Thee MF
New Member
- Sep 26, 2016
- 2
- 18
Mfumo wa Ajira Nchini kwetu umeshindikana kabisa hasa kwa tusio na Koneksheni kabisaa!
Mfano: nimewahi kuitwa kwenye interview nyingi tu za serikalini ila zote zinafanywa kwa ushahidi tu ili wale wasahili walipwe kwa kupoteza muda wetu.
Viongozi wanakazia eti vijana mjiajiri wanasahau kama Kuji-ajiri pia kunataka Pesa tena muda mwingine ni pesa ndefu kuliko mshahara uliokuwa una vizia kwenye Ajira zao.
Nina rafiki zangu wamesomea Mambo ya tourism 😂 sasa sijui wafuge simba wao au wanunue land cruiser la Million 100 wabebe wazungu.
Mwingine kasomea shipping pale TPA temeke sasa yeye ajiajiri vipi wakati hao TPA wenyewe wameporwa kazi
Kibaya Zaidi niliwahi kuomba nafasi za mafunzo ya JKT ila nikakosa kwa sababu za hovyo sana ila kuna dogo alilazimishwa na dingi ake ila dogo hataki kabisa ni vile tu ana koneksheni zimempa hiyo nafasi ambayo sisi tumenyimwa kwa makusudi apewe dogo asiye itaka tena analalamika tangu kafika mpaka anaondoka, tena kuna muda alitaka kutoroka asiandikishwe ila karudishwa na kiongozi wa pale pale!
Wale walioenda kwenye usahili wa SENSA wanakumbuka balaa la pale na figisu za makusudi!
Wiki kadhaa hapa kulikuwa na usahili wa TAKUKURU. Kuna jamaa angu alifika usahili wa ORAL akaulizwa "Arusha kilitokoea nini juzi kati?" Khee, imagine maswali kama hayo mtu umempandisha basi umemsubirisha masaa!! Umempima vipimo, umemvua nguo alafu unamuuliza Arusha kimetokea nini majuzi kati? Au Tarehe ya kufa Lowasa? Khaaa!
Mi sio adui wa kujiajiri ila kuna vitu haviingii akili na vingine viko nje ya uwezo wetu
Mfano: Wengi tumesomeshwa either na wazazi na ndugu au na serikali (mikopo) ila tulio someshwa na ndugu na wazazi HUWEZI kuwaambia nipeni izo milioni 6 nikafungue biashara sitaki degree haina uhakika wa Ajira!! Mzazi gani au ndugu gani atakubali? Tunabaki kwenye kifungo icho mpaka tunakuja kuteseka mtaani!
Pia baadhi ya ajira za kujiajiri zinataka ukaze roho mfano washkaji uliosoma nao msingi wakafeli wakawa bodaboda au bajaji au car washer! Umewaacha karibu miaka kumi alafu unarud mtaani unamuomba 'deiwaka' aisee inataka moyo!
Mi nanyoa watu Saloon ila bosi wangu nilimuacha shule ya msingi jina lake halikuwa kwenye Listi ya form 1, mimi nina degree langu geto lina mhuri wa mwanasheria! Tuna pambana na Koneksheni huku tuna pambana na ndugu wenye wivu wanao nadhani degree ndio Pesa.
Huku tuna kaza sura kwa aibu tunazopata mitaani 2025 mgombea anasimama anasema MKINICHAGUA NAWAPA UBWABWA!