bei Hebu punguza chuki kidogo mfumuko wa Bei sio Tanzania pekee ni duniani kote kwani huyo Magu wenu angekuwepo angezuia Bei ya mafuta kupanda Kama sukari tu ilimshinda kuzuia kupanda bei ambayo inazalishwa hapahapa Tanzania sembuse mafuta tuacheni kidogo watumishi tufurahi kidogo tumeteseka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…