Nimefuatilia comments nyingi hapa halafu naona kuna upotoshaji wa kiaina. Ifahamike ugatuzi ama devolution ni mfumo ambao umetusaidia Wakenya pakubwa sana, ndio kupunguza ukabila ni mojawapo, lakini pia ikumbukwe ukabila ulianza kwa ajili ya kutogawana keki ya taifa kwa uhaki na usawa. Sasa imekua virahisi kwa kila jimbo kujiamulia mambo yake.
Kuna points kadhaa nitazielezea hapa.
- Kwa uwepo wa kabila moja kuanzia gavana hadi MCA ndani ya jimbo fulani hayo sio maajabu maana inategemea na mkoa ni upi na wenyeji wake. Kuna jimbo zenye wakaazi wa kabila moja tu. Hivyo hivyo kuna majimbo ya mjini ambapo makabila yamechanganyikana, kwa mfano Nairobi, Mombasa n.k. Utakuta hata viongozi wametoka makabila mbambali.
- Kwa sisi kujichagulia serikali zetu kwenye majimbo yetu ni jambo bora sana, maana tunayemchagua anakua mtu ambaye amedhihirisha uelewa wake wa maswala ya jimbo husika. Sasa yeye anakua na msaidizi wake na pamoja wanajenga serikali yao ya hilo jimbo na budget yao. Maamuzi yanafanyika humo humo nini cha kujegwa, iwe barabara, hospitali n.k. Sio vile ilivyokua hapo awali maamuzi yafanyika Nairobi halafu sie tunabaki kuona wanakandarasi wanatoka huko na kuanza kujenga vitu ambavyo hata hatuna umuhimu navyo.
- Yaani hali ilikua mbele hapo awali hadi kuna watu ukiwatembelea kwao wanakuuliza vipi habari za huko Kenya, wakati wao wapo Kenya. Sasa kila mtu anajihisi kuwa Mkenya ndani ya nchi yake maana katika kila jimbo watu wana uwezo wa kufuatlia mambo yanayowahusu. Wanachokifanya watu wa jimbo la Homa Bay hakinihusu kama mimi ni mkaazi wa jimbo la Nakuru. Sisi tunafanya yetu, na kila jimbo lipo mbioni kuwavutia wawekezaji kutoka majimbo mengine. Awali wawekezaji walikua wanafukuzwa kwa misingi ya kikabila, lakini sasa kwa vile kila jimbo lina asilimia fulani kutoka kwa mapato yake, basi inakua lazima kama gavana uhakikishe unakua na jinsi na mbinu za kuhakikisha jimbo lako linazalisha ili kiasi cha hela kitakachobaki kwako kiwe kingi.
- Kwa kweli huu mfumo ni muhimu sana kwa kila nchi, haswa nchi kama Tanzania iliyokubwa. Kuna changamoto kadhaa tunazokumbana nazo, lakini pamoja na hayo yote kuna tofauti kubwa na nzuri ukilinganisha na hapo awali.