Mfugale awavimbia Waziri Mkuu na Waziri wa Ujenzi kwa kivuli cha Rais Magufuli?

Acha uchonganishi!
Yule meneja hakubaki pale kwa kile cheo bali alibaki kama mmoja wa wataalam wa madaraja.
Waziri mkuu alieleweshwa vyema na akaelewa.
Asante kwa kumueleza ukweli.
 
Synthesizer, si unachotaka ni ama meneja achuliwe hatua kama PM alivyoagiza au Mfugale atumbuliwe kwa kumpuuza PM? Huo ndo uchochezi

Au PM ajiengue ( ajiuzuru) kwa agizo lake kutotekekezwa.

Ina maana Huyo Engineer gafla paa kanyamaza, tutarajie tatizo la ujenzi wa madaraja?

Kwenye darasa lao Huyo Engineer walikuwa wangapi?

MFUGALE FIKIRI UPYA. MWOMBE RADHI PM.
 
Kwenye instagram page nyingi tu za vyombo vya habari vya Tanzania ikiwemo clouds,Tbc n.k.
Maelezo ya Mfugale yalipelekea Waziri Mkuu amwambie "nashukuru kwa hayo maelezo maana nilifikiri kuna kamgomo baridi."
Ahaa. Mkuu umeongea point nzuri. Sasa kumbuka kwamba hii thread imeandikwa kutokana na habari ilivyoripotiwa katika IPPMedia na Mwananchi, ambazo zimewekwa kama source. Sasa iweje maelezo unayosema yako Instagram lakini magazeti makubwa kama IPP na Mwananchi hawakuipata?

Mkuu angalia isije ukawa unatoa habari ya kutengenezwa baada ya uongozi kuona kuna tatizo na sasa wakatafuta namna ya kufanya "damage control" na kutengeneza hizo habari ulizoona wewe. Serikali itatumia magazeti ambayo ni rahisi "kutumika" katika damage control, lakini hawataenda IPPMedia na Mwananchi.

Hebu tuwekee link ya hivyo vyombo vya habari unavyovisema vimeripoti tofauti na IPPMedia na Mwananchi.

Mimi nadhani kulikuwa na mkakati wa damage control baada ya uongozi kuiona hii thread na kuona kweli protokali iliborongwa. Hiyo ni namna ya damage control na ku-save face, ili Mfugale asiwajibishwe na Majaliwa aridhishwe na wananchi wapigwe goli la dobo.
 

Mkibishana na kuwadharau watendaji mtaiua nchi. Maprofesa ni wengi lakini Einstein ni mmoja tu. Shika kauli yangu na utafakari.
 
Agizo la Majaliwa lilikuwa la kipuuzi sana.

Tangu uhuru kuna madaraja mangapi yamevunjika kwa sababu tofauti tofauti? Hili la mvua linaweza kutokea popote.

Engineer awe na kazi ya kubashiri madhara kwenye madaraja? Kikubwa ni kuhakikisha yana viwango stahiki wakati wa ujenzi.

Ukaguzi ni sawa lakini he akikagua leo lipo sawa na kesho mvua kubwa ikanyesha, bado alaumiwe?

Kwa hili PM alichemsha.
 
Mkibishana na kuwadharau watendaji mtaiua nchi. Maprofesa ni wengi lakini Einstein ni mmoja tu. Shika kauli yangu na utafakari.
Kwa hiyo ni halali kwa watendaji kufanya dharau ili tusiue nchi? Surely kuna katika system yeyote lazima kuwe na checks and controls? Chanzo cha yote ni nini - uzembe katika kusafisha njia ya maji kwenye daraja na kusababisha uharibifu wenye hasara kubwa. Sasa watu wasiwajibishwe kwa kuwa ni watendaji tutaua nchi?

Mara ngapi nimesema humu ndani kwa nini TANROADS hawafanyi ukaguzi wa mara kwa mara wa barabara kuu matokeo kunakuwa na mashimo makubwa ya ghafla barabarani ambayo yamesababisha ajali nyingi zilizoua watu? Kitu gani kinawashinda Tanroads kufukia haya mashimo hata kwa mawe na mchanga kwa muda na kuzuia ajali hizi?

Sema, ni ajali ngapi umesikia zilitokea kwa kuwa dereva alikuwa anakwepa shimo kubwa barabarani aliloliona ghafla? Je umesahau waandishi wa habari waliokufa kwa ajali kama hiyo? Na kwa nini hilo shimo liwepo barabarani kwa muda wa zaidi ya mwezi au hata wiki na Tanroads wapo na pesa ya kurekebisha vitu kama hivyo tunachangia katika kununua mafuta?

