Mfanyakazi wa TRA akutwa amehifadhi pesa taslimu Tsh. Bilioni 7 nyumbani

Mzee B7,
Utaweka mzunguko gani zaidi ya kutengeneza unnecessary attention [emoji19]
B7 ukiziweka ktk mzunguko ni hela ndogo sana..

Iweke tu ktk ujenzi wa kasri moja la maana uone hiy hela inavyopotea ktk level ya msingi tu..
 

Kwa sie wenye vinasaba vya kitomaso ni ngumu kuamini hayo madai .
 
yaani TRA inatakiwa ivujwe isukwe upya. Mimi nilisha wahi kulipia kodi ya jengo kwenye office za TRA Bagamoyo nikapewa list lakini huku Dar ikawa inaonyesha sijalipa. Nikaenda uffisini kwao Dar wakaniambia TRA ni kama black hole ikisha ingiza pesa huwezi kuzitowa. Sasa nikawa na jiuliza kama mtu akilipa kodi eneo moja hakuna system ya kuonyesha kwenye eno lingine zimelipwa inawezekana kodi nyingi haziripotiwi zinaishia mifukoni mwa watu wachache.
 
Kama taifa lazima tuwe na dira ya taifa na siyo maono ya Rais
 
Nyingi zinapigwa
 
System nzima ya nchi imeoza mkuu siyo TRA pekee
 
Waziri mwenyewe wa fedha chenga tu PHD yake ya mchongo wizara ya fedha wamewekwa watu wa michongo michongo,ukabila,kujuana kwingi,hakuna uwajibikaji fedha TRA wanakusanya na kugawana tu,kweli Tz ni shamba la bibi.
 
CCM ni kama ukoo wa panya tu wala msiwategemee eti Takukuru kuwasaidia
Ukoo wa panya uko hivi;
Baba mwizi
Mama mwizi
Watoto wezi
Ndugu wengine wezi pia
 
Kila siku huwa nasema jpm hakuonea mtu bali serikalini yamejaa majuzi na ndo fedha zao zilichukuliwa sababu zilipatikana kwa wizi.nashangaa baada ya mama hela za wizi akawarudisha.hata hivyo inaonekana hata mama anawaogopa kuwashughulikia.kwa kweli nawapongeza sana vijana wa gen z wa Kenya kwa hatua walizochukua na sisi pia tunatakiwa kufanya hivyo shida vijana wa Tz hawana ujasiri.
 
TRA pamoja na kuwa na kutengo cha internal investigation bado tu wanapiga kwa kwenda mbele.

Hapo hakuna mfanyakazi maskini labda utake mwenyewe.

Kila mtu kwenye idara yake ni kututandika tu.
Ukishakuwa staff wa TRA ukawa na vijana wako unakufaje maskini?🀣

Maana hao wazee wenyewe walianzia kwenye unyoka wakatajirika na wao wamefikia level za kuwa na vijana wao. Ni system ya kumegewa mafungu tu. Kampuni ziko zaidi ya buku na zile kubwa zenye hela ndio vinara wa hongo.

Ukienda Kigamboni ukaona mijengo walioshusha maofisa wa TRA ni kufuru. Halafu mtu anakwambia huwezi tajirika ukiwa afisa wa serikalini maana ajira ni utumwa.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Nashangaa takukuru wanafanya nini? Raisi awakumbushe majukumu yao akikaa kimya inaleta ukakasi ukiangalia wanavyokomaa na walipa kodi wadogo na kuua mitaji yao huku wao wakilijimbikizia mali inaleta hasira
System ya nchi iko corrupt inahitajika re shuffle ya nguvu na Kwa system ya katiba yetu anahitajika raisi mnoko na mfuatiliaji kama Magufuli unless otherwise katiba ibadilike na tu copy katiba ngumu kama ya China. Wale hawaruhusiwi kufanya ucenge nchini kwao ila wakachote hela sehemu nyingine WAPELEKWE kwao na wanapewa full support na SERIKAli yao.
 
Hao watoto wa kichaga humo ndio kwao, hapo wazazi wame lobby kinoma na ku temper na mifumo Ili vijana wao waingie kwenye line ya hela.🀣 Hamna mchaga fala aisee.
 
Kuna mtu mmoja mpuuzi nilisoma bandiko lake Jana anadai eti, "Unaandamana mwisho uumie Kwa faida ya nani?"

Nilishangaa sana nikaona hapa mabadiliko itakuwa kitendawili.

Mimi nilifanya mageuzi kwenye chuo nilichokuwa nasoma ilinigharimu ila kizazi nilichoacha kilifurahia mabadiliko ya ghafla. Imagine chuo kikuu hakina facilities za kutosha mnahama na viti kwenye venues. Wifi Hamna mnahangaika na ma bundles na system ya usajili hakuna mnapanga foleni siku nzima mnasota kwenye mabenchi.

Yote haya yalifanyiwa changes kabla hata sijamaliza third year ila ni matatizo ambayo yalikuwepo toka naanza certificate management ikawa inaona sawa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…