Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
★Wizara yaweka lengo la kufikisha mfumo huo katika mikoa yote ifikapo 2027
Serikali imeongeza kasi ya matumizi ya mfumo wa kidijiti wa e-Ardhi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za ardhi na hati miliki, huku ikilenga kuufikisha mfumo huo katika mikoa yote nchini ifikapo mwaka 2027.
Akizungumza kwenye banda la Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa Lindi wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya Madini, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, amesema matumizi ya mfumo huo yatasaidia kufunga mianya ya dhuluma na kero zinazochangiwa na uwepo wa watu wa kati maarufu kama ‘vishoka’.
Mmuya amesema hadi sasa mfumo wa e-Ardhi utaanza kutumika katika mikoa 16 mwishoni mwa Mwezi Oktoba mwaka huu, ambapo amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kutumia teknolojia kuboresha huduma za sekta ya ardhi na kurahisisha upatikanaji wa hati miliki za viwanja na mashamba kwa wananchi.
Katika hatua nyingine, Mmuya amewataka wataalamu na maafisa ardhi kote nchini kutumia majukwaa yenye mikusanyiko ya wananchi kutoa elimu na huduma za sekta hiyo, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha ardhi yote nchini inapangwa, inapimwa na kumilikishwa.
Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Lindi, Bwn. Geofrey Mugisha, amesema mkoa huo unatarajia kuanza rasmi kutumia mfumo wa e-Ardhi mwezi Oktoba mwaka huu.
Amesema kwa mwaka wa fedha 2026/27 mkoa wa Lindi unalenga kuandaa hati miliki 2,400, huku hati takribani 680 zikiwa tayari zimeandaliwa.