Unasubiri ndugu yako wa karibu afe kutokana na gari yao kugongwa na basi lililokuwa linakwepa shimo na kuhama upande wake ndio muelewe uzembe wa TANROADS ambao Majaliwa alikuwa akiukemea hapa?

Angalia hii thread ya 31 Dec 2029. Lazima tukiri uzembe wa Tanroads

Ajali iliyoua watu 6 Dodoma: Wanaopaswa kukamatwa na kuwekwa ndani ni Mfugale na Meneja wa Dodoma wa TANROADS Dodoma, sio dereva wa lori
 
Kwenye instagram page nyingi tu za vyombo vya habari vya Tanzania ikiwemo clouds,Tbc n.k.
Maelezo ya Mfugale yalipelekea Waziri Mkuu amwambie "nashukuru kwa hayo maelezo maana nilifikiri kuna kamgomo baridi."
Mfugale alisema hivi,
Kwamba ameamua kumbakisha engineer wa kawaida na siyo Kama Meneja wa mkoa wa Tanroad ili Elimu na utaalamu wake utumike kwenye kujenga hilo daraja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni kulaumu bila kuwa na taarifa zote. Majaliwa aliuliza chanzo cha daraja kukatika. Akaambiwa kwamba daraja lilikatika kwa kuwa kutokana na mvua za muda mrefu kulikuwa na accumulation ya takataka chini ya daraja zilizofanya maji yasipite vizuri. Kutokana na hili maji yalianza kuchimba kingo za daraja na kutengeneza njia mpya, na hatimae daraja kusombwa.

Ndipo akauliza, kwa nini ukaguzi hauuwa unafanywa kuhakikisha tatizo kama hilo halitokei? Ni kwamba kama TANROADS wangekuwa wanafanya ukaguzi basi wangeona takataka zilizo accumulate chini ya daraja. Zingesafishwa daraja lisingesombwa na kukatika kwa kuwa maji yangekuwa na free flow.

Mbona Majaliwa alieleza hili? Acheni kukurupuka kutoa comment bila kujua kisa chote.
 

Nakuelewa kuhuzunishwa na kusononeshwa na yote uliyoyataja. Na huko ndio kuwajibika na kuwa na uchungu na nchi yako.

Ninachokisema mimi ni hiki na si kwa huyo aliyeondolewa katika nafasi hiyo tu bali kwa nchi nzima kwa ujaumla. Soma vizuri:

Sipendi hata siku moja maswala ya kitaalam yatatuliwe kisiasa. Wakuu wa mikoa, wilaya na mawaziri wamekuwa wakihamaki kutoa adhabu kwa kukurupuka, tena hadharani hivi hasa dhumuni ni nini kama sio kujiimarisha kisiasa. Rejea hotuba ya kiongozi wa chama cha madaktari kwa Rais Magufuli juu ya kipengele cha kuwekwa ndani madaktari na manesi mbele ya hadhara.

Kulikuwa na ugumu gani kwa Waziri mkuu kukaa kikao ofisini na Mfugale na kuchukua uamuzi wa pamoja baada ya kumsikiliza mkuu wa mfanyakzi huyu ana maoni gani? Huu ndio utendaji kazi pahala popote pale, ambao utaweza kuepuka mgongano wa viongozi kama ulivyoueleza katika thread yako.

Najua uchaguzi ni karibu lakini wanasiasa ni lazima wajiangalie sana na kuacha tabia hii mara moja.
 
Jadili mambo ya msingi namna kukwamua jamii yako kiuchumi na kuondoa njaa kijijini kwenu unapata muda wa kujadili watu wenye uhakika na kula.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa ndugu yangu. Sio kuwa nina chuki na Mfugale. Mimi nadhani uhusiano wake na Magufuli unamfanya ajisahau sana. Ingekuwa busara kama Magufuli angemhamisha - siku zote familiarity breeds contempt. In fact suala alilosema Majaliwa kwa nini TANROADS hawakagui barabara nililisema katika hii thread yangu ya December mwaka jana

Ajali iliyoua watu 6 Dodoma: Wanaopaswa kukamatwa na kuwekwa ndani ni Mfugale na Meneja wa Dodoma wa TANROADS Dodoma, sio dereva wa lori
 
Jadili mambo ya msingi namna kukwamua jamii yako kiuchumi na kuondoa njaa kijijini kwenu unapata muda wa kujadili watu wenye uhakika na kula.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na kwa maoni yako suala la uzembe unaosababisha daraja kusombwa na njia kuu ya Morogoro - Dodoma kufungwa kwa siku kadhaa sio suala la kukwamua jamii kiuchumi? Hebu kasome thread za Waziri akojoa kitandani kwenye forum za udaku usitupotezee muda hapa.
 
