Ndugu wananchi,
Kwa kiswahili chepesi, hili dudu linaloitwa mfuko wa jimbo ni lile lile ambalo mwanzoni lilibatizwa jina la takrima. Tukumbuke kuwa ni Bunge ndilo lililotunga sheria, tena mchana kweupee, bila aibu wala soni na kuhalalisha rushwa kuwa eti "African Hosipitality" A.K.A takrima.
Sasa basi,
kama tulivyoichukia takrima hadi tukaibomoa kwa amri ya mahakama, na ikatamkwa kuwa ni kinyume cha Katiba, nadhani hawa Waheshimiwa wamesahau. Kwa hakika na bila shaka kile kikasha tulimotoa wembe ulioinyoa takrima, bado kina nyembe nyingi mpya za kuinyoa CDCF mahakamani na sheria mbofu mbofu. subirini kidogo tu kama mtaisikia CDCF, itabaki kuwa historia.
Maneno yetu mafupi; vitendo vyetu virefu: Eeh Mungu tusaidie.