Mfumo wa counties wa Kenya ni mzuri sana

Ila ukweli unabaki palepale kuwa demerit ya huo mfuno ni kukua kwa ukabila kenya. Umimi utakuwa kwa kasi ya ajabu vilevile. Kumbuka Kenya tayari ina ugonjwa wa ukabila.
hebu sema ni vipi huu mfumo utaleta ukabila?. mifumo kama yetu ndiyo huleta ukabila maana hata vitu vidogo maamuzi hutoka serikali kuu na baadhi ya watu hutumia hiyo chansi kurekebisha kwao na makabila yao.
 
East African Eagle

Nadhani hapo kila county inakuwa imejiwekea malengo kulingana na hali halisi ya ukusanyaji wa mapato hivyo hata alocation ya resources za taifa inazingatia percentage ambayo umechangia na si quantity.

Mfano Mwanza walipewa lengo la makusanyo Bilion 10 alafu Ruvuma bilioni 2 kutokana na fursa za kiuchumi zilizopo maeneo husiko, alafu kwenye makusanyo Mwanza wakakusanya bilion 4 ambayo ni 40% na Ruvuma wakakusanya bilioni 1.5 ambayo ni 75%, kwa uwingi Mwanza wamekusanya nyingi lakini kimahesabu Ruvuma wamejitahidi kukusanya hivyo hata huko kwa watindiga nadhani vigezo vitatumika kwa style hii.
 
Last edited by a moderator:
East African Eagle

Katika Tanzania hakuna Mkoa ambao unakabila moja, hao watindiga mbona ni sehemu ndogo sana ya mikoa husika ?

Kuna haja gani ya mfumo kama wa sasa wa Tz unaomfanya aliyembele asimame na aliyenyuma hasongi? Mikoa kama Arusha , Kilimanjaro ingekuwa mbali sana kama ingekuwa inajipangia mambo yake ila sasa tunatakiwa tunachopata chote kiende Magogoni kuibiwa. Tunabaki kusema sungura mdogo
 
Last edited by a moderator:
Nimefuatilia comments nyingi hapa halafu naona kuna upotoshaji wa kiaina. Ifahamike ugatuzi ama devolution ni mfumo ambao umetusaidia Wakenya pakubwa sana, ndio kupunguza ukabila ni mojawapo, lakini pia ikumbukwe ukabila ulianza kwa ajili ya kutogawana keki ya taifa kwa uhaki na usawa. Sasa imekua virahisi kwa kila jimbo kujiamulia mambo yake.

Kuna points kadhaa nitazielezea hapa.
- Kwa uwepo wa kabila moja kuanzia gavana hadi MCA ndani ya jimbo fulani hayo sio maajabu maana inategemea na mkoa ni upi na wenyeji wake. Kuna jimbo zenye wakaazi wa kabila moja tu. Hivyo hivyo kuna majimbo ya mjini ambapo makabila yamechanganyikana, kwa mfano Nairobi, Mombasa n.k. Utakuta hata viongozi wametoka makabila mbambali.

- Kwa sisi kujichagulia serikali zetu kwenye majimbo yetu ni jambo bora sana, maana tunayemchagua anakua mtu ambaye amedhihirisha uelewa wake wa maswala ya jimbo husika. Sasa yeye anakua na msaidizi wake na pamoja wanajenga serikali yao ya hilo jimbo na budget yao. Maamuzi yanafanyika humo humo nini cha kujegwa, iwe barabara, hospitali n.k. Sio vile ilivyokua hapo awali maamuzi yafanyika Nairobi halafu sie tunabaki kuona wanakandarasi wanatoka huko na kuanza kujenga vitu ambavyo hata hatuna umuhimu navyo.

