Mfugale awavimbia Waziri Mkuu na Waziri wa Ujenzi kwa kivuli cha Rais Magufuli?

Siku kadhaa zilizopita, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo kwamba kutokana na meneja wa Tanroads wa Morogoro Godwin Andalwisye kufanya uzembe wa kutoyafanyia ukaguzi madaraja ya barabara ya Morogoro hadi Dodoma na kusababisha uvunjikaji wa daraja, basi aondolewe mara moja Morogoro na kurudishwa wizarani kupangiwa kazi nyingine. Wazirir Mkuu alikasirishwa na kitendo hicho kwa kuwa fedha za kufanyia ukaguzi zilikuwapo na alibainisha kwamba daraja hilo lingefanyiwa ukaguzi lisingevunjika.

Aliporudi Morogoro kuangalia maendeleo ya kazi, Waziri Mkuu ameshangaa kukuta meneja wa Tanroads Morogoro bado hajaondolewa. Alikerwa na hilo na kuuliza kwa nini meneja huyo bado hajaondolewa licha ya agizo lake. Kwa kujiamini kabisa, Mfugale alimjibu Waziri Mkuu kwamba "Andalwisye ni mmoja wa mainjinia wachache wenye utaalamu wa ujenzi wa madaraja, kwa hiyo huduma yake bado inahitajika hapa. Wewe ulitoa agizo na mimi ndio mtekelezaji, lakini bado tunahitaji utaalamu wake".

Ukweli ni kwamba si kweli kwamba Tanzania hatuna mainjinia wa kutosha wa ujenzi wa madaraja. Wapo wengi sana. Na tangu lini amri ya Waziri Mkuu inapingwa kwa sababu anaetuhumiwa anaonekana bado anahitajika? Watumishi wangapi wanaondolewa kwa amri toka juu licha ya utumishi wao kuhitajika?

Waziri Mkuu ni kiongozi anamuwakilisha Raisi kiutendaji. Je Raisi Magufuli anaweza kutoa amri na mteule wa chini akaikiuka kwa kuwa mtu aliyetumbuliwa bado anahitajika?

Katika hali ya kawaida Mfugale anatakiwa kuwajibishwa. Kufuata protokali, alitakiwa akamuombe Waziri Mkuu Majaliwa kwamba huyo Meneja wa Morogoro abaki kwa sasa - kitu tunaita "no surprise" katika mambo ya utawala. Kitendo alichofanya Mfugale ni kumdhalilisha Waziri Mkuu na Waziri wake wa Ujenzi.

Kwani kulikuwa na ubaya gani kwa Mfugale kuteua meneja mpya wa Tanroads Mororgoro na kumpeleka Andalwisye kwenye site kama mtaalamu tu kutoka Wizarani kama ni kweli anahitajika kiasi hicho? Kwani hilo daraja ni lazima lijengwe Andalwisye akiwa ndio meneja wa Tanroads Morogoro?

Sasa suala la kujiuliza ni kwamba Mfugale ametoa wapi ujasiri wa kumvimbia Waziri Mkuu na hata Waziri wake wa Ujenzi? Mengi sana yamesemwa kuhusu uhusiano wa Magufuli na Mfugale kuhusiana na miradi ya barabara wakati Magufuli ni waziri wa ujenzi. Watu hawakushangazwa na flyover ya Tazara kupewa jina la Mfugale.

Je, hilo ndilo linalomfanya Mfugale aone kwamba yuko "untouchable" na Waziri Mkuu Majaliwa na anaweza kumvimbia? Tangu lini amri ya Waziri Mkuu inakuwa "overruled" na mtu kama Mfugale ambaye kimadaraka yuko chini ya Waziri wa Ujenzi? Kumbuka amri hii ilitolewa na Majaliwa kwa Waziri wa Ujenzi, kwa hiyo kimsingi, Mfugale amemvimbia Waziri wake wa Ujenzi pamoja na Waziri Mkuu.

