Mfumo wa majina katika Passport na ID za Tanzania unasababisha usumbufu sana nje ya Tanzania

Mfumo wa majina katika Passport na ID za Tanzania unasababisha usumbufu sana nje ya Tanzania

Kwa hiyo jina la kati nijitungie?

Halafu kumbuka cheti cha kuzaliwa kinaonyesha mpangilio tofauti, hakionyeshi jina langu ni Musa Salum bali Musa.
Kwani huko majuu au nchi zingine wana hitaji hicho cheti chako cha kuzaliwa , mpaka ukiunganishe hapa kwenye jambo lako la id, passport na system za wengine.
Hiyo nchi offisa wake atakuwa kenge fulani, kitu ambacho sikiamini kuwa hivyo
 
Mkuu, Ukraine haipo dunia ya kwanza, ni economy in transition, kama bado haijawa Thord World country!

Tatizo ni system zao, mara nyingine jina la kwanza linatakuwa kuwa captured kama one word

Kwa mfao Kama wewe ni Musa Salum, system inataka uandike Musa-Salum, ukiandika Musa Salum kama first name inasema error!

Sasa imagine jina la kwanza la Kabudi, Palamagamba-John-Aidan-Mwaluko

Ndio maana kuna wanawake wanaoolewa hawataki kunadili jina wanatumia jina la ukoo wake na mume wake kwa kuweka dash katikati

Utakuta anakuambia naitwa Rehema Rugemalila-Mwatumbeya
Mwatumbeya si ni mnyakyusa huyo
 
Wanajamii,

Unapoomba passport au ya ID, ni kawaida kuulizwa kwenye form Jina lako la Kwanza, la katikati na la Ukoo. Sasa Tatizo ni kwamba Passport au ID vikitolewa, kunakuwa hakuna utenganisho huu, bali Mambo ya Ndani na NIDA wanaamua kuunganisha jina lako la kwanza na la katikati kama jina lako la kwanza (given name).

Yaani, kama ulijaza form namna hii;

Jina la kwanza: Musa
Jina la katikati: Salum
Jina la Ukoo: Zengezenge

Passport au NIDA vitatoka Vikoonyesha hivi

Jina/Given name: Musa Salum
Jina la Mwisho: Zengezenge

Sasa mara kadhaa katika shughuli zako, nimekataliwa katakata kwamba mwenye jina sio mimi, baada ya kuandika jina langu la kwanza kama Musa, la la ukoo kama Zengezenge. Nikaambiwa mtu wanaemtaka jina lake la Kwanza ni Musa Salum. Nilijaribu kujiteteta lakini nikaambiwa system imenikataa!

Tatizo ni kwamba hata unapojaza form ambapo unatakiwa utoe forst name, middle name na surname, ni lazima uandike jina la kwanza kama majina mawili ili uendane na Passport au ID. Ukiandika moja unaambiwa huyu sio wewe. Sasa unajiuliza nikijaza jina la kwanza Musa Salum, jina la kati nijaze nini?

Na kumbuka mpangilio wa majina sasa unakuwa tofauti kwenye Passport /NIDA ID na kwenye cheti cha kuzaliwa.

Sasa hili ni jambo ambalo linapaswa kurekebishwa haraka. Kama Tanzania wanaona hakuna nafasi ya kuweka jina la kati kwenye Passport au ID basi wasiweke kabisa badala ya kuliunganisha na jina la kwanza na kufanya kila mtazania awe na majina mawili ya kwanza au given name.
Ulaya ya kaskazini kuna utaratibu wa kutumia majina mawili tu (lako na la ukoo) ila ukienda nchi za Kusini hususan Uhispania na Ureno (na nchi nyingi za amrika ya kati hadi Kusini) wanatumia majina matatu (kama Sisi Kwa kiasi fulani).
Kwa hiyo mkuu, wewe tumia jina lako na baba yako kama jina 1(LAKO) na la mwisho (la ukoo) libaki moja, inategemea na nchi uliyopo, ukiwa Uhispania/Ureno utatumia kama huku nyumbani.....
 
Kwa hiyo jina la kati nijitungie?

Halafu kumbuka cheti cha kuzaliwa kinaonyesha mpangilio tofauti, hakionyeshi jina langu ni Musa Salum bali Musa.
NID yangu
Jina la Kwanza, jina la pili,jina la ukoo
 
Nenda ardhi kasajili DEED POLL mzee. Watakusumbua kila uendapo. Binafsi nna majina matano kwenye IDs zangu zote isipokuwa cheti cha kuzaliwa.

Ili kuepuka usumbufu nilifuatilia DEED POLL.
 
Back
Top Bottom