- Yaani hali ilikua mbele hapo awali hadi kuna watu ukiwatembelea kwao wanakuuliza vipi habari za huko Kenya, wakati wao wapo Kenya. Sasa kila mtu anajihisi kuwa Mkenya ndani ya nchi yake maana katika kila jimbo watu wana uwezo wa kufuatlia mambo yanayowahusu. Wanachokifanya watu wa jimbo la Homa Bay hakinihusu kama mimi ni mkaazi wa jimbo la Nakuru. Sisi tunafanya yetu, na kila jimbo lipo mbioni kuwavutia wawekezaji kutoka majimbo mengine. Awali wawekezaji walikua wanafukuzwa kwa misingi ya kikabila, lakini sasa kwa vile kila jimbo lina asilimia fulani kutoka kwa mapato yake, basi inakua lazima kama gavana uhakikishe unakua na jinsi na mbinu za kuhakikisha jimbo lako linazalisha ili kiasi cha hela kitakachobaki kwako kiwe kingi.

- Kwa kweli huu mfumo ni muhimu sana kwa kila nchi, haswa nchi kama Tanzania iliyokubwa. Kuna changamoto kadhaa tunazokumbana nazo, lakini pamoja na hayo yote kuna tofauti kubwa na nzuri ukilinganisha na hapo awali.
 
East African Eagle

If they got it wrong doesn't mean we can't do it right! Ni kweli devolution Kenya to a great extent ilikuwa kudiffuse tribal tensions, na kidogo unaonekana umesucceed. Mipaka ya majimbo yao ilichorwa kwa kuzingatia tribal lines.

Lakini huku Tanzania hatuna hilo. Kwanza mikoa yetu ni kama 30 tu, yet makabila huku ni around 120! (Kenya makabila inasemekana ni 40 na county ni 48). Huku mipaka ya mikoa haijazingatia sana makabila.
 
Last edited by a moderator:
Hlio liko kwenye makaratasi tu ni mazungumzo baada ya habari.Limeandikwa kuwa linategemea uwezo kama utakuwepo!!!!!!!

Sio kwenye makaratasi tu acha kupotosha watu. Kuna kitu kinaitwa vertical apportionment kwenye katiba ya Kenya, na hili husimamiwa na Revenue Allocations Commission (RAC) pamoja na Seneti.
Formula iliyopendekezwa na RAC ya kugawana fedha kutoka kwa serikali kuu baina ya majimbo ilikuwa izingatie vitu vifuatavyo
1. Ukubwa wa jimbo lenyewe. Majimbo makubwa kijiografia hupata mgao mkubwa zaidi.
2. Idadi ya watu wanaokaa katika jimbo hilo. Majimbo yenye watu wengi hupata mgao mkubwa zaidi.
3. Basic equal share - hii kila jimbo hupata kiasi sawa bila kuzingatia chochote kile.
4. Level ya umasikini katika jimbo husika. Majimbo masikini hupata mgao mkubwa kuliko yale tajiri.
5. Financial discipline - hii ilikuwa ni kama zawadi kwa yale majimbo yenye discipline ya kutumia fedha.
Majimbo ya Kenya yamekuwa yakipata mgao huu tangu katiba yao mpya ipitishwe na kuadoptiwa.
 
East African Eagle

Jabulani na MK254 wamekujibu vizuri sana. Sijui kwa nini unasisitiza kuitazama Kenya kwa kila kitu kupitia lens ya ukabila.

Kulikuwa na mikoa nane Kenya ambayo ilikuwa imewekwa pamoja na Wakoloni kwa misingi ya kikabila tukasema tuweke gatuzi 47 ambayo itafocus kwa maendeleo.

Mtu ambaye yuko Nairobi hatawaikujua priority za watu wa Turkana hata akuwe mzuri kiasi gani katika kutumia pesa kufanya maendeleo.

Halafu kuna mgao wa mapato na hakuna hiyo mambo ya tax burden kama ulivyoitaja hapo kwa hiyo context.
 
Last edited by a moderator:
What Msemakweli is saying is true.The formula used in deciding what a county(jimbo) gets takes into account the poverty levels.

