shadrack lutengano
New Member
- Jul 13, 2023
- 2
- 2
Elimu ni utaratibu unaotumika kurithishana ujuzi kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine ambappo mfumo huu unaweza kuwa rasmi mfano ile elimu inayotolewa katika taasisi mbalimbali za elimu kama shule za msingi, sekondari na chou pia mfumo unaweza usiwe rasmi ambapo mtu anapata ujuzi kutoka kwa watu wanao mzunguka bila ya kukaa darasani mfano mtu huweza kujifunza namna ya kuendesha biashara kutoka kwa mtu ambae amefanya biashara kwa mude mrefu.
Mifumo hii miwili ya elimu (rasmi na isiyo rasmi) yote imeonekana kuwa na mchango mkubwa katika Maisha ya jamii na kila mfumo ukiwa bora mahali Fulani na mwingine kuwa bora mahali Fulani, hivyo mtu ambae anakua amefanikiwa kupata elimu hizi zote mbili anakuwa na uwezo mkubwa wa kukabiriana na chagamoto mbalimbali za Maisha ukilinganisha na yule ambaye anakua amepata aina moja ya elimu katika hii mifumo miwili.
Katika jamii nyingi za kiafrika hasa Tanzania tumefanikiwa katika elimu isiyo rasmi bali tumeonekana tukiwa nyuma katika mfumo rasmi wa kielimu ndomaana imekua kawaida mtu kuwa na elimu ya chuo kikuu na kurudi mtaani akiwa sawa na mtu ambae hajapata kabisa elmu hyo na elimu isiyo rasmi imeonekana kuwa ndo elimu bora kuliko hii rasmi ihali yakwamba tulitegemea hii elimu rasmi ambayo inamuhitaji mwanafunzi kuigharamia ndo iwe bora kuliko hii elimu isiyo rasmi ambayo maranyingi hutolewa bure. Sasa ni sehemu gani tumeshindwa kuweka sawa katika elimu rasmi.
1). Mitaala ya elimu inayolenga kumuaandaa mwanafunzi kujibu mitihani nasio kukabiliana na chanamoto mbalimbali za Maisha,mfumo wa elimu ya Tanzania umekua ukilenga Zaidi kumuandaa mwanafunzi kuwa na uwezo wa kujibu mitihani na sio kukabiliana na mambo mbalimbali yanayotokea katika jamii na ndiomaana hata mitihani yetu imejikita Zaidi kumpima mwanafunzi nikitugani amekariri nasio ameelewa nini,hili linaweza kuoneknana la kawaida lakini mfumo huu humfanya mwanafunzi kutokuwa mbunifu kwasababu tayari anakua anaaminishwa kuwa kwenye kila tatizo atakalokutana nalo basi kuna namna moja tu ambayo ni sahihi ya kukabiliana na hilo tatizo ambapo katika Maisha ya kawaida tatizo linaweza likawa lilelile lakini sio lazima njia ya kulitatua iwe moja,kitu hiki kinaonekana Dhahiri kwa wasomi wetu ambapo wengi wanakosa kabisa ubunifu juu ya mambo mbalimbali katika jamii kwakua elimu imesha mkaririrsha kuwa kama hiki kitu kipo hivi basi itakua hivyo milele hakiitaji Kwenda tofauti na kilivyo.nini kifanyike?
Mitaala ya elimu iandaliwe katika namna ambayo itamuwezesha mwanafunzi kuwa na ubunifu zaidi na kuachana na kukariri kile anachofundishwa ili kile anachokipata shuleni kimsaidie katika Maisha yake na kusadia wengine katika jamii inayo mzunguka mfano mtaala uwe unampa mwanafunzi uhuru wa kuelezea kile anachohisi yeye amekielewa katika somo husika au mada husika ambayo itakua imeulizwa kwenye mtihani nasio kuishia tuu kwenye majibu ambayo yatakua yameandaliwa na mwalimu husika, hii itasaidia kugundua uelewa wa wanafunzi juu ya mambo wanayofundishwa.
2). Elimu imekuwa na masomo mengi na ambayo hayana uhusiano,mfumo wa elimu ya Tanzania inamrazimisha mwanafunzi kusoma masomo mengi katika kpindi chake cha uanafunzi ambapo mengi ya masomo hayo yamekua hayana uhusiano wa moja kwa moja hii inamfanya mwanafunzi kutokua uelewa mkubwa juu ya vitu anavyofundishwa ukilinganisha na angekua na masomo machache mfano baada ya elimu ya msingi mwanafunzi angekuwa anapewa fursa ya kusoma masomo ambayo yangekuwa na tija kwakwe kulingana na kile anachokiona kuwa ni sahihi kwake na kinaendana na malengo yake ya baadae hivyo kumsaidia kuwa kwenye ramani ya ile sehemu atakayokuwa akiifanyia kazi katika kipindi chote cha Maisha yake iwe ameajiliwa au amejiajili.
3). Elimu rasmi imekua na mlolongo mrefu,kuna haja ya kuifanya elimu ya Tanzania iwe fupi hasa kutoka shule ya msingi hadi shule za sekondari ambapo mwanafuzi amekua akitumia muda mwingi sana katika hizi hatua mbili kabla ya kufikia chou ambapo uko ndo angalau mwanafunzi anakua anapatiwa ile elimu ianyoendana na kile atakachoenda kukifanya mtaani ingawa sio kwa kiwango kikubwa kwasababu hata elimu ya chuo bado imekua ni ya nadharia sana kuliko vitedo kama zile elimu za chini,kufupishwa kwa elimu kutasaidia kumpa mwanafunzi muda wingi katika Maisha yake kujifunza mambo mengine mengi nje ya elimu ya darasani katika umri mdogo nikimanisha anapofikia umri wa kuitwa mtu mzima(miaka 18) anakuwa tayari yupo nje ya shule rasmi anakua tayari kupata ile elimu isiyo rasmi ya mtaani ambapo kwetu imekua si hajabu kuona kijana wa mikana 23 bado yupo katika elimu rasmi ambapo inamfanya anatumia muda mwingi Zaidi wa Maisha yake kijifunza elimu ya darasani ambayo tumesema toka mwanzo inamadhaifu mengi ikiwa ni Pamoja na kutompa mwanafunzi kile anchostahiri ili aweze kuyaendesha Maisha yake.
4). Elimu rasmi imekua ni ya nadharia sana kuliko vitendo,elimu ya nadharia ni elimu ambayo imepitwa sana na wakati hasa katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia unahitaji mwanafunzi afundishwe kwa vitendo ili aweze kuwa mbunifu na kuendana na niwakati sahihi wa serikali yetu kulitazama hili kwa namna ya kipekee na kuamua kuweka bajeti katika elimu itakayoweza kumfanya mwanafunzi awe ni wa vitendo Zaidi ambapo itamsaidia kutofikria sana kuhusu ajira kwasababu atakua na ujuzi ambao utamsaidia kuyaendesha Maisha yake ata akiwa nje ya ajira.
Kwa ujumla ili mwanafunzi aweze kumaliza elimu yake na awe na uwezo wa kuendesha shughuri zake na kuleta mabadiriko chanya anapaswa apate hizi elimu zote mbili ambapo mfumo wa elimu rasmi uwe unamuwezesha mwanafunzi kuwa na muda wa kupata ile elimu isiyo rasmi
Pia elimu rasmi imuwezeshe mwanafunzi kuwa na uwezo wa kuvifanya kwa vitendo vile vitu anavyovisoma kwa nadharia akiwa darasa

Upvote
1