Source:
Majaliwa ahoji aliyemhamisha kuendelea na kazi
PM aghast to find manager he transferred still at work
wewe mchochezi
 
wewe mchochezi
Neno "mchochezi" ni a very subjective and relative term. Inategemea uko wapi na maslahi yako yako wapi.

Magufuli na watu wa CCM siku zote wataona wanachosema viongozi wa upinzani ni uchochezi
Kwa sasa raia wa Tanzania wakimkosoa Magufuli au serikali wanaonekana kuwa ni wachochezi
Ndugai na viongozi wa Bunge siku zote wataona wabunge wapinzani wakipinga hoja za seerikali BUngeni ni uchochezi
Ndugai aliona Prof Assad akiwa CAG kulikosoa Bunge ni uchochezi japo aliongea ukweli
Serikali ya Makaburu iliona kile Mandela na wenzake walichoongea kudai haki sawa Afrika Kusini ilikuwa uchochezi

Watu wasiofuata haki siku zote wana maana yao ya neno uchochezi kwa namna ya kulinda maslahi yao. Ni wazi sana hapa maslahi yako yako wapi.
 
Synthesizer,

Mi naona kuna tatizo kubwa zaidi kwanza kumekuwa na maagizo yanayotolewa kuwa ondoa mtu fulani pale au pale wakati huyo mtu kiutendaji haripoti kwa huyo anayeelekeza aomdolewe.

Utaratibu mtu kama utendaji wake una mapungufu yanaonekana na boss wake anayemsimamia sasa anapotokea kiongozi wa juu anaruka wasimamizi anakwenda kuondoa mtu ambaye siyo yeye anayemsimamia haieleweki ametumia utawalam gani kuona mapungufu ya mtu ambaye hasimamiwi na yeye na hivyo kuwajengea hofu watendaji wa chini bila sababu.

Kama Waziri Mkuu angekuwa yuko makini alitakiwa kumuondoa yule anayeripoti kwake moja kwa moja kuhusiana na hayo na kama hana mamlaka ya uteuzi wa huyo mtu angeweza kuelekeza mamlaka ya uteuzi lakini siyo kumwambia waziri ondoa yule pale kwani huyo Waziri hamuoni huyo mtu utendaji wake hadi asubiri kuelekezwa na Waziri Mkuu.

Hiwezekani kiongozi wa juu aniagize mimi nimfukuze msaidizi wangu wakati sioni mapungufu ya utendaji wake wa kazi na yeye bosi wangu hawezi kuona mapungufu ya msaidizi wangu yeye ataona mapungufu ya mimi na ana haki ya kuniwajinisha mimi kwa mapungufu anayoyaona na siyo kuniruka mimi na kuanza kuwajibisha mtu wa chini yangu Hiyo siyo sahihi.

Mimi kwa hili nasimama na Mfugale, nina imani litaondoa hofu kwa wafanyakazi wa Ngazi ya kati kufanywa kafara wa kila pungufu linapotokea wakati katika uhalisia hakuna mapungufu yoyote yanayokuwa yamenainishwa na viongozi wao isipokuwa kusema wanatekeleza maagizo kutoka juu kama vile kuna chuki tu binafsi kwa baadhi ya watendaji wa kati.
wamezidi na wao kuiga tabia za kipumbavu za naniii
 
Sidhani kama Majaliwa atasahau hili. Akija kuwa raisi kitu cha kwanza ni kubadilisha jina la flyover ya Tazara. Na usisahau kwamba Majaliwa alikuwa na moto sana mwanzoni, siku moja akazimwa hadharani na raisi na kuambiwa hata yeye anaweza kutumbuliwa kama wengine. Hiyo ilimnyamazisha sana Majaliwa.

Lakini tambua kwamba Magufuli anajua hilo. Sio rahisi Majaliwa kuja kuwa raisi katika mazingira kama hayo.
hivi mnadhani hii nchi ni uraisi ni vyeo vya kupokezana kindugu,yani tumetoka kutawaliwa na kikwete tena mnataka ndugu yake mama salma kikwete majaliwa nae awe raisi.hivi huwa mnawaza nini akilini mwenu nyie.
 
