Mfanyakazi usithubutu kuacha kazi kwa kushawishiwa kwa njia yoyote ile

Mfanyakazi usithubutu kuacha kazi kwa kushawishiwa kwa njia yoyote ile

Si kweli kabisa hawa wa forex .... Wanapata hela kwa training.. Lakini hawafanyi trading wao wenyewe.. Mtu anayefanya trading halisia kwa a/c yake , hawezi kusema hivyo.. Ni biashara ya up and down, sasa yeye anajihakikishia vipi kuwa mwezi ujao mambo yatakuwa mazuri..Sound tu za forex..
Teh, kila muwamba ngoma....
 
😀 Hapo imebidi nicheke. Yap, you have said it perfectly well. Falsafa yangu siku zote ni kuwa "maisha ni mtazamo" na mtazamo wa mtu (au hisia zake) - ambao ni wa kipekee kwa kila binadamu - ndio unaoainisha mafanikio, mkwamo hata kuanguka kwake. Wengi huishia kushangaa sana wanapogundua kuwa adui zao hasa au hofu zao kuu ZIMO NDANI YAO na si nje na kwamba MWISHO WA YOTE kufaidi au kutofaidi maisha ni jinsi hisia zako zilivyokuongoza.
Ume "drift" vizuri sana na wewe hapo, mitazamo kimaisha yatofautiana, kuridhika kwa ki kimaisha lazima itakuwa tofauti na mwenzako..Je yamaanisha tusisukumane kupata maendeleo?! Je unapomsukuma mwenzako yaweza akasukumika kwenye shimo la maendeleo au la kumpoteza? Ebu endelea kufafanuwa boss Drifter
 
Niko kwenye ajira mwaka wa pili huu.
Nimeanza Kutrade Forex mwezi September.
Kwa mpunga naopiga next month naandika resignation letter. Kwanini, kwa sababu mshahara wangu wa mwezi naweza kuupata ndani ya week moja soko likikubali.
Kuajiriwa ni utumwa, ukweli utabaki milele
Uoga wako Umasikini wako
hakika upo sahihi...ukitaka pato zuri ndivyo utumwa kwa maslahi ya wengine unavozidi
 
Habari wanajukwaa!

Uzi huu ni maalumu kwa ajili ya waajiriwa wa serikali na wale wa sekta binafsi. Pia unawahusu wale watakaoajiriwa siku za machoni.

Kuna upuuzi siku hizi unasambazwa sana na watu mbalimbali unaohusu kupondea ajira(kuajiriwa) na kutukuza kujiajiri.

Katika haya maisha kila mtu ana mpango kazi wake kichwani wa kumwezesha kufika mahali pale anapopahitaji, ili kufika mahali unapopalenga unahitaji ushauri kwa sehemu ndogo sana.

Kwanini niseme ushauri unahitajika kwa sehemu ndogo sana?

1. Wewe ndiwe mwenye picha halisi ya kule uendako na utakako

2. Watu wengi hawawezi kubeba mzigo wa mwingine kama mzigo wao. Watu wamejawa wivu (hasa ngozi nyeusi)

3. Watu wanaishi kwa maigizo, mfano humu ndani mtu utakuta amekosa ajira na sasa anasajili line kwa mwezi anaingiza laki mbili tu ila ukiomba ushauri yeye atajiintroduce kama mmiliki wa kampuni na hana mpango wa kuajiriwa tena maishani mwake.

Unaweza kujiajiri ukiwa mwajiriwa na kuzikabili changamoto nyingi kwa urahisi zaidi ya yule asiyeajiriwa. Kivipi?
(A) Ni rahisi kupata mtaji
(B) Ni rahisi kukuza mtaji wako pindi unapoona biashara yako ina soko zuri
(C) Unaweza kuwageuza wafanyakazi wenzako kuwa kama soko la awali huku ukisoma somo la biashara kwa vitendo

Note:
Usiache kazi mpaka pale utakapoona biashara yako inaweza kuendelea kukuingizia fedha hata kama unaumwa ,hapa namanisha mpaka pale itakapojiendesha yenyewe. Uwe jela, uwe umelazwa n.k system iwe inaoperate, kinyume na hapo usithubutu.

Pia napenda kusema kuwa mafanikio ni pale moyo wa mtu unaporidhika na vile alivyo na si kumiliki magorofa au kampuni. Mwingine hata kuwa mpika chai wa waziri kwake ni mafanikio hivyo acha kumbughudhi ili ajione mnyonge aache kazi.
rich dad poor dad hiki kitabu nakipenda kimegusa vizuri sna habari za kuajiriwa na kujiajiari...
 
Tunaofanya Kazi kwa Mhindi Uzi huu hautuhusu
 
Kuna jamaa yangu anataka acha kazi aje kufuga kuku ila nimemwambia kuna changamoto kubwa huku dunian kasema Kazi za kuajiriwa zimemchosha

...Uwoga tuu wa maisha mkuu, hivi out of 50 mill plus Tanzanian walioajiriwa ni wangapi?
 
