Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jielimishe noti za 10,000 zikiwa 7m ni zaidi ya 7bn.Wana masihara hao waandishi, yaani unamaanisha ameweka nyumbani MILIONI ELFU SABA
7,000,0000,000/-
Yaani noti za elfu kumi MILIONI SABA
Ukute hata Rusumo hujawahi kufika, ila upo na ngonjera tuu, na safari hii huko DR atalitema Bungo tuu.anayeweiza tz ni PK.
Hivi billion saba unadhani zinaweza kujaza container hata ya 20FT? Hizo hela mbona ni za kupanga kabatini tu zinakaa fresh tu ikiwa sio za madafu. Kama ni $2mHuyu jamaa alizitunzia ndani sehemu gani hela nyingi ivo?
Aisee Ili la michango vijijini ni hatari kila mara ni michango na kwenda kwenye maendeleo yaan vijijini ni shida , michango ya zahanati, nyumba ya mganga, nyumba ya mtendaji, mchango mradi wa maji, madarasa shule shikizi, yaani wanavizia watu hadi usiku saa Tisa kisa michango .Utakuta wazazi wako kule kijijini wanachangishwa daily michango ya kijenga zahanati, Endelea na ufala
May be no one is clean !! Someone out-there....saying Join us and follow suit or keep complaining !!!TRA kuna maajabu sana yaani vijana wa 2000 wamemaliza vyuo sababu ni wachaga wamepata kazi TRA wana ukwasi na magorofa ya hatari.
Yupo.kijana mmoja mtoto wa Shao( maarufu kama mtoto wa mama teddy) pale mbezibeach rainbow kamaliza ifm miaka ya 2018. Nilimkuta kwa mkuu wa wilaya anafuatilia kibali cha kumiliki bastola kisa yupoTRA ana pesa nyingi eti atakabwa.
Yupo mwingine Ngajiro alikiwa longroom lakini walimfukuza kwa ufisadi. Kuna akina Kimaro na wale wa airport Tra wana ukwasi wa hatari.
Sijui takukuru wamelala wapi. Na ile Fass sijui ya TRA law enforcement department inafanya kazi gani.
Atakapo kuja Dikiteta Mzalendo Muadilifu hapo tutachanja mbuga bila wasiwasi ! 😳Kinachofurahisha watanzania kuamini kwao ipo siku watu wenye nafasi za kufanya ubadharifu watabadalika na kuwa wema tu wenye maadili kwa maslahi ya taifa.
Hakuna kazi ngumu duniani kama ya kuwabadili watu tabia (tafuta kitabu chochote cha ‘change management), wenzetu wazungu washaelewa changamoto hizo ndio maana wakaja na science ya kubadili tabia na taratibu za kufanya hiyo shughuli.
As far as change management process is concerned ata huyo Magufuli alikuwa soft kwa standards za wazungu, shida ni kwamba alianza mabadaliko ambayo watanzania hawajazoea na support ya watu wachache.
Lazima atokee Magufuli mwingine ili nchi ibadilike tabia na hiyo ni nusu kazi; maendeleo pia ni culture ambayo lazima iwe imposed by force na jamii kuwa adoptive to changes, msingi wa mabadiliko uwe sheria mpya, technology, ushindani wa kibiashara, regional integration, societal attitude or whatever.
Nchi inahitaji mtu wa kubadili watanzania tabia or else miaka 50 ijayo itabaki kuwa miongoni ya nchi maskini bado.
Dunia inataratibu zake za kufanya mambo kwenye kila, na mambo hayafanyiki kama tunavyodhani kwenye vichwa tu; kuna science logic behind decisions.
Ni nchi yetu pekee ambapo Public Servant anaruhusiwa kumiliki na kuendesha Club ya soka wakati mshahara wake unajulikana.Wazir mwenyewe ana timu ya Mpira. Na anatumia takribani 100m to the minimum kila mwezi kuendesha timu. Je, anapata wapi pesa zote hizo?