Neno "mchochezi" ni a very subjective and relative term. Inategemea uko wapi na maslahi yako yako wapi.

Magufuli na watu wa CCM siku zote wataona wanachosema viongozi wa upinzani ni uchochezi
Kwa sasa raia wa Tanzania wakimkosoa Magufuli au serikali wanaonekana kuwa ni wachochezi
Ndugai na viongozi wa Bunge siku zote wataona wabunge wapinzani wakipinga hoja za seerikali BUngeni ni uchochezi
Ndugai aliona Prof Assad akiwa CAG kulikosoa Bunge ni uchochezi japo aliongea ukweli
Serikali ya Makaburu iliona kile Mandela na wenzake walichoongea kudai haki sawa Afrika Kusini ilikuwa uchochezi

Watu wasiofuata haki siku zote wana maana yao ya neno uchochezi kwa namna ya kulinda maslahi yao. Ni wazi sana hapa maslahi yako yako wapi.
Synthesizer, hapa rais na CCM wameingiaje sasa?
 
Acha uchonganishi!
Yule meneja hakubaki pale kwa kile cheo bali alibaki kama mmoja wa wataalam wa madaraja.
Waziri mkuu alieleweshwa vyema na akaelewa.
 
Sidhani kama Majaliwa atasahau hili. Akija kuwa raisi kitu cha kwanza ni kubadilisha jina la flyover ya Tazara. Na usisahau kwamba Majaliwa alikuwa na moto sana mwanzoni, siku moja akazimwa hadharani na raisi na kuambiwa hata yeye anaweza kutumbuliwa kama wengine. Hiyo ilimnyamazisha sana Majaliwa.

Lakini tambua kwamba Magufuli anajua hilo. Sio rahisi Majaliwa kuja kuwa raisi katika mazingira kama hayo.
Atakuwa Rais wa wapi?
 
Mbona mnajadili sana habari ya Engineer wa Tanroad?

Huo ni uchonganishi.

Au mlitaka PM ajiuzuru kwa vile agizo lake halikutekelezwa?
 
Synthesizer, hapa rais na CCM wameingiaje sasa?
Mkuu, context ya "uchochezi" kwa sasa iko katika jambo lolote utakalosema kuhusu Raisi au upinzani na ushindani wa kisiasa dhidi ya CCM. Ndipo wanapoingia.
 
Mbona mnajadili sana habari ya Engineer wa Tanroad?

Huo ni uchonganishi.

Au mlitaka PM ajiuzuru kwa vile agizo lake halikutekelezwa?
Hahaha! Wewe unatusema sie wachonganishi, sasa kusema tunataka PM ajiuzuru kwa kuwa agizo lake halikutekelezwa huo sio uchonganishi wa PM na Raisi?
 
Acha uchonganishi!
Yule meneja hakubaki pale kwa kile cheo bali alibaki kama mmoja wa wataalam wa madaraja.
Waziri mkuu alieleweshwa vyema na akaelewa.
Basi unaongea kitu ambacho hakijaripotiwa. Wewe hayo yote umejuaje?
 
Kuna hadithi ya barmaid mmoja alikuwa anagawa mzigo kwa mwenye bar alisumbua sana wateja tuliwaachia bar yao wahudumiane wawili tu
 
Basi unaongea kitu ambacho hakijaripotiwa. Wewe hayo yote umejuaje?
Kwenye instagram page nyingi tu za vyombo vya habari vya Tanzania ikiwemo clouds,Tbc n.k.
Maelezo ya Mfugale yalipelekea Waziri Mkuu amwambie "nashukuru kwa hayo maelezo maana nilifikiri kuna kamgomo baridi."
 
Mkuu, context ya "uchochezi" kwa sasa iko katika jambo lolote utakalosema kuhusu Raisi au upinzani na ushindani wa kisiasa dhidi ya CCM. Ndipo wanapoingia.
Synthesizer, si unachotaka ni ama meneja achuliwe hatua kama PM alivyoagiza au Mfugale atumbuliwe kwa kumpuuza PM? Huo ndo uchochezi
 
Back
Top Bottom