SoC04 Mfumo na muundo wa elimu ya kitanzania uboroshwe kuendana na fura za kujiajiri na ajira duniani

SoC04 Mfumo na muundo wa elimu ya kitanzania uboroshwe kuendana na fura za kujiajiri na ajira duniani

Tanzania Tuitakayo competition threads

Gaveh wazah

New Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Utangulizi
Tanzania imekua miongoni mwa nchi ambazo imekua ikukumbwa na janga la ukosefu wa ajira kwa wahitimu wa vyuo, vijana na wananchi wengi kiujumla, na tatizo ni kwamba wasomi wamekua ni wengi lakini mahala pakufanyia kazi pamekua ni pa achache au kwa ufupi ajira zimekua finyu lakini wakati huo huo kuna fursa nyingi sana za kujiajiri na Ajira hapa hapa Tanzania na duniani kote kiujumla. Sasa nini kifanyike ili wananchi wa Tanzania hasa wasomi wetu na vijana wote kwa ujumla waweze kuzitumia fursa hizo ?. Kinachotakiwa ni kuboreshwa kwa mfumo na muundo wa elimu ya kitanzania, kuendana na fursa za kukiajiri na ajira duniani.

kivipi mfumo na muundo wa elimu ya kitanzania utaboreshwa kuendana na fursa za kujiajiri na ajira duniani ?.
Mifumo na miundo ya elimu yetu inatakiwa kuboreshwa katika nyanja zifuatazo.
a).Sayansi na Teknolojia
b).Lugha za kufundishia na muhimu
c).Ulindwaji na ukuzwaji wa vipaji vya michezo vya wanafunzi.
d).Elimu ya kujitegemea na ujasiriamali
e).Elimu ya Ufundi


Sasa nyanja tajwa hapo juu kama zitareboreshwa kama ambavyo nitapendekeza katika ufafanuzi wangu ufuatao na utekelezwaji wake ukaanza katika awamu ijayo ya mwaka 2025, basi nina imani ya dhati kabisa swala la ajira litakua siyo janga tena kwa Tanzania kwa miaka 15 ijayo Tunaanza kama ifuatavyo👇🏾.

a).Elimu ya sayansi na Teknolojia.
Kama tunavyojua maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaenda kwa kasi sana duniani kote, sasa kinachotakiwa kufanyika na kama ambavyo wenzetu wa nchi zilizo endelea mfano Marekani na Uingereza ni kuendana na mabadiliko ya kasi ya sayansi na yeknolojia. sasa kivipi serikali yetu iboreshe sekta hii ya elimu ya sayansi na teknolojia, nina pendekeza ya kwamba elimu hii ianze kufundishwa kwa vitendo kuanzia shule ya msingi kwahyo sasa serikali inatakiwa kufanya uwekezaji wa hali ya juu katika elimu hii kwasababu inahitaji ununuzi wa vifaa muhimu kama vile komputa, tablet, simu janja(smartphones), vyanzo vya mtandao(router, wifi installation n.k), lakini pia lazima iwape mafunzo muhimu walimu amabao watakua wanawafundisha wanafunzia elimu hiyo ndo maana nikasema uwekezaji wa hali ya juu unahitajika.

Sasa ningependa kugusia vipengele baadhi na muhimu katika Sayansi na teknolojia ambavyo kama wanafunzi watafundishwa basi itawasaidia sana katika maisha yao ya kujitafutia vipato vyao baada ya kumaliza masomo yao.

Mfano wa vipengele hivyo ni kujifunza kutengeneza website, application za simu na Software za kufanyia kazi mbali mbali(computer science),lakini pia kujifunza jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii kama vile instagram na tiktok na youtube kwa maana ya kuwaingizia vipato, vile vile, kujifunza namna yakutumia mtandao(internet) vuzuri kwa mamba ya msingi yenye tija katika maisha yao.

Tukianza na kipengele cha Ufunzwaji wa kutengeneza website, applikesheni za simu na computer, na software mbali mbali. kwa dunia ya sasa hapa ndo kwenye hela nyingi kwa wahitimu wa taaluma hii kwa sababu kazi nyingi siku hizi zimekua zikifanyika kwa njia ya computer na mtandao, Wahitimu wa nchi zilizoendelea mfano Marekani wamekua wakitengeneza software na kuziuza sehemu mbali mbali mfano viwandani na kwenye makampuni au maofisi makubwa makubwa kwa pesa nyingi tu za kutosha, na tumejionea kwa wale ambao tumefanikiwa kupita au kufanya kazi viwandani, kazi nyingi zinafanyika kwenye computer kwa msaada wa software hizo, lakini pia hizi Appikesheni za simu mfano facebook, twitter, Tiktok zjnatengenezwa na hapo hao ambao wana elimu ya computer science na wamiliki wa application hizo ni ma trillionea, mfano mzuri kwenye mtandao wa Tiktok kuna mchekeshaji mmoja wa italy anaitwa Khaby lame, yeye analipwa dola laki nne na nusu kwa post yake moja ya Tiktok ni zaidi ya billioni moja nukta 15 kwa fesha ya kitanzania sasa fikiria hao wanaomiliki mtandao huo wanaingiza kiasi gani kwa siku na sio mmoja naelipwa hivyo ni wengi wanalipwa kulingana na wafuasi wake.

