Mfumo wa counties wa Kenya ni mzuri sana

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Kabla ya katiba mpya Kenya ilikuwa na mikoa 8 ikigawanyika kwenye wilaya 46. Katiba mpya imefuta mikoa na wilaya zikageuzwa kuwa counties zilizoongezewa mamlaka. Hizo conties zinaendeshwa hivi.

1.Kunakuwa na gavana anaechaguliwa na wananchi na makamu wake ambaye ni mgombea mweza. Lazima awe na digrii.

2.Kunakuwa na baraza la county ambalo huundwa na madiwani.

3.Theluthi ya madiwani huwa sehemu ya kamati ya uongozi.

4. Kunakuwa na katibu anayeteuliwa na gavana.

5.Kila county hutoa seneta.

Hapa watu lazima kuwajibika. Kwanini hatujaiga jambo zuri hivi?
 
Red Giant

Huo mfumo uliwekwa kujibu matatizo ya kikabila yaliyoko Kenya. Makabila mengine yalikuwa yakilalamika kuwa yanaletewa wakuu wa mikoa na wilaya wasio wa makabila yao kuja kuwatawala. Walipoweka mfumo huo sasa kila kabila linajichagulia gavana wake na msaidizi wake toka kabila husika.Hivyo unakuta kwenye hizo counties Gavana mkikuyu,msaidizi wake mkikuyu,madiwani wote wakikuyu na senator mkikuyu,na katibu mkikuyu.

Ukienda UJALUONI ni hivyo hivyo GAVANA JALUO,KATIBU JALUO,MADIWANI WAJALUO n.k

Nenda kaangalie viongozi wote wa counties utashangaa ni kabila hilo hilo.CHADEMA Mfumo huu ndio wanautaka kwenye sera zao wanaita sera za majimbo.

Tanzania huo mfumo haufai na sisiti kusema hata Kenya haufai unalea ukabila na ueneo.

angalia mfano KIsumu County uongozi wote jaluo tupu

http://kisumu.go.ke/ click area ya cabinet uone
 
East African Eagle

Mkuu East African Eagle

Premises ulizotumia kujenga hoja yako iko wrong, biased and inclined more to partisan politics. Sio kweli kwamba dhana ya mfumo wa majimbo huko kenya ni ili kujibu takwa la kikabila, siyo kweli hata kidogo. Ukweli ni kwamba mfumo wa kijimbo ulibuniwa kama suluhu ya kugatua madaraka hadi kwa wananchi. Unaondoa mfumo wa kuwa na centralized government system kama waliokuwa nao mwanzo na kama huu tulionao sisi.

Mkuu East African Eagle

Ukweli ni kwamba centralized government system imefeli popote duniani na sababu kubwa mbili ni bureaucracy katika kufanya mipango na maamuzi iwe ya kiutawala au kiutekeleza wa mipango-mikakati. Lakini pia kushindwa ku-prioritize issues kuligana na geo-economics na demands za sehemu husika.

Mfano simanjiro yenye wamasai wengi mahitaji yao makuu ni maji na malisho ya uhakika kwa mifugo yao. Wakati nyanda za juu kusini ni pembejeo kwa ajili ya kilimo. Kwa mfumo wa majimbo kama ule wa kenya county zinakuwa na mamlaka ya kupanga na kuamua namna ya kutatua matatizo yao kulingana na priority.

Kwa taarifa yako tu ni kwamba kwa sasa ukienda Kenya kila county iko busy kujenga miundombinu ya barabara, maji, shule etc tena kwa kushindana. Ni mfumo ambao utaipaisha sana kenya in the next 10 years watakuwa wako mbali saaaana.
 
Last edited by a moderator:
Munira Almasi

Mfumo wa COUNTY kenya ni wa kikabila na nina uhakika na ninachokisema.

Yaite Ni mashindano ya kikabila yatakayopaisha baadhi ya makabila kenya.Kuna makabila kama ya waturkana wako hoi hawana wakushindana naye sababu wamekuwa marginalized kwa miaka.Hawana elimu,hawana vianzo vya mapato ya kueleweka.Mfumo wa county unachofanya aliyekuwa nyuma ahesabu maumivu.

Resources nyingi zililiwa na kuwekezwa kwenye makabila tawala ya wakikuyu,wajaluo na wakalenjin.Sasa leo unapotangaza sera ya kushinda ya counties hao waliokuwa maginalized kwa miaka watatokea dirisha lipi kimaendeleo sababu hawana hata pa kuanzia.Hawana Capital ya kuanzia kama wenzao waliolimbikiza viwanda,vitega uchumi,miundo mbinu mizuri kwenye maeneo yao kwa miaka nenda rudi
 
Last edited by a moderator:
bona

Demokrasia ni utawala wa walio wengi sio wachache wenye digrii tu.

Msimamo wa CCM ni kuwa Katika nchi kila mtu ana haki ya kupiga kura lakini pia ana haki ya kupigiwa kura awe na digrii au asiwe nayo.Huwezi kuwa na nchi ambayo kuna watu ambao kazi yao ni kupigia kura wengine tu lakini wao hawana haki ya kupigiwa kura kwa kisingizio cha digrii hiyo itakuwa si demokrasia ni Demokrasia after all mbona Mbowe mwenyekiti wa CHADEMA hana digrii lakini anaongoza maprofessor kibao wengine hata kawafukuza akina professor Mkumbo.
 
Last edited by a moderator:
East African Eagle
Ninazungumzia ufanisi wake katika kuleta maendeleo na uwajibikaji. na pia point ya msingi ni ule uwezo wa mwananchi kuchagua kiongozi wake badala ya kuletewa mtu toka dar. mtu wa kuchaguliwa huwajibika na kuwa na uchungu wa maendeleo kuliko wa kuteuliwa.

Pia suala la kuwa na viongozi wa kabila moja kwenye eneo kuna ubaya gani? ukienda ludewa utakuta mbunge mpangwa, madiwani wapangwa na mwenyekiti wa halmashauri mpangwa.
 
Last edited by a moderator:
East African Eagle
Ukiondoa majimbo ya mijini, majimbo mengi ya vijijini hapa Tanzania wabunge wanaochaguliwa ni wazawa wa hapo na hasa kabila la hapo. Sioni ajabu Gavana na Naibu Gavana wakachaguliwa kwa kuwa ni wazawa au wenye kabila la pale wanapogombea.
 
Last edited by a moderator:
Red Giant

Si makabila yote yanapenda maendeleo wapangwa wakiwemo ndio maana hakuna maendeleo ya maana kule hata nyumba za kuishi za maana hamna .Kuna makabila yanabidi yasaidiwe kwa kupelekewa wapenda maendeleo toka maeneo mengine kama wakuu wa mikoa,wilaya n.k kuwasaidia.

Hivi unasema watindiga wachague mkuu wa mkoa mtindiga,wa wilaya mtindiga watatoka kimaendeleo kweli?

UKiweka mkuu wa mkoa atoke kabila ya mpiga ngoma ya sindimba,mkuu wa wilaya mcheza sindimba,governor mnengua kiuno ngoma ya sindimba hilo kabila kutoka itachukua muda sababu ngoma ya sindimba ikilia tu wote wanatoka ofisini wanaenda kucheza sindimba.

Sisi tuna kitu kinaitwa madaraka mikoani ambako mikoa husika yenyewe hupanga mambo yao na vipaumbele vyao vikisimamiwa na madiwani wabunge wao n.k
 
Last edited by a moderator:
East African Eagle
Inawezekana hujaujua huu mfumo vizuri. serikali hugawa pesa kwenye counties kwa kuangalia idadi ya watu, eneo na umasikini nk. mfumo tulio nao ni wakinyonyaji sana kuliko wa counties. sisi pesa zinapelekwa kwenye mawilaya kisiasa kama hisani wakati wenzetu mgawanyo upo kisheria.

Tanzania ya leo kuna maeneo yanahuduma bora sana kuliko zingine, mawaziri hupendelea kwao. kwenye mfumo wa kenya hakuna ujinga huo.
 
