Mfanyakazi wa TRA akutwa amehifadhi pesa taslimu Tsh. Bilioni 7 nyumbani

Mimi sijazungumzia kupambana ila nilichomaindi ni kukatisha tamaa mtu ambaye ameamua kupambana. Mimi siko kwenye position ambayo naweza kuleta impact ndio maana siwezi jihusisha na harakati kwa sasa.
Hamna mtu ataekatishwa tamaa na vimaneno vya mtandaoni mtu aliyeserious ataingia barabarani tu lasivyo ni muoga
 
Hizi nyepesi zenyewe zinafatwa? Yaani wezi wajitungie sheria kali dhidi yao?.
Nani alitunga sheria ya kinga dhidi ya viongozi? Na juzi juzi kuna mtu aliongeza list ya viongozi wasioshtakiwa kwa jinai wanazofanya.
😳 labda akitokea Dikiteta Mzalendo Muadilifu !
Atazibadili tu sheria !
Maana Sheria sio Msahafu ! Zinabadilishwa tu πŸ™ŒπŸ‘
 
Swali la kwanza kwanini akae na pesa nyingi kiasi hicho ndani? Nini kinanfanya asiziweke benki? Haofii usalama wake kukaa na kiasi chote hicho cha pesa ndani???

Jibu linaloniijia kichwani ni dhairi hizo pesa hajazipata kwa njia halali na ndio maana amezihifadhi kienyeji hivyo..... na kama hajazipata kihalali, kazipataje na ni mtumishi? Na je ana biashara gani yoyote ya kumuingizia pesa nyingi hivyo?

Jibu linaloniijia kichwani ni hapana, mfanya biashara hawezi kuhifadhi hela nyingi kipuuzi hivyo.

So ni wazi kwamba huyo ni FISADI na hizo pesa amezipata kwa njia za kifisadi akitumia madaraka au nafasi ya utumishi aliyonayo.

Swali lingine, sasa kama hana cha kuzifanyia hizo pesa na amezihifadhi tu ndani aliziiba za nini??? Je ni kweli hakuna jambo la maana ambalo anaweza kuzifanyia hizo pesa zikawanufaisha na wengine?

Jibu linaloniijia kichwani ni kwamba huyu ni mbinafsi.... kama ni mambo ya maana yenye tija kwa jamii akiamua kuyafanya kupitia hizo pesa yapo mengi sana.

Kuliko kuzihifadhi hizo pesa ndani alikuwa anaweza kutafuta walau hata wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini wa fani mbali mbali ambao hawana ajira na kisha kwa makundi wakaleta ideas zinahusu ujuzi walionao na kisha yeye akazifadhili ideas hizo kwa makubaliano maalumu..... ukienda pale SUA kila mwaka wanazalisha maengineer wa kilimo halafu maengineer hao hawana pakwenda, sasa huyu mficha vibunda wa TRA anaweza kuwakusanya hao wahitimu angalau hata 200 wenye ujuzi wa hali ya juu kabisa kwenye sekta ya kilimo.

Akitenga angalau hata 1B kisha akawafund hao vijana 200 kwenye kwenye project hata ya zao la karanga, wakaifanya kisasa na kwa umakini wa hali ya juu kabisa projec hiyo.... naamini kabisa italeta mabadiliko chanya makubwa sana, kwani baada ya miaka 3 kupitia hiyo project hao vijana wanaweza kuwa wamezalisha ajira zingine 1000 na kupanua wigo wa wanufaika.

Kwa kufanya hivyo huyo kigogo wa TRA angekuwa ameisaidia jamii pakubwa sana, kwanza kwa kuingiza hela kwenye mzunguko, pili kupunguza makali ya tatizo la ajira na njaa hapa nchini ....... na kubwa zaidi hata Mungu nae angemsamehe kwa wizi alioufanya maana angekuwa amezurudisha pesa hizo kwa wananchi katika namna ambayo ni nzuri zaidi baada ya kuzikwapua kwenye mikono ya serikali.

Ila ni bahati mbaya sana kwenye taifa hili mafisadi waliopo ni wabinafsi na wenye roho mbaya sana.
 
Akili huna hela azitafute Kwa ujanja wake aje awape nyie mkalimie karanga we boya kwel unaitamka tu billion 1 kirahisi kama unayo
 
Kulalamika pekee hakutoshi. Mbona watanzania tunapenda sana kulalamika bila vitendo. Tuchague moka, tukae kimya au na sisi tuandamane kama huko Kenya.
 
Pita naye bhana nawe upate ka baby walker hapo town πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…