kwahyo sasa katika kipengele hicho ni mapendekezo yangu computer science ianze kufundishwa tangu shule ya msingi watoto wajue baadhi ya masomo kama vile Java, Html, CSS, na python japo kwa uchache ili wakifika chuo wasipate kigugumizi. wenzetu washaanza kuwafunza watoto wao elimu hyo.
IMG_0299.jpeg

chanzo:
View: https://youtu.be/_j4Lj-BT00g?si=q5tjptuQ3gkbpBwP

Ufunzwaji wa jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii kwa mantiki ya kuwaingizia kipato na kupata ajira
Mitandao mingi ambayo inalipa ukiwa na wafuasi wengi mfano instagram, tiktok na youtube. lazima tuwafunze watoto wetu jinsi ya kutumia mitandao hii kuwapati kipato badala ya kuitumia kwa ajili ya kuburudika tu. Vile vile kuna mitandao kama vile linkedin, fiver, na job finden hii ni kwa ajili ya kutafuta ajira duniani kote na watu wengi wanapata kazi mbali mbali kupitia mitandao hyo duniani kote.

b). Lugha ya kufunshia na lugha muhimu
Serikali ya Tanzania lazima ikubali kwamba kiingereza ndio lugha muhimu sana kwa vijana wetu mashuleni kwasababu masomo karibia yote yapo kayika mfumo wa kiingereza hivyo basi ili kuwawwpesishia maisha wanafunzi, kiingereza ndio kiwe lugha ya kufundishia tangu shule ya msingi ili wanafunzia waweze kuizoea pia na kama tunavyojua utotoni ndio umri mzuri wa kunasa mafundisho hasa lugha hilo ni moja.
pili. Lazima wanafunzi wajue lugha muhimu ambazo zitawasaidia kufanya kazi watakapo hitimu popote duniani. Lugha hizo ni kiingereza,kama lugha mama, kifaransa, kichina, na kiarabu, hizi ndo lugha ambazo zinatumiwa na asilimia kubwa ya watu duniani, hivyo basi hata kama mtanzania atafungua chanell yake ya Youtube ataweza kupata wafuasi wengi pale atakapo tumia kiingereza au kiarabu badala ya kiswahili kwasababu kuna kitu kitaalamu kinaitwa Algorithim, Hii ni lugha ambayo inamsaidia mtu akitafuta kitu kwenye search engine mfano youtube akipate kiurahisi kwahyo basi watu wengi duniani wanatumia kiingereza au kiarabu kwahiyo ukitumia lugha hizo itakua ni tahisi kwako kujioatia wafuasi wengi badala ya kutumia kiswahili.

c)Ulindwaji na ukuzwaji wa vipaji vya michezo vya wanafunzi.
Kwa dunia ya sasa michezo ni ajira kama tunavyoona kwa wenzetu ulaya wacheza mpira wanalipwa pesa nyingi sana ndani ya wiki moja, kwahyo sasa hivi vipaji vya wanafunzia wetu mashuleni tukivilea vizuri katika maadili ya kimichezo vitaweza kuwasaidia waweze kujipatia ajira zao wenyewe kupitia michezo, kwasababu sio lazima kila mtu apate kazi ofisini michezo pia ni kazi.

d). Elimu ya kujitegemea na ujasiriamali
Katika hili sekta yetu ya elimu lazima iangalie kwa jicho la tatu, ili tuweze kujikwamua kutoka katika janga la ukosefu wa ajira. Hivyo basi katika hili ningependa kupendekeza baadhi ya mawazo ya kijasiriamali ambayo yangeweza kufundishwa kwa wanafunzi mashuleni mpaka vyuoni mfano wanafunzi wafundishwe jinsi ya kutengeneza sabuni za maji, unga, na kipande, Uuzaji wa vyakula kwa njia ya kipekee, lakini pia ubunifu wa idea mbali mbali ambazo zimejikita katika kutatua changamoto mbali mbali katika jamii.

e)Elimu ya ufundi
Elimu ya ufundi ianze kufundishwa tangu shule ya msingi siyo mpaka mtu afeli form four ndo apelekwe veta, inatakiwa watoto wetu waanze kujua ufundi tangu udogoni kwani pengne ndo vipaji vyao vipo huko. Elimu ya ufundi kama vile ufundi seremala, ufundi mekanika ( kutengeneza magari, pikipiki, na bajaji), ufundi ujenzi nakadhalika kwani wenzetu mfano China wanawafundisha watoto wao mambo yakiufundi hali yakuwa bado ni wadogowatoto. Gusa linki hiyo kuona watoto wakichina wakifanya yao
IMG_0301.png

chanzo: wakichina waki assemble bunduki
Kwahvyo basi kuna tija ya serikali kuweka karakana katika kila shule kuanzia msingi, sekondari mpaka chuo ili kuwezesha watoto wetu kujua fani mbali mbali ambazo zitawawezesha kujikwamua katika janga la ajira mara baada ya kuhitimu mafunzo yao

Hitimisho
Endapo mapendekezo haya ya uboreshwaji wa sekta ya elimu ilikuendana na fursa ya ajira na kujiajiri dunia yatafatwa vilivyo na kutekelezwa na serikali ya awamu ijayo basi bila shaka na ukweli usiopingika naiona Tanzania yetu 2050 ikiwa nimiongoni mwa nchi ambazo zimeendelea kwani wananchi wake watakua sio masikini tena, asilimia kubwa watakua wanauwezo wakujipatia vipato vyao vya halali kabisa na bila shaka uborwshwaji huo hautaenda kuwasaidia wanafunzi tu bali pia wazazi wao kwani ujuzi ambao wanafunzi wata upata utakuwa ni rahisi kuwafundisha wazazi wao pia kwani itakua elimu ya vitendo zaidi nasi nadharia.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom