Mficha uchi hazai....

Mficha uchi hazai....

1gb

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2013
Posts
2,199
Reaction score
2,859
Habari wana Jf
Mimi ni kijana wa kiume mwenye umri kati ya 21-26.Tatzo nilonalo ni kwamba huku sirini nimepatwa na viupele vidogovidgo vinavyotoa majimaji lkn hayana harufu kali.majimaji yanayotoka ni kama vile ya mgonjwa alieungua na moto,sasa yale majimaji yanayotoka katika jeraha la moto yana fanana hivyhivyo na haya yanayotoka kwenye vipele hivi kwenye dushe yangu.vipele hivi vimekaa takribani wiki 2 na nusu na havionyeshi dalili ya kupona/kukauka na ukizngatia na hali ya hewa ya mji nnaoishi ni ya joto.mdawoote sikutumia dawa yeyote nikiamini vitakauka tuu nilichokuwa nafanya ni kuvisafsha vyema na sabuni na kufunga vyema na kitambaa safi na kutoka kwa ajili ya mishemishe.Nilivyoona hali ni ileile nikaenda famasi nikamweleza famasia nikapewa hii dawa CALAMINE ANTIPRURITIC.Lkn naona majimaji hayaishi,nikanunua baby powder nikawa nikioga najipiga mapowder kibao kwenye dushe,lkn itakaa kwa muda kama nusu saa ikiisha poda vimajimaji kamakawa.
CHANZO CHA VIPELE
Mwanzo nilikuwa natumia mafuta mazito kupaka mwili wangu,baadae nikabadilisha na kuanza kutumia lotion iitwayo NIVEA nourishing milk.Ndipo hapo tatzo la vipele lilipoanza,vipele vianza mikonino katikati ya vidole na juu ya vidole,nikawa navitumbua,baadae vikahamia mapajani mpaka sasa kwenye dushe ndpo nilpoiacha hiyo lotion.
Labda unaweza ukasema nimeambkizwa na m/mke w/wake kwa hili ntakataa 99.9% kwa sabb kabla ya kupatwa na hili tatzo ckuwahi kudu kwa zaid ya wk 4,kutokana na u busy na kazi ngumu nnazofanya,nikirudi geto nikulala tuu.Mpka nilipopata tatzo wk 2na zaidi sijaduu pia.
MSAADA KWA WANAOFAHM TIBA/WALIWAHI KUPATWA NA TATZO KAMA HILI WAKAPONA KWA DAWA ZIPI/IPI?
kweli mficha uchi hazai nimeona bora nijisalimishe,isije ikaoza yoote ikakatwa.Loooh salaaale maana dushe ndo kila kitu kwa m/ume.
 
Ushauri wangu wa haraka ni uende hospitali...onana na madaktari wa tiba ya ngozi
 
Hayo ni magonjwa ya zinaa, wahi kwa daktari, kuna magonjwa ya zinaa ambayo yanaweza kujitokeza baada ya wiki 3 mpk 6 baada ya kujamiana hii inategemea mtu na mtu, pia ni muhimu kwenda na mwenzio..

Kama hujaoa kumbuka condomu ni muhimu na kama umeoa ni wakati wa kuongea na mke ni wapi amepata magonjwa ya zinaa na kwanini anajamiana bila condomu. (kama si wewe uliyemwambukiza)
 
Herpes Zoster/shingles- ndio ugonjwa ulianao wahi haraka hospital ukafanyiwe matibabu mdogo wangu
Ukanda%20wa%20jeshi%20picha.jpg
 
Ahsanteni kwa mawazo yenu wadau wa jf.Na hata wale waliofunua uzi na kuondoka bila kutia neno,shkran ziwafkie nyoote.Na hii ndo maana halisi ya forum,kusaidiana kwa kila hali.
 
Herpes Zoster/shingles- ndio ugonjwa ulianao wahi haraka hospital ukafanyiwe matibabu mdogo wangu
Ukanda%20wa%20jeshi%20picha.jpg
Sawa nimekupata kaka.
Swali(kwa faida yangu na wengne );Herpes Zoster ugonjwa huu hukimbilia sirini tuu au ni ugonjwa unao deal na ngozi, sehemu yeyote ile ya mwili wa mwanadamu?
 
Mkuu 1gb ninakupa kwanza First aid lakini fuata ushauri kama wa wenzangu nenda haraka Hospitali acha

kutumia hizo dawa. Fanya hivi: dawa za Vipele u
chukue kitunguu Saumu

Ukitwange mpaka kiwe laini kisha uchukuwe maji ya moto uoshe sehemu zenye vipele ufanye kama

unasugua .

kwa uwezo wa Allah utapona.

Au pia waweza
kitunguu Saumu.Menya chote kama vile uandaavyo kwa ajili ya kupikia.Twanga ama

saga,vikishasagika changanya na maji ya uvuguvugu kidogo kipimo cha kijiko cha chai ili vilainike.Chota

msagiko wote wa vitunguu na uvimeze.


Tahadhari,jitahidi uwe na mfuko ama sehemu ya maliwatoni maana kama hauna tumbo zuri unaweza tapika.

(Mara chache sana hutokea kutapika)
Ukishakaa kama dk 15 hali yako itarudi kawaida. Pia kama una presha

ya kushuka usitumie hii dawa maana huwa inashusha sana presha,labda unywe na kahawa baada ya kuinywa

dawa hii ili kuipandisha tena presha! Tumia kisha uje unipe feedback.


 
Heshima kwako MziziMkavu nilijua sitakosa chochote kutoka kwako Allah akuzidishie na mawazo yako utoe bure.Ntayafanyia kazi mawazo ulonipatia.
 
Last edited by a moderator:
Pole kaka,,...usijali utapona tu,,...na usisite kwenda kumuona daktar
 
Sawa nimekupata kaka.
Swali(kwa faida yangu na wengne );Herpes Zoster ugonjwa huu hukimbilia sirini tuu au ni ugonjwa unao deal na ngozi, sehemu yeyote ile ya mwili wa mwanadamu?
siyo sirini tuu hata sehemu nyingine ya mwili nasiyo ugonjwa wa zinaa, ni tatizo la kiafya ukiwa na afya nzuri hauwezi kutokea, pia kuwahi matibabu ni vyema zaidi hivyo bora uwahi pistali chali yangu.
 
dogo two weeks hujaenda hospital?hebu wahi hospital usije ukapata madhara makubwa zaidi
 
Hivi vitunguu saumu vya MziziMkavu vinatibu kila ugonjwa?
Mkuu Truth Matters


JUISI YA KITUNGUU: HUPONYA MARADHI YALIYOSHINDIKANA HOSPITALI!


attachment.php





Katika makala ya leo nawaeleza faida za juisi ya kitunguu maji katika mwili wako, ikiwemo uwezo wake wa kuzuia na kutibu magonjwa sugu na yaliyoshindikana kwa kutumia dawa za hospitali.

Tunapaswa kutambua kwamba viungo vingi tunavyotumia jikoni kwenye vyakula vyetu kila siku vina uwezo mkubwa wa kuponya magonjwa yanayotusumbua. Sina shaka kama kuna mtu ambaye hakijui kitunguu, nyanya, au kitunguu saumu.

Kitunguu maji ni kiungo cha mboga, ambacho aghalabu hutumika katika mapishi ili kuongeza ladha katika chakula na wakati mwingine hutumika kutengenezea kachumbari. Baadhi ya watu hawapendi kula kachumbari kwa kutokujua umuhimu wake mwilini.

KITUNGUU KINATIBU YAFUATAYO
Katika orodha ndefu ya magonjwa yanayotibika PASIPO SHAKA kwa kutumia juisi ya kitunguu, ni pamoja na ugonjwa unaowasumbua watu wengi wa kutokwa na damu sehemu ya haja kubwa wakati wa kujisadidia.

Ugonjwa huu, ambao kwa kitaalamu unajulikana kama
‘hemorrhoids’ au ‘Piles’, unawatokea watu wengi ambao kama mtu hukupata nafuu kwa kula vidonge, suluhisho la mwisho huwa ni kufanyiwa upasuaji mdogo katika njia ya haja kubwa, upasuaji ambao huambatana na maumivu makali.

Kwa wale ambao wameshakutwa na tatizo hili au wanalo hadi sasa, dawa kama vile
ANUL SUPPOSITORIES,SECNIDAZOLE, n.k zinajulikana sana kwao, kwa sababu ndiyo dawa zinazopendekezwa na madaktari wengi kutumiwa ili kutibu PILES. Unaweza ukapona kwa muda na tatizo likajirudia baadaye au unaweza usipone na ukalazimika kufanyiwa upasuaji.