You have a point if that is the case.
Kwa maana hiyo naona Mfugale anamlinda mwizi mwenzie wajenge lingine wapige pesa na kiranja mkuu
 
You have a point if that is the case.
Kwa maana hiyo naona Mfugale anamlinda mwizi mwenzie wajenge lingine wapige pesa na kiranja mkuu
Thanks brother, apologies for any misunderstanding between us
 
sikiliza kuanzia sekunde ya 2.30 mpaka 4.01 utajua ukweli halisi.
ahsante
 
sikiliza kuanzia sekunde ya 2.30 mpaka 4.01 utajua ukweli halisi.
ahsante
Asante sana Mkuu. Hii imeondoa ukakasi wote wa hili suala. Nashangaa kuna watu walikuwa wanabisha humu bila hata kuwa wameona hii clip ambayo inasaidia sana.

Me namuunga mkono Majaliwa 100%, na bado nasema Mfugale naye ni wa kuwajibishwa tu, TANROADS ni wazembe hata ukiniamsha usingizini nitakuambia hivyo.

Kwa nini Mfugale anangoja kuambiwa na PM juu ya kugagua madaraja hasa katika kipindi cha mvua? Na sio madaraja tu, hata mashimo makubwa barabarani. Watu wangapi wamekufa katika ajali ambazo chanzo chake ni shimo la ghafla barabarani? Mfugale hilo halioni hadi aambiwe na PM kuhusu jinsi ya kushugulika na hayo mashimo? PM amemkumbusha kwamba kuna hela za matengenezo ya kila siku, TANROADS wanazitumia wapi?

Yaani Mfukgle yeye anachoona ni kujenga flyover Dar es Salaam, ili amfurahishe Magufuli. Nimesema haya, zaidi ya ukaguzi wa madaraja;

Ninachotaka kuona ni kimoja tu - Magufuli atoe amri kwa Mfugale kwamba kuanzia sasa sitaki kusikia ajali imetokea kwenye barabara kuu za lami za TANROADS na chanzo eti kulikuwa na gari ikikwepa shimo dereva aliloona ghafla katikati ya barabara.
  1. Fanya ukaguzi wa kila wakati wa barabara kuu zote za lami na kuhakikisha eidha mashimo yamefukiwa permanently au kwa hatua za muda
  2. Shimo lolote lililofukiwa kwa hatua za muda sehemu hiyo iwekwe alama za tahadhali kwa madereva kuwaonya juu ya uwepo wa shimo kubwa barabarani. Kwa hiyo wakaguzi watembee na alama za onyo kuweka barabarani
  3. KIla mvua kubwa ikinyesha TANROADS wapite kufanya ukaguzi barabarani kuhakikisha hakuna vifusi vilivyuporomokea barabarani. KUna ajali ilitokea mikumi kutokana na hili
  4. KIla Mkoa wa TANROADS uwe na kikosi cha kazi cha kurekebisha barabara kwa muda na kiwe on call masaa 24 kwa siku katika siku saba za juma
  5. TANROADS wawe na call centre ya road emeregencies na watoe namba za simu za emergency au watumie 112 ili madereva wanapoona hali mbaya barabarani wawapigie na watatue hilo tatizo mara moja. Namba hizi zitangazwe kikamili pamoja na kuwekwa kwenye stika za insurance ili watu wazione na kuzijua
Hebu niambieni wana JF, Mfugale akitekeleza haya, ni ajali ngapi na vifo vingapi vitaepushwa? NI gharama kubwa kiasi gani itahitajika kufanya haya?

Je tumesahau ile ajali ya Mafinga iliyoua watu zaidi ya 40 palepale ilikuwa tu ni suala la uzembe kama huu ambapo upande mmoja wa barabara ulikuwa haupitiki na basi (Majinja) ikagongana na lori katika kukwepa upande wa barabara usiopit
ika?
 
PM hajakurupuka kutoa ilo agizo kumbuka nae ana inteligency inayompa taarifa za kila kitu.
 
Siri kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…