Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari!
Huu mfumo si mpya sana maana una miaka zaidi ya miaka 2 hivi hapa nchini tangu uanze kutumika.
Ni mfumo wa Kidijitali wa pamoja wa malipo ya kiserikali.
Mfumo huu ni mwiba kwa wahasibu wezi na watumishi mafisadi.
Ulianzishwa na serikali ya Magufuli. Uliweza kufuta matumizi ya check katika ofisi za umma. Wakati check zinatumika wahasibu wahuni either kwa kushirikiana na mabosi wao au kwa kughushi saini za mabosi walikuwa wanaweza kuiba mpaka milioni 100 pasi kushitukiwa, lakini sasa hawawezi.
Kwa mfumo huu wa MUSE kama unasoma uhasibu ili uje uchote mapesa serikalini basi ni heri uache chuo na hiyo ada ukanunue mbwa kawinde sungura pori.
Ok turudi kwenye mada. Mazuri ya mfumo huu atakuja kuyazungumzia mwingine, mimi leo nazingumzia mabaya ya mfumo huu wa MUSE.
Mfumo huu unachelewesha malipo kwa watumishi wa mkataba ambao hawalipwi direct na B.O.T, kwakuwa ofisi nyingi za umma hasa zinazojiendesha kibiashara watumishi wake wengi ni wa mkataba.
Kwa mfano tangu mwezi huu wa saba uanze mfumo huu ni kama umekataa kabisa kufanya kazi. Yawezekana watu wa IT nguvu wameishiwa au umefungwa kwa kusudi ili kufanya hesabu za mwaka. Watumishi wa mkataba wanakosa mishahara, watumishi karibu wote wanakosa posho ambazo zinawapa ahueni maana mishahara wameshaikopea.
• Wakandarasi wanashindwa kulipwa kwa wakati kutokana na MUSE, hivyo basi wakandarasi wanashindwa kulipa mishahara kwa watumishi na vibarua na hata materials wanashindwa kununua. Hivyo miradi inasuasua.
Zamani ukipata safari ya kikazi mchana chap unaandikiwa check unasafiri, sasa unakopwa na serikali, utumie gharama zako utakuja kulipwa. Je ni watumishi wote wanaweza kuwa na Malaki ya ghafla kwasababu ya safari za ghafla huku tumishahara twenyewe ni tia maji? Kazi zinalala, morali inakata.
Huu mfumo ni mbaya sana kwa maendeleo ya nchi. Ufutwe na kuanzishwa mfumo mwingine au uboreshwe.