Mfumo wa majina katika Passport na ID za Tanzania unasababisha usumbufu sana nje ya Tanzania

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Wanajamii,

Unapoomba passport au ya ID, ni kawaida kuulizwa kwenye form Jina lako la Kwanza, la katikati na la Ukoo. Sasa Tatizo ni kwamba Passport au ID vikitolewa, kunakuwa hakuna utenganisho huu, bali Mambo ya Ndani na NIDA wanaamua kuunganisha jina lako la kwanza na la katikati kama jina lako la kwanza (given name).

Yaani, kama ulijaza form namna hii;

Jina la kwanza: Musa
Jina la katikati: Salum
Jina la Ukoo: Zengezenge

Passport au NIDA vitatoka Vikoonyesha hivi

Jina/Given name: Musa Salum
Jina la Mwisho: Zengezenge

Sasa mara kadhaa katika shughuli zako, nimekataliwa katakata kwamba mwenye jina sio mimi, baada ya kuandika jina langu la kwanza kama Musa, la la ukoo kama Zengezenge. Nikaambiwa mtu wanaemtaka jina lake la Kwanza ni Musa Salum. Nilijaribu kujiteteta lakini nikaambiwa system imenikataa!

Tatizo ni kwamba hata unapojaza form ambapo unatakiwa utoe forst name, middle name na surname, ni lazima uandike jina la kwanza kama majina mawili ili uendane na Passport au ID. Ukiandika moja unaambiwa huyu sio wewe. Sasa unajiuliza nikijaza jina la kwanza Musa Salum, jina la kati nijaze nini?

Na kumbuka mpangilio wa majina sasa unakuwa tofauti kwenye Passport /NIDA ID na kwenye cheti cha kuzaliwa.

Sasa hili ni jambo ambalo linapaswa kurekebishwa haraka. Kama Tanzania wanaona hakuna nafasi ya kuweka jina la kati kwenye Passport au ID basi wasiweke kabisa badala ya kuliunganisha na jina la kwanza na kufanya kila mtazania awe na majina mawili ya kwanza au given name.
 
Wewe ndio mwenye tatizo. Andika majina yako kama yalivyo kwenye documents zako kuepusha usumbufu.

Kama wanahitaji majina mawili na kitambulisho chako yako matatu, andika majina maawili mwanzoni.

e.g Jina la kwanza: Mussa Juma

Jina la pili: Kibindankoi
 
Kwa hiyo jina la kati nijitungie?

Halafu kumbuka cheti cha kuzaliwa kinaonyesha mpangilio tofauti, hakionyeshi jina langu ni Musa Salum bali Musa.
 
Kama wakihitaji jina la kati liandike.

Jina la kwanza: Mussa

Jina la kati: Juma

Jina la mwisho: Kibindankoi
Ndivyo nilivyofanya na kupata matatizo mara kadhaa, ikidaiwa jina langu la kwanza sio Musa bali Musa Salum
 
Kama vipi tumia majina mawili:

Jina la kwanza: Mussa

Jina la kati:

Jina la Mwisho: Juma kibindankoi
 
Sawa, huo ni ushauri kwa watu wanaoomba Passport na NIDA ID kwa sasa. Thread yangu inaeleza tatizo la watu ambao tayari tuna Passport na NIDA ID. Majina yamekoroganywa na hayaendani na vyeti vya kuzaliwa, na yanasababisha usumbufu
Kwa hapo cheti cha kuzaliwa ndio rahisi kupata, kama majina yako tofauti tafuta kingine chenye majina sahihi.
 
Kama vipi tumia majina mawili:

Jina la kwanza: Mussa

Jina la kati:

Jina la Mwisho: Juma kibindankoi
Naona huelewi, maana hapo ndio utaharibu kabisa. Ukiulizwa toa ushahidi kuwa jina lakoo la mwisho passport itaonyesha Kibindankoi, sasa ukikataliwa sijui utalalamikia nani?

Kwa nini unabisha kitu kiko wazi, uko Mambo ya Ndani nini? Mara nyingine ni rahisi kukiri kuwa ukihiyo umefanyika. Hawa watu watambue mfumo wa majina si kwa Tanzania tu, lazima uendane na system za kimataifa, first name should be first name, middle name should be middle name, and last name should be last name.
 
