Mfanyakazi wa Vodacom aeleza alivyochunguza Simu za Sabaya

Mfanyakazi wa Vodacom aeleza alivyochunguza Simu za Sabaya

Nimesoma comments zote kwenye uzi huu nimejiifunza kwamba Tanzania tuna raia wengi mbumbumbu sana!

Suala la kutoa taarifa za mteja wa benki au mtandao wa simu kwa masuala ya usalama ni matakwa ya lazima kwa mujibu wa sheria. Na wala mtoa huduma haitaji consent yako taarifa zako hizo zinapohitajika na taasisi za usalama kwani unakuwa tayari ulisharidhia kwenye customer relationship agreement!

Sasa mmekazana mara huyo kipenyo! mara Voda masinichi kumbe nyie ndo weupe vichwani! Halafu wengi wenu ndo akina Mbowe wanawatumia kudai katiba mpya wakati hata sheria basic za Nchi hamjui! Hovyo kabisa ! Vijana wa Tanzania tafuteni maarifa mmekalia sana urongo urongo tu!
 
Me sio muumin wa matendo ya sabaya ila vodacom ni masnitch sanaaaa
Issue sio Vodacom
Issue ni Sheria yetu iliyopitishwa bungeni inamtaka mtoa huduma kutoa ushirikiano

Tusilaumu tu ina faida zake
Mfano yule dada aliyechomwa na gunia la mkaa muuaji wake alipatikana kwa mbinu hii

Moral of the story:
Mawasiliano yetu sio siri.,hivyo tuwasiliane tukijua yanaweza hitajika sehemu na yakatolewa

Bottom line
Tutii sheria bila shuruti na
Tuwe Raia wema
 
Nimesoma comments zote kwenye uzi huu nimenifunza kwamba Tanzania tuna raia wengi mbumbumbu sana!
Suala la kutoa taarifa za mteja wa benki au mtandao wa simu kwa masuala ya usalama ni matakwa ya lazima kwa mujibu wa sheria. Na wala mtoa huduma haitaji consent yako taarifa zako hizo zinapohitajika na taasisi za usalama kwani unakuwa tayari ulisharidhia kwenye customer relationship agreement!
Sasa mmekazana mara huyo kipenyo! mara Voda masinichi kumbe nyie ndo weupe vichwani!
Halafu wengi wenu ndo akina Mbowe wanawatumia kudai katiba mpya wakati hata sheria basic za Nchi hamjui! Hovyo kabisa ! Vijana wa Tanzania tafuteni maarifa mmekalia sana urongo urongo tu!
Thank you
Na watu hawajui kuwa ignorance of the law is not an excuse
Utahukumiwa hata kama hio sheria huijui
 
Mara nyingi ushahidi wa simu hautumiki katika maamuzi hata kama umekubaliwa.Kwani ni lazima simu ikisoma mnara wa mtaa fulani basi na mimi nitakuwepo hapo?Uthibitisho wa sauti ni mgumu kwani kuna watu wana vipaji kuiga sauti za watu...mwishoni unakuwa ushahidi wenye shaka
Watasema ni wewe kwani laini ni yako
Kama utajitetea sio wewe
Hakikisha una ushahidi wa loss report ya laini hiyo
Vinginevyo umekwisha
 
Mpaka leo ulikuwa hujui tu? Tatizo ni nani wa kumfunga paka kengere.
 
Ngoja tukufahamishe kidogo ili uache mambo ya kukalili

Unapozungumzoa Sera za faragha za mteja (customer privacy) sio kwa service provider company pekeee, hio ni kwa kila kampuni lazima iwe na Sera ya faragha za wateja wake ingawa zinatofautiana kutokana na huduma inayotolewa na kampuni husika...
Acheni kukalili 3+2=5 nikitu kilekile ukisema 2+3=5. Utofauti wake ni kwamba kwenye swali no 1 tumeanza na 3 lakini kwenye swali la pili tumeanza na 2.
We unampeleka mbali mkuu, apple pia ni service provider wana huduma kama iMessage, apple pay, wana huduma kama FaceTime haina tofauti na Skype ya kuwasiliana kwa njia ya video utasema hawa sio service provider kweli? Hapo kinachomchanganya jamaa ni lugha ya kiingereza lakini apple ni watoa huduma kama kampuni nyingine tu na wanahifadhi data za watumiaji wao kwa umakini mkubwa..
 