Those that have a high poverty index get more on that account alone.Of course the formula has other variables such as population size,land mass size and others.
 

Cc East African Eagle
CCM minds! SMH!
 
Last edited by a moderator:
IAfrika

Mimi huwa najiuliza watumishi wa serekali huwa wanapelekwa Swaziland kujifunza nini au Ulaya kufanya nini kabla ya kujifunza kwanza kwa Jirani?
Rais Kibaki alipokuja kuaga alisema wazi tatizo letu wa Tz hatupendi kutembea kujifunza kwa jirani tunapenda kwenda tu Pwani
 
Last edited by a moderator:
Umeandika uongo.Katizame Kenya county budget allocation ya mwaka uliopita na miaka ya nyuma.Ulichoandika si kweli.
soma hata hapa tu
Nairobi to get highest allocation from counties' budget - Politics and policy - businessdailyafrica.com

Huu ushabiki wako ukichanganya na uwongo sielewi ni kwa nini, yaani vipi unalipwa ama nini. Mbona unakazana kuwandanganya Watanzania wenzio, huu ni mjadala tu na hauwezi ukabadilisha katiba yenu kwa sasa, hivyo hamna haja ung'ang'ane na ushabiki ule wenu wa vyama.

Jimbo la Turkana linafahamika kama maskini wa kutupwa, ndiko huwa watu wengi hufa kwa njaa na majanga mengine, lakini ukiangalia kwenye formula ya mgao baada ya ugatuzi utaona ndilo linaongoza likifuata Nairobi. Fuatlia hii taarifa hapa

Nairobi and Turkana will receive the largest share of the Sh253 billion to be given to counties in the next financial year, which starts on July 1.

The total amount to be given to the 47 counties will, however, increase to Sh274 billion, when conditional grants for key projects and money for the equalisation fund are factored into the allocations.

This will be the third time the two counties will be bagging the highest share of allocation since the launch of devolution after the 2013 General Election.

Nairobi and Turkana to get biggest share of county cash from July - Politics - nation.co.ke

 
MK254

NAIROBI ni maskini wa kutupwa hadi apate mgao mkubwa kuliko counties zingine? NIMEOMBA MNIPE DATA ZA KILA COUNTY ILICHOPATA MNANILETEA HABARI ZA MAGAZETINI.
 
Last edited by a moderator:
East African Eagle

Nimekupa mfano wa Turkana sio Nairobi, fahamu sio umaskini tu unaotumika, kuna vigezo vingine pia. Jimbo la Nairobi ndilo linaongoza kwa wingi wa watu.

Jimbo la Turkana ndio linaongoza kwa umaskini, poverty index halafu lina watu wengi yaani laki nane.

Fuatilia huu mgao.

Population 45%
Poverty Index 20%
Land Area 8%
Basic Equal Share 25%
Fiscal Responsibility 2%
 
Last edited by a moderator:
i have no time or motivation to spoon feed you with data.Just do your own leg work.this info is publicly available here in Kenya

LYING NEEDS DATA ALSO.Anyway if you don`t want to provide data to prove your lies then I will remain with my stand that you are a liar.
 
LYING NEEDS DATA ALSO.Anyway if you don`t want to provide data to prove your lies then I will remain with my stand that you are a liar.


Which other data are you insisting on, wacha kusumbua watu na uongo wako, I've provided you with information but you still want to be fed deep your throat.


Turkana which was allocated more funs than any other county, second to Nairobi has the following data
- Is the most poor county with a poverty rate of 92%
- Has a population of more than 855,399
- And the size of 71,597.8 sq km in area


Nairobi which was allocated more than all contains the following
- Poverty index of 21.8%
- Has a population of more than 3,138,369
- And the size of 694.9 sq km in area


Now do the maths following the model below
Population 45%
Poverty Index 20%
Land Area 8%
Basic Equal Share 25%
Fiscal Responsibility 2%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…