Siyo kila mtu ana majina mengi. Mimi mwenyewe natumia majina mawili.

Na kuna wazanzibar wana majina mpaka manne.

Unayaweka vipi kwa mfumo huo.
 
Hewaaa, itabidi jina la kwanza katika hali hiyo liwe na majina matatu!

Hivyo waambiwe wasije wakaandika majina mawili ya kati, itakula kwao. Utakuta mtu kwenye passport jina la kwanza limeandikwa Musa Abdallah Shaaban kwa kuwa jina la kati kwenye form aliandika Abdallah Shaaban. Sasa aikli hiyo hawa watu wa Mambo ya Ndani?!
 
Wanajamii,

Unapoomba passport au ya ID, ni kawaida kuulizwa kwenye form Jina lako la Kwanza, la katikati na la Ukoo. Sasa Tatizo ni kwamba Passport au ID vikitolewa, kunakuwa hakuna utenganisho huu, bali Mambo ya Ndani na NIDA wanaamua kuunganisha jina lako la kwanza na la katikati kama jina lako la kwanza (given name).

Yaani, kama ulijaza form namna hii;

Jina la kwanza: Musa
Jina la katikati: Salum
Jina la Ukoo: Zengezenge

Passport au NIDA vitatoka Vikoonyesha hivi

Jina/Given name: Musa Salum
Jina la Mwisho: Zengezenge

Sasa mara kadhaa katika shughuli zako, nimekataliwa katakata kwamba mwenye jina sio mimi, baada ya kuandika jina langu la kwanza kama Musa, la la ukoo kama Zengezenge. Nikaambiwa mtu wanaemtaka jina lake la Kwanza ni Musa Salum. Nilijaribu kujiteteta lakini nikaambiwa system imenikataa!

Tatizo ni kwamba hata unapojaza form ambapo unatakiwa utoe forst name, middle name na surname, ni lazima uandike jina la kwanza kama majina mawili ili uendane na Passport au ID. Ukiandika moja unaambiwa huyu sio wewe. Sasa unajiuliza nikijaza jina la kwanza Musa Salum, jina la kati nijaze nini?

Na kumbuka mpangilio wa majina sasa unakuwa tofauti kwenye Passport /NIDA ID na kwenye cheti cha kuzaliwa.

Sasa hili ni jambo ambalo linapaswa kurekebishwa haraka. Kama Tanzania wanaona hakuna nafasi ya kuweka jina la kati kwenye Passport au ID basi wasiweke kabisa badala ya kuliunganisha na jina la kwanza na kufanya kila mtazania awe na majina mawili ya kwanza au given name.
Usifuate unavyotaka wewe, fuata mfumo unavyotaka
 
Hewaaa, itabidi jina la kwanza katika hali hiyo liwe na majina matatu!

Hivyo waambiwe wasije wakaandika majina mawili ya kati, itakula kwao. Utakuta mtu kwenye passport jina la kwanza limeandikwa Musa Abdallah Shaaban kwa kuwa jina la kati kwenye form aliandika Abdallah Shaaban. Sasa aikli hiyo hawa watu wa Mambo ya Ndani?!
Mfano 👇👇

Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.

👆👆👆
Imagine, Hapo jina kwanza ni lipi, kati ni lipi na la mwisho ni lipi ?
 
Hivi kwa nini hizi taasisi zetu zenye watumishi wanaolipwa mamiljoni wanashindwa kusolve issue ndogo ndogo kama hizi
 
I see...mbona waelewa sana wale....au Ulikuwa Ukraine? Maana kwenye rushwa na wanakimbizana na Nigeria.
Mkuu, Ukraine haipo dunia ya kwanza, ni economy in transition, kama bado haijawa Thord World country!

Tatizo ni system zao, mara nyingine jina la kwanza linatakuwa kuwa captured kama one word

Kwa mfao Kama wewe ni Musa Salum, system inataka uandike Musa-Salum, ukiandika Musa Salum kama first name inasema error!

Sasa imagine jina la kwanza la Kabudi, Palamagamba-John-Aidan-Mwaluko

Ndio maana kuna wanawake wanaoolewa hawataki kunadili jina wanatumia jina la ukoo wake na mume wake kwa kuweka dash katikati

Utakuta anakuambia naitwa Rehema Rugemalila-Mwatumbeya
 
Back
Top Bottom