Mfanyakazi wa TRA akutwa amehifadhi pesa taslimu Tsh. Bilioni 7 nyumbani

Huyu jamaa alizitunzia ndani sehemu gani hela nyingi ivo?
Hivi billion saba unadhani zinaweza kujaza container hata ya 20FT? Hizo hela mbona ni za kupanga kabatini tu zinakaa fresh tu ikiwa sio za madafu. Kama ni $2m
 
Utakuta wazazi wako kule kijijini wanachangishwa daily michango ya kijenga zahanati, Endelea na ufala
Aisee Ili la michango vijijini ni hatari kila mara ni michango na kwenda kwenye maendeleo yaan vijijini ni shida , michango ya zahanati, nyumba ya mganga, nyumba ya mtendaji, mchango mradi wa maji, madarasa shule shikizi, yaani wanavizia watu hadi usiku saa Tisa kisa michango .

Ili nalo mkalitazame
 
May be no one is clean !! Someone out-there....saying Join us and follow suit or keep complaining !!!
 
Atakapo kuja Dikiteta Mzalendo Muadilifu hapo tutachanja mbuga bila wasiwasi ! 😳

Magufuli alionyesha kwa vitendo kwamba panapo nia njia ipo 🙄🙌
 
Ukiskia watu wanaenda 10,000 kugombea nafasi 5 TRA uwe unaelewa. Sababu za MSINGI zipo za kurundikana UDOM. Ukifanikiwa kuingia kule ndani ya miaka 10 tu unakuwa umefuta umaskini wa vizazi vyako 5 hadi sita mbele.
 
Sahivi uchawa unalipa kuliko kushughulikia matatizo ya nchi
Basi kama huo uchawa unalipa ni bora uchawa ufanywe kuwa tasnia kabisa na mtaala uandaliwe ili degree ya uchawa iwepo na pia iwe ajira rasmi.

Kwasababu vijana wanapelekwa na wazazi wao kwenda kusomea mambo ambayo yatawalipa huko mbeleni kwenye maisha yao.

Waambie kabisa, maths and science havilipi. Wakasomee uchawa na waendelee kupiga wakipata nafasi kama unavyowashauri.
 
Hata mimi ningekua ni yeye lazima ningeiba hata mnaompinga mgekua ni nyinyi mgeiba tu
Hakuna mtu ambaye angepata chance ya kupiga hela halafu akomae na ukristo au uislamu safi 😂! Wewe wenzio wanapiga wanajenga mahekalu ndani ya miezi 6 tu wewe ni nani ukomae na uzalendo huku umepanga upande wa nyumba Mbagala.
 
Sheria zinatungwa na majangili unategemea nini? ukipata nafasi mkuu wewe iba haswa tafuta mawakili wasomi hata 6 walipe nzuri na uwekaribu na majaji watatu
Huwezi kufungwa, hii nchi mafisadi wanakula na watu potential ndio maana jela hawawezi kwenda. Mtu anapiga malundo anapeleka mgao white house utamfungaje huyo.
 
Huko Goba watoto wa kichaga ndio wamejazana huko. Ukifuatilia Kwa maskini lazma ukute ni Kimario huyo 🤣 na aliingia Kwa line ya shangazi yake TRA
 
Tatizo kila anayewekwa anawaza kuchumia tumboni tu wazalendo wa kweli wamepungua sana kwenye hili taifa
Kwani si tulilalamika tunataka maendeleo ya watu sio vitu sababu tunaishi mara moja😂 kipindi JPM yupo madarakani. Mzee alilenga vizazi vijavyo sisi Kwa ubinafsi tukampinga maana hivyo vitu tutakufa bila kunufaika navyo.

Tuendelee kufurahia maendeleo ya watu sasa Kwa namna hio. Watu wakusanye Kodi WENGINE wajenge mahekalu na sio Barabara Wala hospitali.
 
Kama tunahitaji mabadiliko. Basi mabadiliko ya kweli yanaanza kwa mimi na wewe tuanze kuwafundisha watoto wetu kuanzia ngazi ya familia namna ya kulinda rasilimali. Muda bado upo tusikate tamaa
Uanze kumfundisha mtoto gani kulinda rasilimali wakati anaona unavyobadilisha mipira hapo uwani kwako. Leo Range kesho Discovery keshokutwa Benz. Mtoto gani atakuelewa umwambie uzalendo ni kushika bomba kwenye Eicher
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…