Mfumo wa kimataifa wa mambo ya kifedha wakosolewa na nchi za Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
美国激进加息.jpg
Mkutano wa kilele wa katikati ya mwaka wa Umoja wa Afrika ulifanyika hivi karibuni mjini Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Viongozi wa nchi za Afrika walioshiriki kwenye mkutano huo kwa mara nyingine tena walitoa wito wa mageuzi ya mfumo wa kimataifa wa mambo ya kifedha.

Rais William Ruto wa Kenya aliungana na viongozi wengine wa Afrika katika kutoa wito wa mageuzi ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa. Rais Ruto alisema, mfumo wa kimataifa wa mambo ya kifedha sio wa haki kwa nchi za Afrika, ambazo zinabeba riba kubwa ya mara nane kuliko nchi tajiri zinapokopa fedha kutoka kwenye mashirika ya kimataifa.

Alisisitiza kuwa, sio kwamba nchi za Afrika zinaomba takrima, bali zinataka tu haki na usawa katika mfumo wa kimataifa.

Hii ni mara ya pili ndani ya muda mfupi kwa nchi za Afrika kutoa kauli kama hiyo. Katika Mkutano wa Kilele wa Makubaliano Mapya ya Kifedha uliofanyika mjini Paris mwishoni mwa mwezi uliopita, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini alisisitiza kuwa “Nchi za Afrika si ombaomba, kilicho muhimu ni haki sawa miongoni mwa nchi mbalimbali duniani. Na sasa ni wakati wa nchi za Afrika kushiriki katika mashirika ya kimataifa na majukwaa ya ushirikiano wa kiuchumi wa kimataifa kama washirika sawa.”

Mfumo wa Bretton Woods ulioanzishwa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia unaonyesha hasa muundo wa nguvu za kisiasa na kiuchumi wa karibu miaka 80 iliyopita. Wakati Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa zilipoanzishwa, zaidi ya robo tatu ya nchi duniani, haswa nchi za Afrika hazikuwepo.

Matokeo ya hali hii ni kwamba, utaratibu na kanuni za mfumo huo vimetungwa na nchi zilizoendelea, ambazo mara kwa mara zinapuuza maslahi ya nchi zinazoendelea kwa makusudi au bila kukusudia, na pia ni kinyume kabisa na haki na usawa.

Kati ya dola bilioni 650 za haki maalum za kukopa zilizotolewa na IMF mwaka 2021, dola bilioni 160 zilikwenda kwa nchi za Umoja wa Ulaya, huku nchi za Afrika zikipata dola bilioni 34 tu. Kulingana na idadi ya watu, mtu kutoka nchi tajiri za Umoja wa Ulaya alipata fedha karibu mara 13 kuliko mtu wa nchi maskini za Afrika.

Zaidi ya hayo, nchi za Afrika zinalazimika kubeba gharama za kukopa ambazo ni mara 4 hadi 8 zaidi kuliko nchi zilizoendelea. Aidha, mfumo wa fedha wa kimataifa unaozingatia dola ya Marekani umezifanya nchi za Afrika ziwe na hali mbaya zaidi zinapokabiliwa na changamoto.

Tangu mwaka mmoja uliopita, Marekani imeongeza viwango vya riba kwa kasi, na matokeo yake ni kwamba, nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kushuka kwa thamani ya sarafu zao, mfumuko wa bei, matatizo ya madeni na kuzorota kwa uchumi.

Hivi sasa, Afrika inahitaji fedha zaidi kwa dharura ili kukabiliana na changamoto hizo na kufikia malengo ya maendeleo. Hata hivyo, chini ya mfumo uliopo wa fedha wa kimataifa, kutokana na utaratibu usio wa haki uliotungwa na nchi za Magharibi, ni vigumu kwa nchi zinazoendelea, zikiwemo nchi za Afrika, kuhakikisha mazingira ya kifedha ya ndani na nje, na maendeleo ya jamii na uchumi katika nchi hizo yanaathiriwa vibaya.

Ni wakati wa kufikiria kujenga upya mfumo wa fedha duniani unaolingana mahitaji ya nchi zote katika karne mpya.
 
Sisi waAfrika tumewekeza mtaji kiasi gani kwenye huo mfumo ? Unao tupa haki ya kudai haki sawa?
 
Hizo ni ndoto za alinacha fu, kama kila mwaka ripoti ya CAG ni ufisadi mtupu na hakuna kabisa hatua zinazochukuliwa dhidi ya hao mafisadi sasa Afrika ina miujiza gani ya kujikwamua. Sisi tubaki tu kukimbizana na mwenge maanake ndio akili yetu ilipofikia. Bure kabisa.
 
View attachment 2693879Mkutano wa kilele wa katikati ya mwaka wa Umoja wa Afrika ulifanyika hivi karibuni mjini Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Viongozi wa nchi za Afrika walioshiriki kwenye mkutano huo kwa mara nyingine tena walitoa wito wa mageuzi ya mfumo wa kimataifa wa mambo ya kifedha.

Rais William Ruto wa Kenya aliungana na viongozi wengine wa Afrika katika kutoa wito wa mageuzi ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa. Rais Ruto alisema, mfumo wa kimataifa wa mambo ya kifedha sio wa haki kwa nchi za Afrika, ambazo zinabeba riba kubwa ya mara nane kuliko nchi tajiri zinapokopa fedha kutoka kwenye mashirika ya kimataifa.

Alisisitiza kuwa, sio kwamba nchi za Afrika zinaomba takrima, bali zinataka tu haki na usawa katika mfumo wa kimataifa.

Hii ni mara ya pili ndani ya muda mfupi kwa nchi za Afrika kutoa kauli kama hiyo. Katika Mkutano wa Kilele wa Makubaliano Mapya ya Kifedha uliofanyika mjini Paris mwishoni mwa mwezi uliopita, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini alisisitiza kuwa “Nchi za Afrika si ombaomba, kilicho muhimu ni haki sawa miongoni mwa nchi mbalimbali duniani. Na sasa ni wakati wa nchi za Afrika kushiriki katika mashirika ya kimataifa na majukwaa ya ushirikiano wa kiuchumi wa kimataifa kama washirika sawa.”

Mfumo wa Bretton Woods ulioanzishwa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia unaonyesha hasa muundo wa nguvu za kisiasa na kiuchumi wa karibu miaka 80 iliyopita. Wakati Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa zilipoanzishwa, zaidi ya robo tatu ya nchi duniani, haswa nchi za Afrika hazikuwepo.

Matokeo ya hali hii ni kwamba, utaratibu na kanuni za mfumo huo vimetungwa na nchi zilizoendelea, ambazo mara kwa mara zinapuuza maslahi ya nchi zinazoendelea kwa makusudi au bila kukusudia, na pia ni kinyume kabisa na haki na usawa.

Kati ya dola bilioni 650 za haki maalum za kukopa zilizotolewa na IMF mwaka 2021, dola bilioni 160 zilikwenda kwa nchi za Umoja wa Ulaya, huku nchi za Afrika zikipata dola bilioni 34 tu. Kulingana na idadi ya watu, mtu kutoka nchi tajiri za Umoja wa Ulaya alipata fedha karibu mara 13 kuliko mtu wa nchi maskini za Afrika.

Zaidi ya hayo, nchi za Afrika zinalazimika kubeba gharama za kukopa ambazo ni mara 4 hadi 8 zaidi kuliko nchi zilizoendelea. Aidha, mfumo wa fedha wa kimataifa unaozingatia dola ya Marekani umezifanya nchi za Afrika ziwe na hali mbaya zaidi zinapokabiliwa na changamoto.

Tangu mwaka mmoja uliopita, Marekani imeongeza viwango vya riba kwa kasi, na matokeo yake ni kwamba, nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kushuka kwa thamani ya sarafu zao, mfumuko wa bei, matatizo ya madeni na kuzorota kwa uchumi.

Hivi sasa, Afrika inahitaji fedha zaidi kwa dharura ili kukabiliana na changamoto hizo na kufikia malengo ya maendeleo. Hata hivyo, chini ya mfumo uliopo wa fedha wa kimataifa, kutokana na utaratibu usio wa haki uliotungwa na nchi za Magharibi, ni vigumu kwa nchi zinazoendelea, zikiwemo nchi za Afrika, kuhakikisha mazingira ya kifedha ya ndani na nje, na maendeleo ya jamii na uchumi katika nchi hizo yanaathiriwa vibaya.

Ni wakati wa kufikiria kujenga upya mfumo wa fedha duniani unaolingana mahitaji ya nchi zote katika karne mpya.
Hao viongoz kazi kulalamika tu kwan kukopa walilazimishwa? viongozi wenyewe 99.9% mijizi na mifisadi ya kufa mtu! yaan wao ni kutafuta wa kuwaangushia majumba mabovu ilhali vyanzo ni wao wenyewe!
 
Back
Top Bottom