Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
kuna documentary moja niliicheki inaitwa money as debt. ziko tatu ila nimecheki mbili. pesa mara nyingi inavyoingizwa kwenye mzunguko huwa ni deni ambalo linatakiwa kurudi na faida. yaani ikiingia 1000 itatakiwa kurudi 1100,1200 au 1300 kulingana riba. pia inazungumzia historia ya pesa toka enzi za magoldsmith hadi modern banking. inaeleza jinsi mfumo wa pesa wa dunia ulivyo mbaya, mabenki yanavyo tengeneza faida out of nothing na jinsi yanahakikisha watu hawafundishi somo la jinsi pesa zinatengenezwa. itafute ni nzuri sana.
Nafikiri hii imejikita zaidi kwenye mikopo. Benki zina regulate mikopo kwa riba. Lakini gumzo hili limejikita zaidi katika kuangalia pesa zinawezaje kuwa sawia bila noti kupungua au kufurika katika uchumi. Hili ni swali tofauti kidogo (lakini muhimu) na habari ya benki kuu zinavyoweza kutumia monetary policy ku regulate inflation, unemployment and eventually economic growth.