allymshindo
New Member
- May 23, 2016
- 2
- 2
Nimetoka muda huu katika Terminal 3 ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, ambapo nililipa ada ya maegesho ya gari. Baada ya muda, nilipofika kwenye geti la kutokea, magari yalikuwa yakifuatana. Gari lililokuwa mbele yangu lilipita likitumia tiketi yangu kutokana na mfumo wa kamera kulisoma kama gari lililolipia.
Mtoa huduma wa getini alishindwa kutatua tatizo hilo na kuwasiliana na Control Room. Niliambiwa kuwa mfumo hauwezi kutoa one-time pass, hivyo nikalazimika kuambiwa nilipie tena licha ya kuwa tayari nilikuwa nimelipia parking.
Hili ni jambo la kushangaza kwa uwanja wa ndege wa kimataifa. Ikiwa tatizo limetokana na hitilafu ya mfumo na si kosa la mteja, kwa nini mteja ndiye anayelazimika kulipia tena?
Naomba wahusika wafanye maboresho katika mfumo wa parking, pamoja na kuwawezesha wahudumu wa getini kushughulikia changamoto kama hizi kwa haraka bila kumlazimisha mteja kulipia huduma mara mbili.