MENEJA Ulinzi na Ushirika wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Kampuni ya Vodacom (T) Makao Makuu Dar es Salaam, James Wawenje (39), ameieleza mahakama jijini hapa kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa Arusha ilimuagiza achunguze namba za simu ya kiganjani za washitakiwa watatu akiwemo alyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya.

Wawenje ni shahidi wa sita katika kesi ya uhujumu uchumi, kuongoza genge la uhalifu na kutakatisha fedha inayomkabili Sabaya (34) na wenzake sita katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha.

Washitakiwa wengine ni Enock Mnkeni (41), Watson Mwahomange (27) maarufu Malingumu, John Aweyo (45), Sylvester Nyengu (26) maarufu Kicheche ambaye ni msaidizi wa Sabaya, Jackson Macha (29) na Nathan Msuya (31).

Akiongozwa na Mwendesha Mashitaka Mwandamizi wa Serikali, Ofmen Mtenga mbele ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Patricia Kisinda, Wawenje alidai namba za simu alizokabidhiwa ni za Sabaya, Mnkeni na Macha ambazo Takukuru ilitaka taarifa zake za Julai 20, mwaka huu za kupiga, kupigiwa simu na jumbe mfupi.

Wawenje alizitaja namba hizo alizokabidhiwa na Takukuru kuwa ni namba 0758 707171 iliyosajiliwa kwa jina la Lengai Ole Sabaya, 0757 978686 iliyosajiliwa kwa jina la Enock Mnkeni na namba 0746 935569 iliyosajiliwa kwa jina la Ramweli Jackson Macha.

Alisoma nyaraka za mtandao za Vodacom zikionesha watuhumiwa Sabaya, Mnkeni na Chacha walivyokuwa katika Jiji la Arusha maeneo ya Mbauda, Sombeni, FFU Kwa Mrombo na Makao Mapya kati ya saa 8.44 mchana, saa 9.52 na saa 9.55 alasiri.

Wawenje alidai alitoa taarifa zake kwa Kamanda wa Takukuru Mkoa Arusha kama alivyotakiwa ikiwa ni pamoja na taarifa za kupiga, kupokea na ujumbe mfupi wa sms kwa tarehe iliyotajwa kwa mujibu wa sheria ya nchi.

Alidai kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka ya kutoa taarifa za mteja kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini pindi vitakavyohitajika.

Alisema tangu Agosti 25, 2014 amekuwa akifanya hivyo kwa ushirikiano mkubwa kwa kuzingatia sheria ya nchi na kwa kuzingatia misingi ya sheria ya usalama kwa kuwa ndio mtunza kumbukumbu zote za Vodacom (T) za kupiga, kupokea na ujumbe mfupi wa sms kutoka kwa wateja wote wa mtandao huo.

Alidai kumbukumbu za kupiga, kupokea na jumbe za sms za wateja wa Vodacom hukaa zaidi ya miaka 10 kwa mujibu wa sheria.

Alikabidhi mahakamani nyaraka ya barua kutoka Takukuru kwenda Vodacom kama ushahidi katika kesi hiyo na upande wa utetezi haukuwa na pingamizi kuhusu nyaraka hiyo.

Nyaraka zingine ambazo zilipaswa kuwasilishwa mahakamani hapo kama kielelezo cha ushahidi wa Jamhuri ni taarifa ya mteja ya kupiga, kupokea na ujumbe mfupi wa sms za Sabaya, Mnkeni na Macha.

Wakili wa utetezi wa washitakiwa wa tano, sita na saba, Edmund Ngemela alipinga na kudai kuwa sheria inapingana kupokelewa vielelezo hivyo.

Mahakama ilikataa pingamizi hilo hivyo vilipokelewa kama ushahidi.

Chanzo: Habari leo
Hachomoki .mshamba yule funga 100
 
Ila kwa Mbowe ndio kuna privacy?

[emoji23][emoji23][emoji23]Huwa nacheka sana bavicha mnapojikaanga kwa mfuta yenu wenyewe
Unamfanisha Mbowe na Jambazi Sabaya hahaha, Mbowe dunia yote inajua ni innocent ni hila za kisiasa tu, na Mungu atonyesha njia
 
Back
Top Bottom