Niko kwenye ajira mwaka wa pili huu.
Nimeanza Kutrade Forex mwezi September.
Kwa mpunga naopiga next month naandika resignation letter. Kwanini, kwa sababu mshahara wangu wa mwezi naweza kuupata ndani ya week moja soko likikubali.
Kuajiriwa ni utumwa, ukweli utabaki milele
Uoga wako Umasikini wako

.....Watu wamesubiri salary increment for almost two yrs, juzi nimesikia ongezeko ni around TZS 20,000.... ambayo ni sawa na income ya muuza maji kwa siku....Anyway kupanga ni kuchagua.
 
Niko kwenye ajira mwaka wa pili huu.
Nimeanza Kutrade Forex mwezi September.
Kwa mpunga naopiga next month naandika resignation letter. Kwanini, kwa sababu mshahara wangu wa mwezi naweza kuupata ndani ya week moja soko likikubali.
Kuajiriwa ni utumwa, ukweli utabaki milele
Uoga wako Umasikini wako
Je biashara ikigoma una mbadala au maana hiyo forex sio uhakika
 
Daaaah we jamaa si juzi tu ulikua unalilia mshahara leo hii ushakua tajiri wa forex unawaambia wenzio waache kazi?
Ama kweli maisha bila unafiki hayaendi
e4558cdaecb9ff64737d9dbf5e972330.jpg
944704163041c8a1e080fba5c6f2fe69.jpg
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji119] [emoji119]
 
Unadhani nategemea ajira moja.
Niko Serikalini, niko Private company (japo kwa kuibia napo nataka kuwatema), niko na biashara zangu mbili (Forex imekua ya tatu sasa).
Na hizo Freezer Tabora niliamua kuuza baada ya mtu nilomweka kuuza samaki kunizingua.
Maisha kupambana. Ukilegea subiri upambaniwe. Kalagabaho
Hatari sana chief [emoji23] [emoji23]
 
Kuna watu wameibuka siku hizi, wanajiita Inspirational Or motivational speakers, hawa wanakula sana hela za vijana kwa semina za ujanja ujanja wakihamasisha vijana wajiajiri wakati wao wameajiriwa.
Hili neno fursa siku hizi nalo limekuwa fursa
 
Niko kwenye ajira mwaka wa pili huu.
Nimeanza Kutrade Forex mwezi September.
Kwa mpunga naopiga next month naandika resignation letter. Kwanini, kwa sababu mshahara wangu wa mwezi naweza kuupata ndani ya week moja soko likikubali.
Kuajiriwa ni utumwa, ukweli utabaki milele
Uoga wako Umasikini wako
Ila make sure
1.ushakua pro na una make consistent profit by your own analysis sio kwa signal za mtu
2.grow your bank acc and not your trading acc in case of any thing unaweza fund tena trading acc bila kuyumba
Ni uamuzi mzuri
 
Huu uzi umetawaliwa na watu wenye vichwa vigumu sijapata kuona japo sijawai kuajiriwa pia sijawai kujiajiri bado lakini concept nzima ya kuacha kazi nimeielewa vilivyo labda nijaribu kui summarize

“unakusanya mtaji kwenye ajira uliyoajiriwa una invest katika shughuri za kijasiriamali izo biashara zako zinakuwa mpaka zinazidi mapato ya mshahara unaoupata kwenye ajira yako na zinavyokuwa ivyo sasa zinaitaji usimamizi wako wakaribu hivyo ndio muda sahihi wa kuacha ajira yako na kusimamia biashara zako kwasababu zinakuingizia mapato kuliko kwenye ajira yako pia zinaitaji usimamizi wakaribu hii inamaana katika stage hiyo weutegemei ajira tena"
Hiyo ndo concept fupi sasa wengi wenu humu munaposikia kuacha kazi nahisi uwelewa wenu ni mtu from no where tu anaacha kazi ndomnavyoelewa

NB: kuajiriwa kutakufanya uwishi na stress maisha yako yote hii aina maana kwamba usiajiriwe, ajiriwa ili ukusanye mtaji siri ya utajiri ilishafaamika sasaivi sio kurumbana tu apa
Watu wanasema kuajiriwa ni utumwa sijui stress na bla bla blahh
Kama hiyo ndio sababu tu ya kukufanya uache kazi unafeli
Kujiajiri ni utumwa sana sana hasa stage za mwanzo unapotaka kusimamisha brand yako na pia kuajiri watu ni stress sana kuliko kuajiriwa yaan ku organise people watembee na vision zako with accuracy maaaan si mchezo
Talking from experience
So we jiajiri tu lakin zisiwe hizo sababu mbili eti ajira ni utumwa sijui stress
 
Daaaah we jamaa si juzi tu ulikua unalilia mshahara leo hii ushakua tajiri wa forex unawaambia wenzio waache kazi?
Ama kweli maisha bila unafiki hayaendi
e4558cdaecb9ff64737d9dbf5e972330.jpg
944704163041c8a1e080fba5c6f2fe69.jpg

huyu jamaa anashauri watu waache kazi ili wawe kama yeye, aache mambo ya hovyo
 
Back
Top Bottom