Joseph Isaack
JF-Expert Member
- Aug 8, 2011
- 450
- 89
Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa tatizo la kuporomoka kwa ubora wa Elimu linasabishwa na mfumo mbovu wa ukaguzi. Akiongea na Wakuu na wamiliki wa shule na vyuo binafsi jijini mbeya, Raisi kikwete amesema kuwa tatizo la kushuka kwa Elimu nchini kunasababishwa na mfumo mbovu wa Ukaguzi toka ngazi ya shule hadi kwenye idara ya ukaguzi. Aidha Rais Kikwete ameahidi serikali yake kuzishughukia kasoro hizo pamoja na kufanya kurekebisho katika Sera ya Elimu nchini. Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu nchini Mh. Philip Mulugo amesema serikali inafanya utafiti kuweza kubaini gharama halisi za Elimu nchini ili kutoa gharama elekezi za ada ya shule Kwa shule zote nchini. Source: RFA.