Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
Wataalamu wa sekta ya ardhi mkoani Mtwara wakiendelea kupata mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa e-Ardhi katika Ukumbi wa Chuo cha Stella Maris, Mtwara, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita kuboresha na kurahisisha upatikanaji wa huduma za ardhi kwa wananchi.
Kupitia mfumo huo, huduma mbalimbali ikiwemo utoaji Hati Milki za Ardhi zinaendelea kutolewa hatua inayolenga kusogeza huduma karibu na wananchi na kupunguza changamoto zinazohusiana na upatikanaji wa huduma za ardhi.