Mfugale awavimbia Waziri Mkuu na Waziri wa Ujenzi kwa kivuli cha Rais Magufuli?

Naona kama umejaa chuki tu, nae waziri mkuu kuna muda awe anatumia busara sio kukurupuka tu. Huyo RM angefanya ukaguzi ndio angezuia mvua? Acheni kukurupuka tu, kwakuwa ameongea PM. Hiyo ndio inaitwa force majoue, yaani hakuna wa kuizuia labda Mungu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Huyo ndiye waziri wa ujenzi ajaye kwenye baraza lijalo la mawaziri.
 

Huyo ndiye waziri wa ujenzi ajaye kwenye baraza lijalo la mawaziri.
 
Mfugale ni kakiba ya watu wasiotayari kupelekeshwa. PM angemjua vizuri huyu jamaa, angejadiliana nae kabla ya kuchukua hatua hiyo.
 
Namwona mfugale yupo sahihi. Andendekisye sijui andembwisye aitwe ahojiwe.wanasiasa wa hovyo sana.kuna mmoja mjinga alitaka sababisha jamaa yangu amwache mkewe kwa ushauri wa kijinga
 

Majaliwa sio mamlaka ya nidhamu ya huyo Injinia, wala si mamlaka ya nidhamu ya Mfugale. Kama usemacho ndicho basi angemtumbua Waziri Kabisa, sio mfugale wala sio huyo injinia. Hiyo ndio dhana ya uwajibikaji. Itoshe tu kusema Majaliwa alichemka
 
Serikalini ni majungu vita na fitina kila uchao..yawezekana wewe ulieleta uko Tanroad unataka Andalwisye afukuzwe ..chuki tu kazi za umma zinamfanya mtu anakua na roho mbaya itadhani atakaa milele...mwache Mfugale na PM wataelewana
 
Lihehe lina kiburi lile balaa. Yani Mfugale muoneni tu hivi ila ana kiburi na kujiona mwamba. Nahisi ndiyo maana kabla hata kile ki fly over uchwara pale TAZARA Magufuli alikipa jina la Mfugale kabla hata hakijaanza kujengwa ili Mfugale akisimamie kwa umakini zaidi. Wahehe ukijua kuchezea akili yao mbona anaweza hata kujinyonga kwa furaha! Nakumbuka siku ya uzinduzi wa hicho ki fly over mwandishi akajichanganya akakiita TAZARA acha povu limtoke Mfugale eti umekosea haiitwi TAZARA bali inaitwa MFUGALE 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 

Mtanzania halisi huyu. Mpenda magomvi. Mpenda unbeya na mchonganiishi. Ulikuwepo ukaona na kusikia jinsi mazungumzo yalivyojiri? Then unasahau kuwa JPM na KM Ni watu wa Karibu sana. Na KM anaaminika na JPM. Ndo mana bado Waziri Mkuu.

Why watanzania tunafurahia sana visasi na kuanguka kwa wengine?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfugale ni mmoja Kati ya viongozi wachache wa vitengo wanaojielewa hawafanyi kazi Kwa mihemko hata hao wa juu yake wanajua hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,

Unamkumbuka injinia wa jengo la hospitali kuwekewa lifti alivyopambana na Magufuli.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfugale aliongea kuwa hiyo barabara inahitaji matengenezo makubwa na umri wa madaraja ni 25 years wakati sasa imefikisha 40 years. Wewe unalalamika tu je, una uhakika gani kama wanapewa fedha zote zinazohitajika kufanya ukarabati wa madaraja? Viongozi wengi sasa hivi wanakurupuka tu na kutoa maagizo bila kutafuta sababu kwa nini kitu fulani kiko hivyo kilivyo. Nasimama upande wa Mfugale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa. Eti hospital isiwe na elevator. Uliona wapi???!!!!! Kama wodi ziko juu na mortuary iko chini mtu akifa anapelekwaje? Suppose jiko liko chini wodi juu vyakula vya wagonjwa vitapelekwaje??!! Wagonjwa wasioweza kutembea wanapelekwaje from one floor to another? Uongozi wa camera camera camera mpaka unatia kichefuchefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inamaana wewe unataarifa kamili kuliko Waziri Mkuu kuhusu hizo barabara? Si hao hao watendaji ndio wanaomtaarifu Waziri Mkuu juu ya mpangilio wa utengenezaji wa hizo barabara?
Hali ya hiyo barabara aliizungumzia Mfugale mwenyewe kuwa ni nzee na inahitaji matengenezo makubwa hasa madaraja ambayo life span yake ni 25 years wakati hadi sasa yana 40 years.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…