Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo: CDCF

Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo: CDCF

Sorry Mods sikuiona hii kumbe imeshapostiwa, naomba ifute hii thread iunganishe kule.
 
Huu mfuko sina wasiwasi nao kabisa kwa maana hautakuwa mikononi mwa wabunge bali utakuwa chini ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya DED- ambaye atafuata taratibu zote za kutoa pesa kwa shughuli zilizokusudiwa.Hii siyo desturi ngeni ..... Nch kadhaa wanao - Mauritius, Zambia,Kenya na wanapewa pesa in billions.Huu wa TZ unapewa hela kidogo tu kama milioni 40-50 KWA MWAKA.Ni kwa ajili ya matatizo ya wananchi.
 
Kwa kweli bunge moto, baada ya kupitishwa kwa muswada huu wa CDCF kiulaini, muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Wanyamapori wakwama, Mwakyembe, Sendeka na Zitto wautilia ngumu, hebu na tusubiri tuone mwisho wake.
Serikali imekubali, imekifuta kifungu cha 5 na sasa umepitishwa.
 
Last edited by a moderator:
Ninachoshangaa sana Waziri Mhusika ni Waziri wa TAMISEMI. Hivi haoni kama hiyo inaleta mkanganyiko na kazi za council? Anyway, sijajua huu mfuko utasimamiwa vipi? signatories ni nani? miradi ya kutekeleza itachaguliwa vipi? auditors wapi ndo watahusika nk.

Endapo mfuko huo utasimamiwa na ofisi ya Mbunge, basi kuna haja ya kufanya blanda kubwa zaidi na kuajiri watumishi wa ofisi ya Mbunge. Vinginevyo huu ni wizi tu, na wale wapambe wa wabunge wanaandaa midomo ya kuila pesa ya walipa kodi.
 
Huu mfuko sina wasiwasi nao kabisa kwa maana hautakuwa mikononi mwa wabunge bali utakuwa chini ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya DED- ambaye atafuata taratibu zote za kutoa pesa kwa shughuli zilizokusudiwa.Hii siyo des.Tena huu wa TZ unapewa hela kidogo tu kama milioni 40-50 KWA MWAKA.Ni kwa ajaili ya matatizo ya wananchi.

Jirani, ni nani atakayekuwa anaufuatilia mfuko huo kuhakikisha hakuna upendeleo katika kutoa pesa hizo za matatizo ya Wananchi? Maana unaweza kukuta pesa zinatolewa hata kwa wananchi ambao hawaishi jimboni. Kwa maoni yangu ni lazima CAG aweze kuukagua mfuko huo kila mwaka vinginevyo kutakuwa na ufisadi wa hali ya juu na kama unavyoijua nchi yetu hakuna hata kimoja ambacho huwa kinaendeshwa bila dosari. Si unaona mabilioni ya Mkuu w Kaya yalipigiwa debe zito nchi nzima lakini sasa hivi ukiuliza mabilioni hayo yamefanikisha kipi cha maendeleo katika nchi yetu hutapaka jibu la kueleweka.
 
nina shaka kubwa na usimamizi wa mfuko huu kwani sina imani na wasimamizi wake hata kidogo. Hii ni aina nyingine ya ufisadi na matumizi mabaya ya pesa za umma. Je kweli tunahitaji wabunge kupitia huu mfuko kutatua matatizo ya wananchi? Ni matatizo gani ambayo kweli yatatuliwa na Shs 40 millioni? Wabunge wetu ni "wamelo", "wabinafsi" na wametindiwa mawazo! Ukiangalia takwimu nchi yetu bado kushinda vita dhidi ya umasikini, ujinga na maradhi! Je pesa hizo mfano zingepelekwa kuboresha hospitali za rufaa mbeya au mwanza je si jambo la kujivunia! Hebu ifike wakati wabunge nao wawajibike kwa maslahi ya taifa na sio kuiga mambo yasiyo kuwa na msingi. Je kweli nchi zenye mfumo huu wamefanya nini cha maana kuliko sisi? Ukweli ni kwamba hakuna chochote hali ni mbaya tu na pesa za walipa kodi zinapotea bure! Sijui na sipendi kukata tamaa kwani nimechoshwa na dhuluma zinazofanywa na viongozi wetu chini ya mwamvuli wa kusaidia wananchi. Natamani siku ile ambayo wananchi wote wataingia barabarani na kudai haki zao, natamani kuiona siku ile ambayo nitaona dola hii iliyokosa hisani ikianguka maana imeshindwa kuwajibika ipasavyo. Kama wahenga wasemavyo Mungo si athumani ipo siku tu haya yatatimia.
 
Ndugu wananchi,
Kwa kiswahili chepesi, hili dudu linaloitwa mfuko wa jimbo ni lile lile ambalo mwanzoni lilibatizwa jina la takrima. Tukumbuke kuwa ni Bunge ndilo lililotunga sheria, tena mchana kweupee, bila aibu wala soni na kuhalalisha rushwa kuwa eti "African Hosipitality" A.K.A takrima.

Sasa basi,
kama tulivyoichukia takrima hadi tukaibomoa kwa amri ya mahakama, na ikatamkwa kuwa ni kinyume cha Katiba, nadhani hawa Waheshimiwa wamesahau. Kwa hakika na bila shaka kile kikasha tulimotoa wembe ulioinyoa takrima, bado kina nyembe nyingi mpya za kuinyoa CDCF mahakamani na sheria mbofu mbofu. subirini kidogo tu kama mtaisikia CDCF, itabaki kuwa historia.
Maneno yetu mafupi; vitendo vyetu virefu: Eeh Mungu tusaidie.
 
Nafikiri mfumo wa kikoloni ingawa ulikuwa ni wa kibaguzi lakini ulikuwa na tija kuliko huu ambao tumejiwekea sasa. Mfumo wa kikoloni ulikuwa na dira na hakika walifanikiwa katika kutimiza azma yao. Muundo wa mfumo tulio nao ni mbovu na hata mtaalam na msomi aliyebobea kwa mambo ya miundo na mifumo ya kiutawala alipondekeza mfumo wa serikali hasa za mitaa alipingwa kweli na proposal yake ikatupwa! Mfumo tulio nao una gaps nyingi tu na ndio kikwazo kikubwa cha kutokuwa na maendeleo ya jumla ya kijamii na kiuchumi. Hakuna uwajibikaji bali ni siasa tupu, longolongo kila mahali, mgongano wa madaraka etc. Sasa cha kustajabisha ni mfuko wa maendeleo ya wabunge.... hiki ni kioja kabisa! Hivi hiyo pesa itatoa chachu gani ya maendeleo jimboni? kwanini hizo pesa basi zisielekezwe kwenye ujenzi wa nyumba za walimu, ujenzi wa madarasa bora, zahanati au ununuzi wa vifaa kwenye hospitali za rufaa! hii haitaji mtaalamu wa maroketi kuweza kujua ni nini jamii inakosa au inahitaji.
 
Back
Top Bottom