Lakini kwa kutumia juisi ya kitunguu, unaweza ukapona kabisa na inawezekana tatizo lisijirudie, kwani mzizi wa tatizo huondoka kabisa kutoka tumboni.

SIFA YA KITUNGUU SAUMU
Kitunguu kina virutubisho vyenye uwezo wa kuua
bakteria(Antibacterial) na fangasi mwilini. (Anti fungus). Pia kina virutubisho vyenye uwezo wa kuzuia wadudu wanaosababisha magonjwa nyemelezi (anti free radicals) na magonjwa ya uvimbe (anti informatory).

Mbali na sifa hizo, Kitunguu Saumu kina kiwango kikubwa cha madini kama vile
‘calcium’, ‘magnesium’, ‘sodium’, ‘potassium’, ‘selenium’, ‘phosphorus’ na bila kusahauu kiasi kidogo cha aina fulani ya mafuta ambayo huimarisha kinga ya mwili.
JINSI YA KUJITIBU ‘HEMORRHOIDS.’

Kama nilivyoanza kusema awali, pamoja na magonjwa mengine yanayotibika kwa kitunguu, leo tutaanza kwanza na ugonjwa huu unaosumbua watu wengi. Dawa hii ni ya uhakika kwa mtu atakayeweza kuitumia kama inavyotakiwa.

Kunywa juisi ya kitunguu kila siku asubuhi kwa muda wa siku saba hadi siku 14, ikitegemea na ukubwa wa tatizo lako. Juisi hiyo lazima uinywe asubuhi kabla ya kula kitu chochote
(on empty stomach) na utaruhusiwa kunywa kifungua kinywa chako saa moja baada ya kunywa juisi hiyo.

Dozi hii ni maalum kwa ajili ya kutibu ‘
hemorrhoids’, ingawa wakati ukitibu tatizo hilo, matatizo mengine yaliyomo mwilini yatakuwa yakijiondoa, kama tutakavyoona katika makala haya wiki ijayo. Napenda kukuhakikishia kuwa tiba hii ni ya uhakika na haina madhara yoyote.

TAHADHARI
Mara baada ya kuinywa juisi hii kwa mara ya kwanza na siku chache zitakazofuata, utajisikia vibaya na tumbo kuchafuka. Hali hii ni ya kawaida, unachotakiwa kufanya mara baada ya kunywa, ni kukaa au kulala kwa muda, baada ya muda hali yako itarejea kama kawaida. Baada ya siku tatu, ukinywa mwili utaizoea na utajisikia kawaida tu.

attachment.php


Kitunguu Maji chekundu ndio dawa kwa kila maradhi.

Wiki iliyopita tulianza

makala haya kwa kuangalia jinsi kitunguu kinavyoweza kutibu ugonjwa wa kutokwa damu wakati wa kutoa haja kubwa. Katika makala hayo, watu wengi wameonekana kuguswa nayo. Wiki hii, pamoja na mambo mengine, nitakujuza jinsi ya kuitengeneza juisi hiyo.


Halikadhalika katika makala ya leo, utajua magonjwa mengine yanayoweza kutibika kwa kitunguu, iwe kwa kunywa juisi yake au kwa kula kitunguu chenyewe. Kitu kimoja napenda kukuhakikishia kuwa, unayoyasoma hapa kuhusu kitunguu, tayari yalishafanyiwa utatifi na kuthibitishwa na wataalamu waliobobea katika masuala ya vyakula tangu enzi za mababu zetu.

Vile vile, watu wanaoamini lishe kama tiba na kutumia, matokeo yake siku zote huwa dhahiri na wako wengi wanaoweza kuthibitisha jinsi afya zao zilivyo imara leo tofauti na miaka kadhaa iliyopita kabla ya kugundua siri ya chakula kama tiba.

JINSI YA KUTENGENEZA
Kinachotakiwa ni kitunguu maji kimoja cha ukubwa wa wastani ambacho utatengenezea juisi na kupata kiasi cha glasi moja saizi ya kati. Safisha kitunguu chako kwa kuondoa gamba la juu kisha katakata vipande vidogo vidogo ili kurahisisha usagaji.

Kuna njia mbili unazoweza kuzitumia kutengeneza juisi hiyo. Ya kwanza ni ya kisasa ambapo unaweza kutumia ‘blender’ au ‘juicer’, kwa kuweka maji kidogo na kuanza kuisaga hadi kupata juisi. Njia ya pili ni ya kiasili, ambapo utatumia kinu kidogo na maji kidogo kwa kutwangwa hadi kupata juisi.

Ukimaliza kusaga (kwa njia utakayoitumia) kamua na ichuje juisi yako kwa kutumia chujio la kawaida ili kupata juisi pekee ya kitunguu na kuacha masalia ya maganda peke yake. Mara baada ya kuiweka juisi yako kwenye glasi,

HAKIKISHA UNAINYWA HAPO HAPO. Hairuhusiwi kuihifadhi au kuinywa baadaye, kwa sababu itapoteza virutubisho vyake muhimu.

Kunywa glasi moja mara moja kwa siku au mara mbili, ukiona tatizo lako ni kubwa. Fanya zoezi hilo la kundaa juisi na kuinywa kwa muda wa siku saba hadi 14.
Kama nilivyoeleza wiki jana, hali ya kuchafuka kwa tumbo na kujisikia vibaya baada ya kunywa, isikuogopeshe, baadaye utaizoea na utajisikia vizuri zaidi.

Mbali ya kutibu tatizo la kusikia maumivu na kutokwa na damu wakati wa kwenda haja kubwa (Hemorrhoids au piles), juisi hiyo pia itatoa ahueni au kinga kubwa dhidi ya matatizo mengine ya kiafya yafuatayo:
Pumu, mafua, magonjwa ya kuambukizwa na bakteria, matatizo ya kupumua kwa shida, kiungulia na kutapika.

Itaongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi, vile vile kwa kutafuna vitunguu vibichi na kukaanavyo mdomoni kwa sekunde kadhaa, kutaua bakteria wote wa kinywani na kutoa kinga dhidi ya kuoza kwa meno na kuondoa harufu mbaya.

Ulaji wa vitunguu maji vibichi mara kwa mara, hulainisha damu na kuzuia kuganda ambako husababisha mishipa kuziba na kusababisha magonjwa ya moyo, ikiwemo presha ya kupanda.

Juisi ya kitunguu ni dawa mara moja ya kuzuia kutapika, mtu anayetapika mfululizo akinywa juisi ya kitunguu, hupata nafuu haraka. Vile vile juisi hii ni dawa ya tumbo linalouma na hutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe tumboni.

Kama unasumbuliwa na chunusi, pakaa juisi ya kitunguu iliyochanganywa na asali sehemu yenye chunusi vitaondoka na kukuacha na ngozi nyororo. Chukua kiasi kidogo cha juisi na kijiko kimoja kidogo cha asali changanya kisha pakaa.

Juisi ya kitunguu pia ni dawa ya kutibu majeraha ya kuumwa na nyuki. Kama unapata maumivu wakati wa haja ndogo au unatoa mkojo mchafu sana, kunywa maji mengi yaliyochanganywa na juisi ya kitunguu kiasi kidogo, tatizo litakwisha.

Juisi ya kitunguu ina virutubisho vyenye uwezo wa kudhibiti chembechembe hai za mwili zenye kansa na hivyo kuwa kinga nzuri dhidi ya ugonjwa wa Saratani (cancer).

Ulaji wa vitunguu au juisi pia hutoa ahueni kwa mgonjwa wa kifua kikuu. Juisi iliyopashwa moto pia ni dawa ya sikio linalouma. Weka matone mawili tu kwa kila sikio linalouma.

Juisi ya kitunguu pia ni dawa ya majeraha yatokanayo na moto. Ukiungua, pakaa juisi hiyo sehemu zilozoungua kwa nafuu ya haraka. Pia kitunguu ni dawa ya mbu, pondaponda vitunguu, kisha jipakae sehemu za miguu na mikono - mbu hawatakugusa.

Faida za kitunguu na juisi yake ziko nyingi na zote ni muhimu kwa ustawi wa afya zetu. Nakushauri kuanzia leo, kunywa juisi hiyo au kula kitunguu katika kila mlo kwa jili ya kutibu maradhi uliyonayo au kwa kuupa mwili wako kinga imara, na kamwe hutajuta!


 

Attachments

  • Juisikitunguuu.jpg
    Juisikitunguuu.jpg
    32.7 KB · Views: 913
  • kitunguuu chekundu.jpg
    kitunguuu chekundu.jpg
    37.7 KB · Views: 892
Back
Top Bottom