Ukiskia watu wanaenda 10,000 kugombea nafasi 5 TRA uwe unaelewa. Sababu za MSINGI zipo za kurundikana UDOM. Ukifanikiwa kuingia kule ndani ya miaka 10 tu unakuwa umefuta umaskini wa vizazi vyako 5 hadi sita mbele.Kuna shangaz yang ni mwalim wa primary mara huko, alikuja dar akanambia nimsimdikize kwa mwanafunz wake aliemfundishaga shule ya msingi, asee kaolewa na kijana mmoja anafanya kaz TRA, aisee lile jumba sijawah kuliona tangu nizaliwe lipo kinyerez ni kufuru.. kuna had gym yenye vifaa vyote.. wakat tunaondoka tukapewa vibunda na hela ya mafuta..nilitaman namm nipate kazi TRA
Basi kama huo uchawa unalipa ni bora uchawa ufanywe kuwa tasnia kabisa na mtaala uandaliwe ili degree ya uchawa iwepo na pia iwe ajira rasmi.Sahivi uchawa unalipa kuliko kushughulikia matatizo ya nchi
Hakuna mtu ambaye angepata chance ya kupiga hela halafu akomae na ukristo au uislamu safi 😂! Wewe wenzio wanapiga wanajenga mahekalu ndani ya miezi 6 tu wewe ni nani ukomae na uzalendo huku umepanga upande wa nyumba Mbagala.Hata mimi ningekua ni yeye lazima ningeiba hata mnaompinga mgekua ni nyinyi mgeiba tu
Sasa kama hakuna wa kuwafunga breki wafanyejeSahivi watu wanaiba kupita kiasi
Huwezi kufungwa, hii nchi mafisadi wanakula na watu potential ndio maana jela hawawezi kwenda. Mtu anapiga malundo anapeleka mgao white house utamfungaje huyo.Sheria zinatungwa na majangili unategemea nini? ukipata nafasi mkuu wewe iba haswa tafuta mawakili wasomi hata 6 walipe nzuri na uwekaribu na majaji watatu
Hahahahaha lazma afungue pochi maana game ilikuwa serious.People made money wakati wa Magu. Unakuta tajiri kapigwa mkwara wa uhujumu uchumi, anafanya nini? People made serious money. Tena untraceable
Huko Goba watoto wa kichaga ndio wamejazana huko. Ukifuatilia Kwa maskini lazma ukute ni Kimario huyo 🤣 na aliingia Kwa line ya shangazi yake TRATRA wadada wale na vibwana mdogo vinajenga apartment GOBA kule ma'mae zimetapakaa tu mpaka Salasala Madale huko wanaporomosha Mahekalu tu
Kuna apartment 1 nilionyeshwa IPO GOBA haijaishaisha Ila unaambiwa haikusimama mpaka inafika juu ni apartment ya Ghorofa alafu naambiwa mwenye hio apartment ni kabinti tu kana miaka 21 ukikaona huwezi kukazania km ndio kamiliki ka hio apartment TRA noma
Kwani si tulilalamika tunataka maendeleo ya watu sio vitu sababu tunaishi mara moja😂 kipindi JPM yupo madarakani. Mzee alilenga vizazi vijavyo sisi Kwa ubinafsi tukampinga maana hivyo vitu tutakufa bila kunufaika navyo.Tatizo kila anayewekwa anawaza kuchumia tumboni tu wazalendo wa kweli wamepungua sana kwenye hili taifa
Uanze kumfundisha mtoto gani kulinda rasilimali wakati anaona unavyobadilisha mipira hapo uwani kwako. Leo Range kesho Discovery keshokutwa Benz. Mtoto gani atakuelewa umwambie uzalendo ni kushika bomba kwenye EicherKama tunahitaji mabadiliko. Basi mabadiliko ya kweli yanaanza kwa mimi na wewe tuanze kuwafundisha watoto wetu kuanzia ngazi ya familia namna ya kulinda rasilimali. Muda bado upo tusikate tamaa