Mfuko 1 wa cement unajengea tofali ngapi (block inch 5)?

Kichwa cha habari kinajieleza.

Kwenye ujenzi ile concreteNess ndio itaamua zaidi utumie ndoo ngapi/per ndoo hizo 50 to 70 ni za cement ya kupapasa ambapo baada ya muda nyumba zinatoa nyufa. ..ulihitaji uimara wa nyumba tumia 35 as max.
 
Naona kila mtu anatoa, majibu yake. Mimi nipo kwenye field kimsingi mimi natoa tofali 45-48 ila ukizidisha hapo tofali zinakua sio imara. Mchanga unakua mwingi kuliko ratio ya cement, ndio zile tofali zinazopukutika au ukibeba kwenye gari zinavunjika nyingi
 
mimi sio Fundi ila kuna uwiano mkubwa kati ya ratio ilotumika kwenye kufyatua tofali na ratio ya mota ya kujengea.

Ni ukweli kwamba mfuko mmoja unaweza kujenga tofali hata 80 na nyumba ikawa imara na usione nyufa kabisa na unaweza jenga tofali 40 na nyumba ikajaa nyufa. kila kona.

mfano. tofali za ratio ya 50 kwa mfuko katika ufyatuaji huezi jengea kwa mota ya ratio ya tofali 30 ukakosa nyufa katika nyumba.

NENDA Arusha nyumba zimejengwa kwa tofali inaitwa chepele (biscuit) ukiiona unaeza shika kichwa lakini zinadumu na nyufa hakuna japo cement ni harufu tu na tofali hiyohiyo imejengwa 1/90.
 
Naona kila mtu anatoa, majibu yake. Mimi nipo kwenye field kimsingi mimi natoa tofali 45-48 ila ukizidisha hapo tofali zinakua sio imara. Mchanga unakua mwingi kuliko ratio ya cement, ndio zile tofali zinazopukutika au ukibeba kwenye gari zinavunjika nyingi
Hujaelewa swali
 
Kichwa cha habari kinajieleza.

Mfuko 1 wa cement unajengea tofali ngapi (block inch 5)?
Kwa ratio ya 20 yaani ndoo ndogo 20 kwa mfuko, zinajenga tofali 80-90 za kusimama.

Kwa ratio ya 25, ndoo 25 ndogo kwa mfuko, zinajenga tofali 100+ za kusimama.
 
Naona kila mtu anatoa, majibu yake. Mimi nipo kwenye field kimsingi mimi natoa tofali 45-48 ila ukizidisha hapo tofali zinakua sio imara. Mchanga unakua mwingi kuliko ratio ya cement, ndio zile tofali zinazopukutika au ukibeba kwenye gari zinavunjika nyingi
Sio kufyatua tofali,
bali kuunga tofali na tofali (mota)
 
Pia, mfuko Mmoja wa cement unapiga plasta mita square au mita za mraba 162.
Sio sahihi, chumba cha futi 10 kwa futi 10 tu kinatumia mifuko miwili ya cement ktk plastering na kina surface area ya 30m² ~ 35m². Kiufupi area coverage ya cement ktk plastering inadepend na ratio iliyotumika, mtu aliyetumia ratio ya 1:4 area coverage yake itatofautiana na mtu aliyetumia ratio ya 1:5 etc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfuko ni tofali sabini gawa hapo.
Duh! Zitakua tofali kweli hizo mkuu! Ndio maana nyumba za sshv hazidumu! Fundi kama ww hata ukipewa site yenye cctv camera utaiba tu! Hufai kabisa
 
Sijui inaweza ukawa unaongelea nadharia lakini kwa vitendo na nyumba hizi za kawaida mfuko average unajenga tofali 70. Kama unafyatua mfuko unatoa tofali 35 hadi 45.
 
Pole sana fundi maiko[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom