Mfumo mbovu wa Ukaguzi ndo chanzo cha kushuka kwa Elimu nchini:JK.

Mfumo mbovu wa Ukaguzi ndo chanzo cha kushuka kwa Elimu nchini:JK.

Joseph Isaack

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2011
Posts
450
Reaction score
89
Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa tatizo la kuporomoka kwa ubora wa Elimu linasabishwa na mfumo mbovu wa ukaguzi. Akiongea na Wakuu na wamiliki wa shule na vyuo binafsi jijini mbeya, Raisi kikwete amesema kuwa tatizo la kushuka kwa Elimu nchini kunasababishwa na mfumo mbovu wa Ukaguzi toka ngazi ya shule hadi kwenye idara ya ukaguzi. Aidha Rais Kikwete ameahidi serikali yake kuzishughukia kasoro hizo pamoja na kufanya kurekebisho katika Sera ya Elimu nchini. Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu nchini Mh. Philip Mulugo amesema serikali inafanya utafiti kuweza kubaini gharama halisi za Elimu nchini ili kutoa gharama elekezi za ada ya shule Kwa shule zote nchini. Source: RFA.
 
Waakaguzi wa Elimu hawana mafungu ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.Mafungu machache yanawezesha kufanya kazi kwa kiwango cha chini na mwisho wa siku taarifa zao hazifanyiwi kazi.Matokeo yake ndio tunayaona sasa.Tusimtafute mchawi wa matokeo tunayoyashuhudia sasa.Tutaendelea kushuka sana hadi mitaala ipitiwe upya kwa mahitaji ya sasa.
 
mkuu suala si mfumo mbovu bali posho ya wakaguzi hao ni ndogo ndo mana kazi wanaripua ripua jaribuni kuongeza posho mtaona kazi itakavyo kuwa.
 
Tatizo sio kukaguliwa tatizo ni kukata tamaa kwa waalimu,hata wakiwakagua usiku kucha kama hawatawafanya walimu wawe na moyo wa kufundisha hakuna watakalofanya. Mfano walimu huwa wanafundisha mpaka mida ya jioni ila kwa miaka ya hivi karibuni hawafundishi tena je nalo hilo linahitaji wakaguzi?
 
sasa kama rais hajui kwa nchi yake maskini unategemea atujua chanzo cha kushuka kwa elimu tatizo watanzania tunapenda sana majibu ya zimamoto kwenye maswali magumu.
 
naona mheshimiwa anajaribu kutibu dalili badala ya ugonjwa.ts just a mattaer of time....
 
Back
Top Bottom