BLACK MOVEMENT
JF-Expert Member
- Mar 11, 2020
- 4,548
- 11,901
Gazeti la Raia mwema leo, Julai 10, 2024, linaeelezea utajiri wa kutisha wa mabosi wa TRA, hawa ndio wale hutuma vijana wao waje kiusumbua mtaani na kodi za Tsh. 100,000 wakati kuna watu wanakwepa kodi za trilion za pesa kwa makubaliano.
Hawa ndio wale tunaambiwa tutunze amani ili waibe na kula kwa amani, yaani ukisikia tenzi za amani yetu sababu ni hizo hapo.
Rais anasisitiza tulipe Kodi, Mwigulu anasisitiza tulipe kodi, Ila shida inakuja kwenye matumizi ya hizo kodi tunazo komaliwa tulipe na tunaambiwa kulipa kodi ni uzalendo. Na hawa watu ni kama Raisi anawaogopa sana.
Ndio maana nashangaa sana wanao jitolea mara kujenga Zahani mara shule, kwa sababu base ya kujitolea haiwezi kuwa habari kama hizi za fedha kupigwa na wengine mnambiwa wajitolee kujenga shule au Barabara au changishaneni.
Jiulize watuhumiwa wa report ya CAG wanafanywaga nini? hawakuna wanacho fanywa na sio hivyo tu bali pia husamehewa.
Hawa huwezi sikia Wakina Makala, na kampuki yake wanawazungumzia, huwezi wakuta waimba pambio humu wanazungumzia mambo kama haya. Wao wako busy na Mbowe na Lissu.
Kule Kilimanjaro kuna raia wanachangishana kulima barabara, vipi wanapo sikia habari kama hizi?