Last edited by a moderator:
Red Giant

 
Last edited by a moderator:
East African Eagle

Kumbe umefungwa na ccm unashindwa kutoka kwenye hilo sanduku. Hapo naona unavuta hisia za Cheyo na mfumo wa majimbo. Nimekusoma, wewe hapo umeisha jikita mpaja ccm yenyewe ikupe uelekeo tofauti.
 
Last edited by a moderator:
Red Giant

Naujua vizuri nikupe tatizo lake nichukue vipengele toka katiba yao

1.Kuna kipengele chao katika katiba kinasema "Sharing the burden of taxation fairly" ina maana county yako kama kwenye kuchangia kodi uko chini mgao wako wa bajeti utakuwa chini.Sasa fikiria kule kwa wapangwa au watindiga kodi yao haiwezi linganishwa na kilimanjaro,arusha au dar kwa hiyo kiasilimia chao cha mchango wa kodi ndicho kitaamua wapewe vipi.

2.Kuna swala la mikopo .Pesa ikikopwa mfano ya barabara kutoka mfano benki ya dunia kwenda kwa watindiga au wapangwa deni hilo linabidi lilipwe na county husika sababu wafaidikaje wakubwa na hilo barabara ni huko inakoenda hivyo huwezi sukuma hilo deni likalipwe na mchaga wa kilimanjaro.Maana yake ni kuwa county zenye nguvu kiuchumi ndizo zaweza himili hilo zile zilizochoka zitaendelea kuchoka sababu hakuna county itakubali kulipa madeni ya county ingine.

3.Recurrent expenditure shall not exceed the county government's total revenue.
Kipengele hiki ukikiangalia ni kwa county zile tu zenye uwezo.County chovu kama kwa wapangwa na watindiga ni vigumu kuendelea.Hawana mapato ya ndani ya kutosha kusukuma maendeleo wanahitaji wasaidiwe kutoka county zingine kitu ambacho si rahisi chini ya mfumo wa county.Unavaa suruali kwa saizi ya kitambaa chako.Hii itafanya county zilizo nyuma zibaki nyuma forever.
 
Last edited by a moderator:
East African Eagle
Ludewa iko nyuma kwasababu mfumo wa sasa hauna utaratibu mzuri wa kugawa na kutumia pesa za nchi. Madaraka mikoani ni fix tu. haikua kazi ya rais kupita kila wilaya kuahidi kujenga vituo vya afya na masoko. hiyo ingekuwa kazi ya magavana.
 
Last edited by a moderator:
East African Eagle

Hayo maendeleo yaliyoletwa na ccm kwa takribani miaka 50+ yako wapi kwa hao watindiga? Tuwe wakweli, waTZ tumetapakaa nchi nzima na huo ubaguzi wa kikabila unaousema hapa TZ hauko kama ilivyo Kenya.

Tunataka maendeleo ya wananchi na sio maendeleo ya viongozi wa chama tawala. Usiwatukane wananchi na kuwaona hawawezi kufanya maamuzi ya maendeleo yao, wewe una fikra za kikoloni.

Kwani wewe ulizaliwa kwenye magorofa ya manzese, unaonaje baada ya kusoma na kuelimika ukarudi kuwa kiongozi kwenu, kwa watindiga, ili uwaletee naendeleo. Umeng'ania kwa wazaramo tu na unataka uendelee kukusanya napato centrally na kuyatafuna kifisadi.

Shame on you East African Eagle.
 
Last edited by a moderator:
Ila ukweli unabaki palepale kuwa demerit ya huo mfuno ni kukua kwa ukabila kenya. Umimi utakuwa kwa kasi ya ajabu vilevile. Kumbuka Kenya tayari ina ugonjwa wa ukabila. Munira Almasi
 
Last edited by a moderator:
East African Eagle
Kumbuka pia kuna pesa unaongezewa sababu ya kuwa maskini. counties maskini huongezewa mgao. hiyo point ya kwanza sidhani iko kama ulivyiweka japo sioni tatizo.

Kumbuka counties huwa na mapato ya ndani.hapo ndiyo huzidiana mapato. kwa hiyo unataka kuniambia mfumo huu ni mzuri na maendeleo ya ludewa na arusha hayapishani?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…